WAZIRI MKUU KUZINDUA MELI YA MV NEW MWANZA KESHO
Na Mwandishi Wetu, Mwanza. MELI ya MV.New Mwanza yenye uwezo wa kubeba abiria 1200 na tani 400 kwa pamoja katika Ziwa Victoria inatarajiwa kuzinduliwa kesho Januari 23, 2025 mkoani Mwanza huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba. Akizungumza leo na waandishi wa habari mkoani Mwanza, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema mpaka kukamilika kwa ujenzi wa meli hiyo zaidi ya Bilioni 120 zimetumika huku katika uongozi wa Serikali ya awamu ya sita zaidi ya Bilioni 79 zikitolewa. "Ina uwezo wa kubeba abiria 1,200 na tani 400 za mizigo, pamoja na magari makubwa 3 na magari madogo 20. Meli hii imeundwa kwa viwango vya kimataifa na ina urefu wa mita 92.6, karibu sawa na uwanja wa mpira wa miguu, na upana wa mita 17, ikiwa na kimo cha ghorofa nne," amesema. Profesa Mbarawa amesema hadi sasa meli ya MV New Mwanza tayari imeshafanya jumla ya safari sita (6) kati ya Mwanza na Bukoba kupitia Kemondo. "Katika safari hizo, meli imebeba jumla ya abir...