Machapisho

AKILI UNDE YATAWALA MKUTANO WA KAHRDC NA FAC

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.  MKURUGENZI wa Masuala ya Kisekta wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Mwesigwa Felician akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Kamati ya Utawala (HRDC) na Fedha (FAC) ya Shirika la Wasimamizi wa Huduma za Mawasiliano wa Nchi zilizopo kusini mwa Afrika (CRASA), tarehe 25 Agosti, 2025 jijini Dar es Salaam.  Katika ufunguzi wa mkutano huo, wajumbe wameshiriki majadiliano kuhusu matumizi ya Akili Unde kwa wataalamu wa rasilimali watu “ Artificial Intelligence for Human Resources Professionals”.   Mkutano huo unaoratibiwa na TCRA unafanyika kuanzia Agosti 25 hadi 29, katika ukumbi wa mikutano wa Hotel ya Serena. #tcratz #digitaleconomy #crasa #regionalintegration #uchumiwakidijiti #hrdc #fac

MAANDALIZI YA KUELEKEA MIAKA 64 YA MAGEREZA YAKAMILIKA.

Picha
MAANDALIZI yamekamilika kuelekea kilele cha maadhimisho ya Miaka 64 ya Jeshi la Magereza Baada ya Uhuru, ambayo yatafanyika Agosti 26, 2025 katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga Dar Es Salaam, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

KEMBAKI AWATAKA WAJUMBE KUWA WATULIVU NA KUWA NA MSHIKAMANO

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma  WANANCHI wa Tarime Mjini wametakiwa kuwa watulivu na kuendelea kuwa na mshikamano, kufuatia kukamilika kwa mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliolenga kumpata mgombea atakayewakilisha chama hicho katika uchaguzi ujao. Kauli hiyo imetolewa leo, Agousti 25 ,2025 jijini Dodoma na aliyekuwa Mbunge wa Tarime Mjini kwa tiketi ya chama cha mapinduzi Michael Kembaki ,alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatima ya mchakato wa kura za maoni na mwelekeo wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu. Kembaki, ambaye amemaliza muda wake wa miaka mitano bungeni, amewashukuru wananchi wa Tarime kwa ushirikiano waliompa wakati wa uongozi wake, pamoja na wajumbe waliompa kura katika kura za maoni. Katika mchakato huo, Kembaki alipata kura ,5572,  Hata hivyo, anasema kuwa chama kilifanya maamuzi yake kupitia ngazi mbalimbali kuanzia vikao vya kata, wilaya, mkoa hadi taifa na hatimaye kumpitisha mgombea mwingine kupeperusha bendera ya ...

RAIS MWINYI ATUNUKIWA PHD YA UCHUMI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu (PhD Honoris Causa) ya Uchumi iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU), ambayo ilitangazwa rasmi Desemba 2024 katika mahafali ya Chuo hicho. Mkuu wa Chuo hicho, Mhandisi Abdulqadir Othman Hafez, alikabidhi rasmi Shahada hiyo kwa Rais Dkt. Mwinyi Ikulu Zanzibar leo tarehe 25 Agosti, 2025. Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amekipongeza Chuo hicho kwa kuthamini na kutambua juhudi zake katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya Zanzibar, hatua ambayo ameieleza kuwa itamwongezea ari ya kuendeleza maendeleo zaidi nchini.

RAIS MWINYI AKUTANA NA WANAFUNZI WATAKAOITEMBELEA NASA, MAREKANI NA KUHUDHURIA HACKATHON, OMAN

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za kuwaandaa vijana wengi zaidi wa Zanzibar kuwa wataalamu wa elimu ya anga. Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na wanafunzi watano waliochaguliwa kutembelea makao makuu ya NASA yaliyopo Washington D.C., Marekani, pamoja na kushiriki katika mashindano ya NASA International Space Apps Challenge 2025 yatakayofanyika jijini Ibra, Oman. Mkutano huo umefanyika Ikulu Zanzibar leo tarehe 25 Agosti 2025. Fursa hiyo imetokana na uwezo mkubwa waliouonesha waliposhiriki katika programu ya Kimataifa ya IASC (International Astronomical Search Collaboration) inayohusu uvumbuzi wa asteroids kwa kushirikiana na NASA (National Aeronautics and Space Administration) ya Marekani.  Jumla ya wanafunzi 22 kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Karume, Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar na Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al-Sumait ambao ...

CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE 2025 BAADHI YA VINARA WA KURA ZA MAONI WAACHWA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) kimetangaza orodha ya makada waliopitishwa kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 baada ya mchujo uliofanywa na vikao vya juu  vya chama hicho.  Wakati baadhi ya majina yakiendelea na safari ya kisiasa, waliokuwa vinara kwenye kura za maoni wamejikuta wakiondolewa katika hatua za mwisho. Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Itikadi, Uenezi na Mafunzo Amos Makalla amesema uteuzi huo umefanywa na vikao vya maamuzi vilivyoongozwa na Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan. Makalla amesema baadhi ya waliokuwa wakiongoza kwenye kura za maoni lakini majina yao hayakurudishwa ni pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Tanga Mjini Ummy Mwalimu na Samuel Malecela ambaye aliongoza kura za maoni katika Jimbo la Dodoma Mjini. Katika Jimbo la Kigoma Mjini, chama kimempitisha Clinton Revocutus maarufu kama Baba Leo licha ya kutoshinda katika kura za maoni. Hali ...

CHAMA CHA MAPINDUZI CCM TAIFA CHATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA NAFSI YA UBUNGE 2025 NA WATEULIWA WA NAFASI MBALI MBALI NDANI YA CHAMA HICHO.

Picha
 

BODI YA USHAURI TARURA YAIPA HEKO SERIKALI UJENZI DARAJA LA MOHORO

Picha
Na Mwandishi Wetu, Rufiji.  MWENYEKITI wa Bodi ya Ushauri ya Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Florian Kabaka ameishukuru Serikali kwa kuwezesha Wakala huo kutekeleza ujenzi wa daraja la Mohoro lenye urefu wa Mita 100 wilayani Rufiji. Mhandisi Kabaka ameyasema hayo wakati wa ziara ya kutembelea ujenzi wa daraja hilo pamoja na ujenzi wa barabara za lami zenye urefu wa Km. 4 zinazojengwa katika mji wa Ikwiriri wilayani humo. “Niipongeze serikali kwa uwezeshaji huu kwa TARURA, kwakweli uwepo wake hata wananchi wanaishukuru kwa kufungua miundombinu kila mahali, nitoe heko kwa serikali kwa kuendelea kutoa fedha kwa TARURA pia nitoe heko kwa menejimenti ya TARURA kwa usimamizi”. Aidha, amewataka wananchi wa eneo hilo kulitunza daraja hilo pamoja na vifaa vyote vinavyozunguka, pia kutochezea tuta la daraja hilo kwani linaenda kuleta uhakika wa mawasiliano yao kwa mwaka mzima hususan kipindi cha mvua. “Daraja hili linaenda kuwaondolea shida iliyodumu kwa miaka min...