TAKA ZAWAKELA WAFANYABIASHARA SOKO LA SABASABA DODOMA

 


Na Hamida Ramadhani, Dodoma.

WAFANYABIASHARA  wa soko la matunda na mbogamboga Sabasaba jijini Dodoma wameliomba Jiji la Dodoma kuondoa takataka zilizojaa katika dampo lililopo ndani ya soko hilo, wakisema hali hiyo inahatarisha afya zao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, watanyabiashara hao wamesema dampo hilo limejaa kupita kiasi na takataka kushindwa kuondolewa kwa wakati, hali inayosababisha harufu kali na mazingira machafu, jambo linalodaiwa kuchangia baadhi yao kuugua maradhi mbalimbali yakiwemo ya mfumo wa hewa.

Paulina, maarufu kama Mama Kibibi, ni mmoja wa wafanyabiashara sokoni hapo. Anasema hali ya taka kujaa kwa muda mrefu imemletea matatizo ya kiafya, hali inayomfanya ashindwe kufanya shughuli zake ipasavyo.

Kwa upande wake, Agaudence Temba, mfanyabiashara wa matunda katika soko hilo, ameuomba uongozi wa Jiji la Dodoma kukaa meza moja na wafanyabiashara ili kutafuta suluhisho la kudumu.

Anapendekeza kuwepo kwa mchango wa shilingi mia mbili kwa siku kutoka kwa wafanyabiashara ili kusaidia uondoaji wa taka mara kwa mara.

Akizungumzia suala hilo, John Lugendo, Afisa Afya wa Mazingira, amesema changamoto ya taka kujaa inachangiwa pia na baadhi ya wafanyabiashara kutupa ovyo taka zisizoruhusiwa katika dampo hilo.







Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.