Machapisho

SERIKALI YASHAURIWA KUVIPA RUZUKU VYOMBO VYA HABARI

Picha
Na Mwamdishi Wetu, WAHARIRI nchini, wameishauri serikali kuvipa ruzuku Vyombo vya Habari ili vifanye kazi kwa ufanisi zaidi. Akizungumza kwenye semina ya siku moja iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) leo, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile alitoa kauli hiyo iliyoungwa mkono na Wahariri wenzake. “Hatuwezi kufanya kazi vizuri bila kuwezeshwa, tuachane na kutoka mataifa ya nje kwamba, serikali ikiwezesha Vyombo vya Habari, havitakuwa huru. “Tunaonaje aibu kuviwezesha Vyombo vya Habari ili vijenge miundombinu ya fikra ili watu wasichome nchi yao? Mbona Vyama vya Upinzani vinapewa ruzuku na bado vinaisimamia serikali bila kuyumbishwa?” amesema Balile. Balile alitoa kauli hiyo baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Hamis Masauni kushauri Vyombo vya Habari kuelimisha wananchi hususani vijana kuhusu faida na fursa zilizopo ndani ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

CHUO CHA UHASIBU ARUSHA MABINGWA SHIMIVUTA

Picha
Na Allan Kitwe, Tabora CHUO cha Uhasibu Arusha (IAA) kimetwaa ubingwa wa jumla wa mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Vyuo Vikuu Tanzania (SHIMIVUTA) yaliyomalizika jana katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wavulana Tabora. IAA imetwaa ubingwa huo baada ya kushika nafasi ya kwanza kati ya vyuo vikuu 16 vilivyoshiriki mashindano hayo mwaka huu kati ya Vyuo Vikuu 25 wanachama wa Shirikisho hilo. Chuo hicho kimekuwa mshindi wa kwanza katika mchezo wa riadha, draft, bao, mpira wa mikono, wavu na kushika nafasi ya pili katika michezo ya pool table, pete, kikapu na nafasi ya tatu kwenye karata. Rais wa Shirikisho hilo Juhudi Elirehema Sam ameeleza kufurahishwa na mashindao ya mwaka huu kutokana na ushindani mkubwa ulikuwepo na kuahidi kuwa mwakani maandalizi yatakuwa makubwa zaidi ya hapo. Amesistiza kuwa licha ya viwanja kujaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini timu zote zilicheza kwa ustadi mkubwa na kuonesha vipaji vya hali ya juu. Akihitimisha mashindano hayo jana...

SERIKALI YATOA MWELEKEO MPYA KATIKA UWEKEZAJI VIWANDA VYA BIDHAA ZA AFYA NCHINI

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam SERIKALI imetangaza rasmi mwelekeo mpya wa kimkakati wa kuharakisha uwekezaji wa viwanda vya bidhaa za afya nchini ikiwa ni lengo la kuimarisha usalama wa afya wa nchi, kupunguza utegemezi wa dawa, na kuliweka taifa kwenye ramani ya uzalishaji wa dawa barani Afrika na Duniani. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Desemba 23, 2025 katika kikao cha wazalishaji wa dawa na bidhaa za afya pamoja na uzinduzi wa kikosi kazi cha uharakishaji mchakato wa uwekezaji wa viwanda vya dawa nchini kilichofanyika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dar es Salaam. “Ujenzi wa viwanda vya dawa si mpango wa majaribio bali ni uamuzi wa kimkakati uliokwisha amuliwa na Serikali, usalama wa afya wa Taifa hauwezi kujengwa kwa kutegemea uagizaji wa dawa pekee, bali unahitaji uzalishaji wa ndani unaokidhi viwango vya kimataifa” amesema Waziri Mchengerwa. Amebainisha kuwa Serikali imeanzisha mfumo maalum wa uharakishaji wa uwekezaji nchini kupitia...

EWURA, TRA KUIMARISHA USHIRIKIANO

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma. WATENDAJI wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na wenzao wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), leo 23 Desemba 2025, wamekutana na  kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano wa utendaji hususani katika usimamizi wa masuala ya kikodi yanayotokana na huduma zinazodhibitiwa na EWURA.  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bwana Gerald Maganga, amesema EWURA ni mshirika mzuri katika kuisaidia TRA kutekeleza wajibu wake wa usimamizi wa kodi nchini.  “Ushirikiano uliopo kati ya taasisi hizi mbili, utatupeleka mbele, tuudumishe na tusimamie utekelezaji wa makubaliano yetu,” alisema.  Meneja wa TRA mkoa wa Dodoma, Bwana Pendolake Elinisafi, ameishukuru EWURA kwa kuipatia TRA ushirikiano mzuri, na kuahidi kuuendeleza ili kuweka msingi imara wa mafanikio ya taasisi hizo mbili na taifa kwa ujumla.

UONGOZI WA APRM WAKUTANA NA VIONGOZI WA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam. KATIBU Mtendaji wa Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa Afrika wa Kujitathmini kwa Vigezo vya Utawala Bora (APRM) Tanzania, Bw. Lamau Mpolo, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini. Lengo la kikao hicho lilikuwa kujadili nafasi ya vijana katika kukuza dhana ya Utawala Bora kama nguzo muhimu ya kuimarisha amani na usalama nchini Tanzania. Katika kikao hicho, Bw. Mpolo alisisitiza umuhimu wa ushiriki wa vijana katika masuala ya utawala, akieleza kuwa vijana ni rasilimali muhimu katika kujenga jamii yenye uwajibikaji, uwazi na maamuzi jumuishi. Kikao hicho cha siku moja kilifanyika Desemba 22, 2025, katika Ofisi za APRM zilizopo katika jengo la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, jijini Dar es Salaam.

KATAMBI AAGIZA KULINDWA USHINDANI WA HAKI, AKEMEA UKIRITIMBA WA BEI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Patrobas Katambi (Mb), ameliagiza Baraza la Ushindani (FCT) kuendelea kusimamia na kulinda ushindani wa haki ili kuondoa vitendo vya ukiritimba, hususan katika suala la kupandisha bei za bidhaa na huduma. Ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika Baraza la Ushindani Desemba 22, 2025 Jijini Dar es Salaam akisisitiza kuwa ushindani wa haki ni msingi muhimu wa ukuaji wa biashara, kwani vitendo vya ukiritimba vimekuwa vikiathiri biashara nyingi na walaji. Ameeleza kuwa biashara zinapaswa kufanyika kwa kuzingatia ulinzi wa walaji, ambapo bei za bidhaa na huduma ziwe za haki, bidhaa ziwe na ubora, na uchunguzi wowote ufanyike kwa haki na kwa kuzingatia misingi ya kisheria. Mhe. Katambi amebainisha kuwa Serikali inaendelea kuhamasisha uwekezaji kwa kuboresha sera rafiki, kufanya marekebisho ya sheria na kuendelea na maboresho ya mazingira ya biashara ili kuhakikisha Tanzania inakuwa mahali salama na rafiki kwa kufanya...

FCC YANG’ARA KATIKA KONGAMANO LA 16 LA WATAALAMU WA MANUNUZI NA UGAVI

Picha
Na.Mwandishi, Wetu. TUME ya Ushindani (FCC) imetunukiwa tuzo maalum ya kutambua mchango wake katika maendeleo ya Sekta ya Manunuzi na Ugavi nchini. Tuzo hiyo imekabidhiwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mshamu Munde, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, na kupokelewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha FCC, Bi. Roberta Feruzi. Hafla ya utoaji wa tuzo hiyo ilifanyika katika Kongamano la 16 la Wataalamu wa Manunuzi na Ugavi, lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), jijini Arusha lililoandaliwa na Bodi ya Wataalamu na Mafundi wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB). FCC imeshiriki kongamano hilo kama mdau muhimu wa sekta ya manunuzi na ugavi, ambapo iliwasilisha mada kuhusu umuhimu wa ushindani wa haki katika masuala ya manunuzi na ugavi, hususan katika kulinda mnyororo wa thamani. Kupitia kongamano hilo, Tume pia ilitoa elimu kwa wadau mbalimbali kuhusu majukumu na kazi zake, ikisisitiza nafasi yake katika kuhakikisha mazingira ya ushindani yanayochochea uwazi, ufanisi na ...

ELIMU YA USHINDANI YAONGEZA UWAZI KWA WAFANYABIASHARA MBEYA

Picha
Na.Mwandishi Wetu. BARAZA la Ushindani (FCT) jana Desemba 18, 2025, limeendesha semina ya elimu kwa wadau mkoani Mbeya kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu majukumu na huduma zinazotolewa na Baraza hilo. Semina hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na kufunguliwa na Katibu Tawala Msaidizi – Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mkoa wa Mbeya, Bi Anna Mwambene, ambaye aliwahimiza wadau kutumia ipasavyo mifumo ya kisheria iliyopo na kuwa mabalozi wa kuitangaza huduma za Baraza la Ushindani. Bi Mwambene alisema uelewa wa sheria na taratibu za ushindani ni muhimu katika kukuza mazingira bora ya biashara na uwekezaji, akisisitiza umuhimu wa wadau kushiriki kikamilifu katika kulinda haki zao kwa kutumia mifumo rasmi iliyowekwa na Serikali. Katika semina hiyo, Baraza la Ushindani liliwapatia washiriki elimu kuhusu matumizi ya mfumo wa kidijitali wa kuwasilisha rufaa zinazotokana na maamuzi ya Tume ya Ushindani (FCC) pamoja na mamlaka mbalimbali za udhibiti, zikiwemo LATRA, E...

TAKA ZAWAKELA WAFANYABIASHARA SOKO LA SABASABA DODOMA

Picha
  Na Hamida Ramadhani, Dodoma. WAFANYABIASHARA  wa soko la matunda na mbogamboga Sabasaba jijini Dodoma wameliomba Jiji la Dodoma kuondoa takataka zilizojaa katika dampo lililopo ndani ya soko hilo, wakisema hali hiyo inahatarisha afya zao. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, watanyabiashara hao wamesema dampo hilo limejaa kupita kiasi na takataka kushindwa kuondolewa kwa wakati, hali inayosababisha harufu kali na mazingira machafu, jambo linalodaiwa kuchangia baadhi yao kuugua maradhi mbalimbali yakiwemo ya mfumo wa hewa. Paulina, maarufu kama Mama Kibibi, ni mmoja wa wafanyabiashara sokoni hapo. Anasema hali ya taka kujaa kwa muda mrefu imemletea matatizo ya kiafya, hali inayomfanya ashindwe kufanya shughuli zake ipasavyo. Kwa upande wake, Agaudence Temba, mfanyabiashara wa matunda katika soko hilo, ameuomba uongozi wa Jiji la Dodoma kukaa meza moja na wafanyabiashara ili kutafuta suluhisho la kudumu. Anapendekeza kuwepo kwa mchango wa shilingi mia mbili kwa siku kutoka kwa wa...

JAFO ARIDHISHWA NA UJENZI WA MABWENI NA MADARASA SHULE YA SEKONDARI DK. SELEMANI JAFO

Picha
Na.Mwandishi Wetu-KISARAWE. MBUNGE wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo, ameridhishwa na hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa mabweni mawili na madarasa katika Shule ya Sekondari Dkt.Selemani Jafo, na kuhimiza Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kuhakikisha mradi huo unakamilika mapema ili ifikapo Januari 2026 shule hiyo iweze kupokea wanafunzi wa bweni. Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani Kisarawe, Dkt. Jafo amesema ziara hiyo ni sehemu ya kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hususan katika sekta ya elimu. “Tumeendelea na ziara yetu ya kuhakikisha tunasukuma utekelezaji wa ilani wilayani Kisarawe, na eneo kubwa tulilolipa kipaumbele ni uimarishaji wa sekta ya elimu. Hapa Shule ya Sekondari Selemani Jafo kuna kazi kubwa inaendelea, ikiwemo ujenzi wa mabweni mawili na madarasa ili kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu,” amesema. Dkt. Jafo amepongeza usimamizi wa mradi huo, akieleza kuwa ujenzi umefikia zaidi ya asil...