CCM YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE 2025 BAADHI YA VINARA WA KURA ZA MAONI WAACHWA
Na Mwandishi Wetu, Dodoma. CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) kimetangaza orodha ya makada waliopitishwa kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 baada ya mchujo uliofanywa na vikao vya juu vya chama hicho. Wakati baadhi ya majina yakiendelea na safari ya kisiasa, waliokuwa vinara kwenye kura za maoni wamejikuta wakiondolewa katika hatua za mwisho. Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayeshughulikia Itikadi, Uenezi na Mafunzo Amos Makalla amesema uteuzi huo umefanywa na vikao vya maamuzi vilivyoongozwa na Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan. Makalla amesema baadhi ya waliokuwa wakiongoza kwenye kura za maoni lakini majina yao hayakurudishwa ni pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Tanga Mjini Ummy Mwalimu na Samuel Malecela ambaye aliongoza kura za maoni katika Jimbo la Dodoma Mjini. Katika Jimbo la Kigoma Mjini, chama kimempitisha Clinton Revocutus maarufu kama Baba Leo licha ya kutoshinda katika kura za maoni. Hali ...