MTINDO BORA WA MAISHA _ LISHE ASILIA.
Maelezo ya Kikundi (Group Description): MTINDO BORA WA MAISHA LISHE ASILIA ni jukwaa la kidigitali lililoanzishwa na Mtaala Mr Roghat Falme Robert kwa ushirikiano na wataalamu wa Lishe, afya na kilimo na kwa sasa tunao mabalozi tunaowaandaa. Kauli Mbiu “Nourish to Flourish Lisha Mwili, Kuza Maisha.” Lengo kuu ni kuhamasisha ulaji wa chakula bora, kuboresha usalama wa chakula majumbani, na kukuza tabia njema za lishe kwa watu binafsi na jamii. Tunalenga kuwawezesha watu kupata maarifa na zana zinazowawezesha kufanya maamuzi sahihi ya lishe ili kuishi maisha yenye afya na ustawi. Malengo (Objectives) Kuelimisha na kuhamasisha kuhusu ulaji bora wa chakula. Kuboresha usalama wa chakula majumbani kwa kutoa rasilimali na msaada. Kukuza tabia njema za lishe kwa watu binafsi na jamii. Kutoa jukwaa la fursa halisi za ajira katika sekta ya kilimo na afya. Kutoa nafasi za matangazo kwa biashara zinazohusiana. Dira (Vision) Dunia ambayo watu na jamii wanapata chakula chenye lishe, elim...