Machapisho

NYANSAHO FOUNDATION YAZIDI KUHAMASISHA MAENDELEO BILLION 1.4 ZAKUSANYWA KWENYE HARAMBEE KIJIJI CHA MUSATI WILAYANI SERENGETI.

Picha
Na Jovina Massano, Serengeti.  KATIKA kuhakikisha jamii inapata huduma muhimu karibu na maeneo yao Nyansaho Foundation na wadau mbalimbali  wachangia Shillingi Billioni 1.4 zitakazowezesha upatikanaji wa huduma za afya na elimu Kijiji cha Musati. Harambee hiyo imefanyika hivi karibuni katika Kijiji cha Musati wilayani Serengeti mkoani Mara ambapo ilitanguliwa na uzinduzi wa kanisa la Waadventista wa Sabato- Musati Central na nyumba ya mchungaji ambavyo vyote kwa pamoja vimejengwa kwa ufadhili wa taasisi ya Nyansaho  kwa kiasi cha millioni 500. Akiongoza harambee hiyo Waziri wa Ujenzi ,Mh.Abdalah Ulega(MB) ameweza kukusanya jumla ya Shillingi Billioni 1.4 zitakazowezesha kujenga Shule pamoja na Zahanati katika Kijiji hicho. Katika harambee hiyo Waziri Ulega na rafiki zake wamechangia shillingi millioni 100 na kuongoza uchangiaji kutoka kwa wadau mbalimbali wa Maendeleo (wafanyabiashara) zikiwemo taasisi za fedha, wageni waalikwa na wananchi na kuweza kufikisha kiasi hicho ...

TABASAMU LA MATUMAINI: WANAFUNZI 16 KIFUBATA WAPATA NGUVU MPYA YA KUSOMA.

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Igunga.  KUNA nyakati ambapo msaada mdogo hugeuka kuwa mwanga mkubwa wa matumaini. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa wanafunzi 16 wanaoishi katika mazingira magumu wa Shule ya Sekondari Kifubata, Kata ya Nkinga, Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, baada ya kupokea msaada wa vifaa vya shule uliolenga kubadili simulizi ya changamoto zao za kila siku. Msaada huo umejumuisha mahitaji muhimu kama madaftari, kalamu, mabegi ya shule, masweta na sare, vitu ambavyo kwa wengi vinaweza kuonekana vya kawaida, lakini kwa wanafunzi hawa ni daraja muhimu kuelekea ndoto zao za kielimu. Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa taasisi ya Nkinga and Save Care Organisation, Edina Kalibate, alisisitiza umuhimu wa mshikamano wa jamii katika kusaidia makundi yenye uhitaji. "Mbunge wetu amekuwa akishirikiana kwa karibu na taasisi yetu kuwafikia watoto wenye mahitaji maalum pamoja na jamii inayowazunguka. Ushirikiano wa kila mmoja ni muhimu ili kuleta mabadiliko ya kweli,...

LISHE BORA SHULENI YATAJWA KUWA MSINGI WA MAFANIKIO YA ELIMU

Picha
  Na Jasmine Shamwepu, Dodoma KAMISHINA wa Elimu Tanzania, Dk Lyabwene Mtahabwa, amesema mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji hauwezi kufanikiwa bila kuwepo kwa huduma bora za chakula na lishe shuleni. Amesisitiza kuwa wadhibiti ubora katika halmashauri zote wanapaswa kuhakikisha chakula kinachotolewa kwa wanafunzi kinazingatia viwango vya ubora ili kuepusha madhara ya kiafya ikiwemo viriba tumbo. Dk Mtahabwa alitoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa mradi wa CRISP unaotekelezwa na SwissAid kwa miaka mitatu katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Dar es Salaam. Amesema maboresho ya elimu hayawezi kuleta matokeo chanya kama hayatazingatia lishe ya wanafunzi, akibainisha kuwa serikali imeweka sera na miongozo kuhakikisha shule zinatoa huduma ya chakula. “Mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji hatuwezi kufanikiwa bila kuwa na huduma bora za chakula na lishe,” amesema Dk Mtahabwa. Ameeleza kuwa serikali imechukua hatua mbalimbali kuimarisha lishe shuleni, ikiwemo waraka wa mwaka 2...

TUMUOMBEE RAIS, TULIOMBEE TAIFA-MASHILI

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Nzega.  WATANZANIA wamehamasishwa kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aweze kupata utulivu wa kuliongoza Taifa la Tanzania kwa amani, upendo na mshikamano. Rai hiyo imetolewa leo Aprili 19, 2026 na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya MASHILI COMPANY LIMITED ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mradi wa Uchenjuaji Dhahabu wa (Matinje Mining, Msilale Mining na Igurubi Mining) Ndg Peter Andrea Mashili aliposhiriki tamasha la Inland Festival lililoandaliwa na kanisa la Africa Inland Church Tanzania - AIC Wilayani Nzega mkoani Tabora. Mashili amesema kuwa Mhe Rais Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuifungua nchi na kuleta maendeleo hivyo ni jukumu la wananchi kuhakikisha wanamuombea ili aweze kuongoza kwa busara na mshikamano wa kitaifa. Pia Mashili amewataka viongozi wa dini na wananchi wote wa wilaya ya Nzega kumuombea Mbunge wa jimbo la Nzega Mjini Mhe Hussein Bashe ili aweze kuitumikia nafasi yake kwa ...

HAMISI KIM KOMANDO AWAPA COMPUTER MAKIBA SEKONDARI

Picha
  Na Mwandishi wetu, Arumeru.  MDAU wa madini ya Tanzanite, Hamisi Kim Komando ametoa zawadi ya kompyuta shule ya sekondari Makiba ya Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, kwa ajili ya matumizi ya masomo ya Tehama. Kim ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Makiba ameeleza hayo kwenye maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa shule hiyo mwaka 1996 na mahafali ya 15 ya kidato cha sita. Amesema anaiunga mkono shule hiyo kwa kununua kompyuta moja kwa ajili ya wanafunzi hao waboreshewe suala zima la Tehama. "Nawapongeza wanafunzi wote kwa kuhitimu kidato cha sita na ninawatakia kila la heri katika mtihani wenu mtakaofanya hivi karibuni," amesema Kim. Mkuu wa shule ya sekondari Makiba, Paul Kimaro amesema wameweka mikakati mbalimbali ya kukabiliana na changamoto ili wanafunzi wasome kidijitali kwa kutumia kompyuta. Kimaro amesema wanaendelea kutafuta wadau wa maendeleo, kuboresha usimamizi wa rasilimali zilizopo na kuhamasisha matumizi sahihi ya Tehama katika el...

MOKIA OLE MREFU AWATAKIA KILA LA HERI MAKIBA SEKONDARI

Picha
  Na Mwandishi wetu, Arumeru.  MWENYEKITI wa chama cha wafanyabishara wa madini Mkoa wa Manyara na kurugenzi ya Habari na Mawasiliano wa chama cha wafanyabishara wa madini Taifa (CHAMMATA) Mokia Ole Mrefu, amewajengea uwezo na kuwapa moyo wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya sekondari Makiba Wilayani Arumeru Mkoani Arusha, wanaotarajia kufanya mtihani wao wa kuhitimu hivi karibuni. Ole Mrefu amezungumza na wanafunzi hao kwenye maadhimisho ya miaka 30 tangu shule hiyo ianzishwe na mahafali ya 15 ya kidato cha sita kwa kuwatakia kila la heri katika mtihani wao wa kuhitimu. 'Hongereni sana vijana wetu jasiri wa kidato cha sita mnaojiandaa kuhitimu, leo nasimama kuwapa moyo na kuwakumbusha jambo moja muhimu: mmefika hapa si kwa bahati, bali kwa juhudi, nidhamu, na uvumilivu wenu," amesema Ole Mrefu . Ameeleza kwamba safari waliyoipitia imekuwa na changamoto nyingi, masomo magumu, mitihani ya majaribio, na nyakati za kuchoka, lakini bado mmesimama imara, hiyo peke yake ni ushin...