DKT. MATARAGIO AAGIZA VIFAA VYOTE VYA UHAKIKI WA JOTOARDHI ZIWA NGOZI KUFIKA KWA WAKATI
Ni baada ya kukagua mradi na kukuta baadhi ya vifaa bado havijafika Asisitiza mradi kukamilika kwa wakati ikiwa ni utekelezaji wa Sera ya Nishati ya mwaka 2015 Kazi ya uhakiki wa Jotoardhi Ziwa Ngozi yafikia asilimia 60. Na Mwandishi Wetu, Mbeya. NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Kampuni yake Tanzu ya Uendelezaji Jotoardhi (TGDC) kuhakikisha kuwa vifaa vyote vya uhakiki wa rasilimali Jotoardhi katika mradi wa Ziwa Ngozi vinafika kwa wakati ili kazi za uhakiki ziweze kumalizika kulingana na muda uliopangwa. Dkt. Mataragio ametoa maagizo hayo leo Oktoba 22, 2025 wakati wa ziara yake ya kukagua kazi zinazoendelea kutekelezwa katika mradi huo wilayani Rungwe mkoani Mbeya. “Huu mradi mnapaswa kuukamilisha kwa wakati kutokana na umuhimu wake nchini, tunapotekeleza miradi hii ya Jotoardhi tukumbuke kuwa tunatekeleza pia Sera ya Taifa ya Nishati ya Mwaka 2015 ambayo inasema Tanzania in...