SALOME MNYAWI MITANO TENA KWAKE MIRERANI
Na Mwandishi wetu, Mirerani MGOMBEA Udiwani wa Kata ya Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Salome Nelson Mnyawi, amewaomba wakazi wa eneo hilo kumpa kura nyingi za ndiyo kwani amefanikisha maendeleo mengi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Salome akizungumza kwenye eneo la Maduka Matatu, Mtaa wa Twiga, Kata ya Mirerani, amesema alichaguliwa kwa mara ya kwanza kipindi kilichopita hivyo anaomba kipindi kingine cha miaka mitano ili aweze kushirikiana nao kufanikisha maendeleo ya eneo hilo. Ameeleza baadhi ya mafanikio yaliyofanyika kwenye kipindi chake ni ujenzi wa kituo cha afya Tanzanite ambapo kimekamilika na sasa kinasubiria kufunguliwa na kutoa huduma kwa jamii. "Pia miundombinu ya barabara za lami kutoka soko la getini hadi lango la kuingia na kutoka ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite pamoja na taa na barabara kutoka transifoma hadi kituo cha mafuta cha Kibobo," amesema Salome. Amesema sekta ya elim...