Na Mwandishi Wetu, Antananarivo. MKUTANO wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umehitimishwa jijini Antananarivo Agosti 17, 2025, huku viongozi hao wakihimizana, umoja, mshikamano na ushirikiano kama njia ya msingi ya kujikwamua kiuchumi na kukabiliana na changamoto zinazoibuka kila siku ulimwenguni. Katika mkutano huo, Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan aliwakilishwa na Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor Mpango, na kama ilivyo ada, mwenyeji wa mkutano huo, Madagascar alikabidhiwa uenyekiti wa jumuiya hiyo kutoka Zimbabwe. Mkutano huo ulihudhuriwa na wakuu wa nchi 9 ambapo Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, mwenyekiti aliyopekea kijiti, Katibu Mtendaji wa SADC na wakuu wa nchi wanne wa Botswana, Namibia, Msumbiji na Mauritius kutokana na kushiriki kwao kwa mara ya kwanza kama wakuu wa nchi walipata fursa ya kuhutubia mkutano huo. Hotuba za viongozi hao ziligusia maeneo makubwa manne ambayo ni amani na usalama, ujenzi wa miundombinu, uchumi, demokrasia n...