Machapisho

NAIBU WAZIRI SANGU AONGOZA KURA ZA MAONI JIMBO LA KWELA

Picha
  Na. Mwandishi Wetu- Sumbawanga ALIYEKUWA Mbunge wa Kwela mkoani Rukwa, Mhe.Deus Sangu ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na  Utawala Bora ameongoza kura za maoni jimboni humo na kuwaacha mbali wapinzani wake wanne  katika mchakato huo. Matokeo yaliyotangazwa mapema leo  Jumanne  Agosti 6, 2025 Mhe.Sangu  amepata kura 9,957,  dhidi ya Justin Hiari aliyepata kura 2,973,  Derick Sikale kapata 507,  Walter Simsokwe kapata 112  na Yuster Bahati  kaambulia kura  102 Taarifa za matokeo hayo zinaeleza kuwa jumla ya Wajumbe 13,496 walipiga  kura   ambapo kura halali zilikuwa 13,278 na kura 218  ziliharibika.

NDIYO MATOKEO MAJIMBO YA IGUNGA

Picha
 

MHE. DOTTO BITEKO ASHINDA KWA ASILIMIA 99.8

Picha
IDADI YA WAPIGA KURA JIMBO LA BUKOMBE - GEITA NI 7,845.  = Wajumbe waliohudhuria 7456.  = Wajumbe wasiohudhuria 389.  Idadi ya kura zilizopigwa 7456.  = Idadi ya kura zilizoharibika 15.  = Idadi ya kura halali 7441.  ✅ KURA ZA NDIO 7441.  = KURA ZA HAPANA 00.  *WASTANI WA WAPIGA KURA WALIOJITOKEZA NI ASILIMIA 95.04.  *WASTANI WA USHINDI NI ASILIMIA 99.8. @BUKOMBE @BITEKO @CCMTAIFA

WASIMAMIZI WASAIDIZI NGAZI YA KATA JIMBO LA MANONGA NA IGUNGA WATAKIWA KUENDELEZA UTENDAJI WAO KIUADILIFU. MSIMAMIZI wa

Picha
Na Mwandishi Wetu, Igunga.  MSIMAMIZI wa Uchaguzi Jimbo la Igunga na Manonga wilayani Igunga mkoani Tabora, Hamisi Hamisi amewaasa Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya kata kuendeleza utendaji wao wa kiuadilifu, uaminifu, uzalendo, uchapakazi na uaminifu. Hamisi ametoa rai hiyo wakati wa mafunzo kwa Wasimamizi hao yaliyofanyika katika ukumbi wa Maxweli mjini Igunga. “Nyinyi mliopo hapa mmeteuliwa kwa mujibu wa sheria, hivyo mnaowajibu wa kikatiba na sheria kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani katika maeneo yenu’’ amesisitiza. Aidha, amewakumbusha wamebeba dhamana kubwa, nyeti na muhimu kwa mustakabali wa Tanzania Bara, hivyo wanategemewa kuzingatia utendaji wao na kuwajibika ipasavyo kipindi chote cha utumishi wao katika Tume Huru ya Uchaguzi.

MATUKIO KATIKA PICHA.

Picha
 Wajumbe wa CCM Kata ya Igunga wakiwa katika zoezi la upigaji kura ya maoni kwa nafasi ya Ubunge na Udiwani linalo endelea  katika ukumbi wa Sakao Igunga mjini .

MATUKIO KATIKA PICHA.

Picha
 Katibu wa Jumuia ya Wazazi CCM Wilaya ya Igunga Bi. Aziza Kiyabo ambaye ni Msimamizi wa Uchaguzi Kura za Maoni Kata ya Igunga akitoa maelekezo kwa Wajumbe kabla ya ziezi la upigaji kura za maoni kuanza.

HABARI PICHA KUTOKA UKUMBI WA SAKAO IGUNGA

Picha
  WAJUMBE KUTOKA MATAWI 9 YA KATA YA IGUNGA WAKIWA TAYARI KUPIGA KURA YA MAONI KUPATA MBUNGE NA MADIWANI KWA TIKETI YA CCM JIMBO LA IGUNGA. 

MADALALI WA MINADA WATAKIWA KUJISAJINI KIELEKTRONIKI.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  WIZARA ya Fedha imeandaa Mfumo wa Kielektroniki wa utoaji Leseni za Udalali na Uendeshaji minada ya hadhara unaowezesha uombaji na upatikanaji wa Leseni kwa njia ya kielektroniki kwa kutumia simu za mkononi au kompyuta mpakato ili kuwaondolea wananchi adha na gharama ya kufuata leseni hizo jijini Dodoma. Akizungumza wakati akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Jijini Dodoma, Msimamizi wa Mali za Serikali wizarani hapo, Bw. George Killo, alisema Mfumo huo utamuwezesha mwananchi kufanya usajili popote alipo hivyo kupata leseni yake kwa wakati. ‘‘Mwombaji wa leseni ya udalali anapaswa kujisajili kupitia Tovuti ya Wizara ya Fedha (www.mof.go.tz) na kisha kubonyeza kipengele cha GAMIS na kujisajili, kujaza taarifa zinazohitajika, kujaza fomu za maombi kikamilifu na kuwasilisha kwa Katibu Tawala wa Wilaya husika kwa ajili ya uhakiki na Saini,’’ alieleza Bw. Killo. Alise...

Total Energies CHAN 2024

Picha
FT’ Madagascar 0️⃣ - 0️⃣ Mauritania

RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALI MBALI.

Picha
 

MAONYESHO YA NANE NANE KANDA YA ZIWA MAGHARIBI 2025 YAFUNGULIWA RASMI

Picha
Na Lubango Mleka, Mwanza. MGENI rasmi Mhe. Hashimu Abdallah Komba, Mkuu wa Wilaya ya Geita akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Geita Ndg. Martin Shigela leo tarehe 03 Agosti 2025, amefungua rasmi maonesho ya Nanenane kanda ya ziwa Magharibi yanayofanyika viwanja vya Nyamhongolo Wilaya ya Ilemela ambapo amesema kila mmoja anao wajibu wa kutembelea maonesho haya ya nane nane kwa ajili ya kujifunza lakini pia kujioatia bidhaa mbalimbali.  “Kama ni mkulima utapata fursa ya kujifunza kilimo cha kisasa na Chenye tija na kama ni mvuvi pia unaweza kujifunza shughuli za uvuvi kwa teknolojia ya kisasa hivyo msiache kutembelea mabanda mbali mbali kujipatia elimu na uzoefu ” Alilisitiza muwakilishi huyo wa mgeni rasmi Mhe Komba.  Akifafanua kauli mbiu ya maonyesho ya Nanenane Mwaka huu “Chagua viongozi bora kwa maendeleo endelevu ya kilimo, mifugo na uvuvi 2025” amewataka wananchi kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani na utulivu na kuchagua viongozi bora watakaowaletea maendeleo.

PPAA YASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE, KUTOA ELIMU KWA WAZABUNI NA UMMA.

Picha
 Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  MAMLAKA ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) inashiriki Maonesho ya NaneNane Kitaifa yanaendelea katika Viwanja vya Maonesho vya Nzuguni Jijini Dodoma kutoa elimu kuhusu ununuzi wa Umma kwa wazabuni, hususan elimu kuhusu Moduli ya kupokea na kushughulikia Malalamiko na Rufaa katika mfumo wa NeST.  Akiongea kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa PPAA, James Sando, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma, Nelson Kessy amesema PPAA imejipanga kutoa elimu kwa wadau wa ununuzi wa umma na wananchi kwa ujumla ili kutoa wigo mpana zaidi kwa wazabuni na wadau wa sekta hiyo.  Pamoja na mambo mengine, Kessy amewasihi wadau wa ununuzi na wananchi kwa ujumla kutembelea Banda la PPAA linalopatikana ndani ya Banda la Wizara ya Fedha katika viwanja vya Nzuguni, Dodoma. Maonesho haya kwa mwaka 2025 yamebeba kauli mbiu “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025”. Maonesho ya NaneNane Kitaifa yalifunguliwa rasmi t...

GST YATOA USHAURI NA UPIMAJI SAMPULI ZA MAJI, MIAMBA NA MADINI.

Picha
Wizara ya Madini yaendelea kutoa elimu ya Sheria, Kanuni za Madini.  Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  TAASISI ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imeendelea kutoa ushauri na huduma za upimaji wa sampuli za miamba na madini kwa wananchi mbalimbali wanaofika kutaka kujua aina za miamba na madini waliokuwanayo. Aidha, GST imekuja na vifaa vya utafiti wa miamba na madini iliyo chini ya tabaka ya juu la udongo ambavyo kitaalam vinaitwa vifaa vya jiofizikia. Sambamba na hayo, Wataalamu kutoka GST wamewashauri wananchi kutumia Maabara ya taasisi hiyo kwa uchunguzi wa sampuli zao za miamba na madini ili kubaini wingi na uwepo wa madini ili kuongeza tija na uzalishaji wa madini. Aidha, Wizara ya Madini kwa kushirikiana na taasisi zake imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya sekta ya madini kupitia banda lake lililopo katika eneo la mabanda ya Serikali, banda namba 5. Kupitia banda hilo, wananchi wanaelimishwa kuhusu shughuli mbalimbali zinazohusu sekt...