Machapisho

WANAWAKE WA TEMEKE WAANZA SHAMRASHAMRA ZA KUMPOKEA MGOMBEA WA URAIS DKT. SAMIA

Picha
Na Hamida Ramadhani, Dar es Salaam. MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) ambaye pia ni Mratibu wa Kampeni za CCM Jijini DSM, Leo tarehe 19 Oktoba, 2025, apokelewa na matembezi ya Wanachama wa UWT Wilaya ya Temeke yaliyoambatana na Ngoma kuelekea kwenye Ukumbi wa Taifa Pub, Kata ya Mibulani, kwa lengo la kufanya Kikao na wajumbe wa Baraza la UWT Wilaya ya Temeke, ili kujiweka sawa na Mapokezi ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombe Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), katika kufanya Mikutano ya Kampeni ndani ya Jiji la DSM, na kunadi ilani ya CCM 2025/2030 na kuomba kura za ndiyo kwa Wananchi kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025.   (

CHATANDA AWAHAMASISHA WANAKIGAMBONI OKTOBA 29, 2025 KWENDA KUPIGA KURA NA KUMCHAGUA DKT. SAMIA

Picha
Na Hamida Ramadhani, Dar es Salaam. MENYEKITI wa UWT Taifa, Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) ameambatana na Katibu Mkuu wa UWT Taifa, Ndg. Suzan Peter Kunambi (MNEC). leo tarehe 18 Oktoba, 2025, katika Viwanja vya Tungi Mnadani, Wilaya ya Kigamboni, amewaomba wananchi wa Kigamboni kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la kupiga kura Oktoba 29, 2025, na kuhakikisha wanapiga kura kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na wagombea wa Ubunge na Udiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).  Aidha, Chatanda amewahimiza wananchi, hususani vijana wa Jimbo la Kigamboni, kutobabaishwa na Wagombea Wengine kwasababu Dkt. Samia amejipambanua kwa Kazi zake. Kauli hiyo aliitoa wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kushiriki Bonanza la Mazoezi ya Kutembea (Jogging) na Michezo Mbalimbali lililoandaliwa na Ofisi ya  Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Ndg. Dalmia Mikaya.

VIONGOZI WA VYAMA VYA USHIRIKA IGUNGA WAPATIWA MAFUNZO YA UONGOZI NA USIMAMIZI VYAMA VYA USHIRIKA.

Picha
  Na Lubango Mleka, Igunga - Tabora. KATIKA kuhakikisha kuwa vyama vya ushirika vinaendeshwa kwa weledi na kuzingatia sheria, Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Tabora (IGEMBENSABO) kimeandaa mafunzo ya siku nne kwa viongozi wa vyama vya ushirika wilayani Igunga. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Kaimu Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tabora, Jerude Juma Magubiko, amewataka viongozi hao kufuata sheria, kanuni na misingi ya ushirika katika kuendesha vyama vyao. Kwa upande wao, viongozi wa IGEMBENSABO waliowezesha mafunzo hayo wametoa wito kwa washiriki kuyachukulia kwa uzito mkubwa ili wawe mabalozi wa mabadiliko ndani ya vyama vyao. Washiriki wa mafunzo hayo kutoka vyama mbalimbali vya ushirika (AMCOS) wilayani Igunga wameeleza kufurahishwa na mafunzo hayo, wakisema yatawasaidia kuimarisha utendaji wa kila siku. Huku baadhi yao wakitoa maoni yao ni pamoja na Adelina Blazi (Katibu Meneja Balimi AMCOS), Maria Ramadhani Makamu Mwenyekiti  Mwamapuli AMCOS...

CHATANDA AWAOMBA WAJASIRIAMALI NA MAKUNDI MAALUM KUMPIGIA KURA DKT. SAMIA

Picha
  Na Hamida Ramadhani, Dar es Salaam MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania, Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), leo tarehe 17 Oktoba 2025, ameshiriki Mkutano wa Makundi Maalum ya Wajasiriamali Mkoa wa Dar es Salaam, amewataka kumchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan ifikapo Oktoba 29, 2025, ili aendelee kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2025–2030. Katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa,  Chatanda amepongeza uongozi wa Dkt. Samia  kwa mafanikio makubwa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na ya kimkakati, nchini tanzania.