DKT. HUSSEIN ALI MWINYI AZINDUA SOKO LA KISASA CHUINI ZANZIBAR
RAIS wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amezindua soko la kisasa la wafanyabiashara Chuini, lililopo Wilaya ya Magharibi A. Soko hilo limejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 43 na lina uwezo wa kutoa ajira kwa wananchi 4000 na kuchangia ukuaji wa uchumi wa eneo hilo. Akizungumza wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa soko hilo, Rais Mwinyi amesema malengo makuu ya serikali ni kuhakikisha wafanyabiashara wanapata mazingira mazuri ya kufanya biashara, huku wakichangia maendeleo ya kiuchumi na kutengeneza fursa za ajira kwa jamii. Ameahidi kuwa serikali itaendelea kuwekeza katika miradi inayoongeza tija na ustawi wa wananchi.