Machapisho

DKT. MPANGO AZINDUA MAONESHO YA 32 NANENANE KITAIFA JIJINI DODOMA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amezindua rasmi Maonesho ya 32 ya Wakulima (Nanenane) yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni, jijini Dodoma yenye kauli mbiu isemayo "Chagua Viongozi bora kwa Maendeleo Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025". Dkt. Mpango amesema kuwa Tanzania inaadhimisha Maonesho ya 32 ya Nanenane yenye hadhi ya Kitaifa na Kimataifa kwa lengo la kukuza uchumi na kuchochea matumizi ya teknolojia bora na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa. Tangu asubuhi ya leo, maelfu ya wananchi kutoka mikoa mbalimbali wamejitokeza kutembelea banda ya Wizara ya Madini na Taasisi zake, wakipata elimu juu ya mchango wa sekta ya madini katika kuimarisha uchumi wa wakulima na taifa kwa ujumla. Banda la wizara hiyo limepambwa na taarifa mbalimbali za kitaalamu kuhusu uongezaji thamani madini, usalama wa wachimbaji wadogo, fursa za uwekezaji, na matumizi ya teknolojia bunifu katika sekta ya madini. Akizungum...

TADB YATOA MIKOPO KWA WAZALISHAJI NA WACHAKATAJI 762,291.

Picha
  IMEELEZWA KUWAMNYORORO WA THAMANI UMEKUWA KWA WAKULIMA NA WACHAKATAJI.  Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  BENKI ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kupitia Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo, imefanikiwa kuwafikia zaidi ya wanufaika 762,291 nchi nzima, kwa kuwasaidia kupata mikopo kupitia taasisi za kifedha bila hitaji la dhamana kubwa. Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dodoma kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji Kitaifa  Rosemary  Gordon Afisa Biashara wa TADB anayesimamia mfuko huo, alieleza kuwa mfuko huo unatekelezwa kwa ushirikiano na benki 13 za biashara, benki za ushirika, na taasisi nyingine za kifedha nchini.  “Mfuko huu unahakikisha kuwa wakulima wadogo, hata wale wasio na dhamana ya kutosha, wanapata mikopo ya kuwawezesha kuendesha shughuli zao za kilimo kutoka shambani hadi sokoni,” akisema Gordon. Amesema mikopo inayodhaminiwa na mfuko huo husaidia wakulima kununua pembejeo kama mbegu, viuatilifu na mbolea, pamoja na dhana za kilim...

TAIFA STARS YAPATA MAFUNZO YA UADILIFU MICHEZONI.

Picha
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo wamepata mafunzo ya Uadilifu michezoni kuelekea mashindano ya CHAN 2024, yanayotarajiwa kuanza 02 Agosti 2025.

BEKA FRAVOUR ANOGESHA MKESHA WA MWENGE IGUNGA.

Picha
MSANII wa Mziki wa kizazi Kipya Beka Fravour ni mmoja ya Wasanii waliopanda na kutumbwiza katika jukwaa la Mkesha wa Mwenge wa Uhuru 2025 katika uwanja wa mpira wa miguu wa Barafu ulio katika Kitongoji cha Kati Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora.  Mwenge wa Uhuru 2025 katika uwanja wa mpira wa miguu wa Barafu ulio katika Kitongoji cha Kati Wilaya ya Igunga. 

COSTECH YAJENGA KITOVU CHA TAASISI ZA UBUNIFU NA UTAFITI DODOMA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma TUME ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH) inatekeleza kwa kasi mradi wa kimkakati wa ujenzi wa Makao Makuu mapya jijini Dodoma, ikiwa ni hatua ya kuiweka Tanzania kwenye msitari wa mbele katika maendeleo ya maarifa, utafiti na ubunifu wa kisayansi. Ujenzi huo, unaotarajiwa kukamilika Machi 2026, umeelezewa na viongozi wa COSTECH kuwa ni zaidi ya jengo bali ni uwekezaji wa taifa katika mustakabali wa uchumi wa ubunifu na teknolojia ya kisasa. Kwa mujibu wa Dkt. Amos Nungu, Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, jengo hilo litakuwa na uwezo wa kutoa huduma kwa watafiti, wabunifu na wajasiriamali wa teknolojia kwa kutumia miundombinu ya kisasa ikiwemo maabara bunifu, vituo vya Atamizi, kumbi za mikutano ya wataalamu, na ofisi zilizounganishwa na mifumo ya kidigitali.  “Tunajenga jukwaa la kisayansi litakalosaidia taifa kufanya maamuzi yanayotokana na ushahidi, tafiti, na maarifa. Dodoma sasa inapata nafasi ya kuwa moyo wa uvumbuzi nchini,” alisema Dkt. Nungu. Nay...

MAKAMU WA RAIS KUONGOZA KONGAMANO KUBWA LA MASHIRIKA YA KIRAIA DODOMA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Kitaifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) linalotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 11 hadi 13 Septemba 2025, jijini Dodoma. Kongamano hilo linaandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Tanzania Bara, kwa kushirikiana na mitandao ya NGOs nchini, na litawakutanisha zaidi ya mashirika elfu moja kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania. Akizungumza kuhusu maandalizi ya kongamano hilo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Bi. Felister Mdemu, alisema kongamano hilo ni sehemu ya tathmini ya miaka mitano ya utekelezaji wa kazi za NGOs, ambapo mashirika yatapima mafanikio, changamoto na mchango wao kwa jamii katika maeneo kama afya, elimu, jinsia, na ustawi wa jamii.  “Mashirika haya yamekuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo ya watu, na serikali ya awamu ya sita inatambua na kuthami...

ISMAIL USSI:- IGUNGA YATIMIZA UJENZI WA MIRADI KWA ASILIMIA 100.

Picha
  Na Lubango Mleka, Igunga. MKIMBIZA Mwenge wa Uhuru kitaifa 2025 Ismail Ali Ussi ameipongeza Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora kwa kusimamia vyema miradi yote iliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru Wilayani hapa kwa asilimia 100. Ussi ametoa pongezi hizo leo tarehe 31.07.2025 alipozungumza na Wananchi na Viongozi mbalimbali waliojitokeza katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Barafu, ambapo amesema kuwa viongozi wa wilaya ya Igunga wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Igunga Sauda Mtondoo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Bi. Selwa Abdalla Hamid wamesimamia maelekezo yote yaliyotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pindi anapotoa fedha za miradi ya maendeleo kwa wananchi. "Nimpongeze Mama yangu Mkuu wa Wilaya na Igunga Sauda Mtondoo na Mkurugenzi Mtendaji kwa kusimamia kwa ukaribu miradi hii yote ambayo tumeizindua leo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6, kwani katika miradi yote hatujakuta dosari yoyote," Mwenge wa Uhuru unapokimbizwa katika mik...

MIRADI 6 YA MAENDELEO YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 2.6 YAZINDULIWA NA MWENGE WA UHURU 2025 WILAYANI IGUNGA.

Picha
Na Lubango Mleka, Igunga.  MWENGE wa Uhuru  zimepokelewa  leo Julai 31,2025 Wilayani Igunga na Mkuu wa Wilaya  hiyo Mhe. Sauda Salum Mtondoo katika Viwanja vya Gulioni kijiji cha Simbo kata ya  Simbo ,Mwenge huo utakimbizwa kwa Umbali wa Kilomita  229.4   utapita katika tarafa tatu na kata tano na kupitia  Miradi  6 ya Maendeleo yenye thamani ya Shilingi Bilioni  2.6 kwa lengo la Kuhimiza maendeleo, Uzalendo na Wanachi Kushiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika  Oktoba 29 Mwaka huu. Katika hatua nyingine Mwenge wa Uhuru Wilayani Igunga  utapitia Miradi mbalimbali ya Maendeleo   ikiwemo Kutembelea na kukagua  vikundi vitatu vya  Vijana wanaojihusisha na Usafirishaji  wa abiria na mizigo  vyenye thamani ya Sh. 63 Milioni,Kuzindua mradi wa ujenzi wa  madarasa manne na matundu Sita ya vyoo Shule ya Msingi Igumila  wenye thamani ya 118.2 Milioni,Kufungua Mradi wa Ujenzi wa Majengo manne Hospit...

SDC NA UNFPA WATOA MWELEKEO MPYA KWA WASICHANA WALIOATHIRIWA NA MIMBA ZA UTOTONI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma  ZAIDI ya wasichana 300 waliopata mimba wakiwa na umri mdogo (Young Mothers) wamewezeshwa kupitia mradi wa "Kijana Imara" unaotekelezwa na taasisi ya Restless Development Tanzania kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (Swiss Agency for Development and Cooperation – SDC) kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (United Nations Population Fund – UNFPA). Mradi huu unatekelezwa Tanzania Bara na Visiwani, na kwa sasa unatekelezwa katika mkoa wa Dodoma kwenye wilaya tano ambazo ni Dodoma Mjini, Chamwino, Kongwa, Bahi na Kondoa DC. Wasichana hao walipewa mafunzo ya ujuzi wa maisha, elimu ya afya ya uzazi, na ujasiriamali. Baada ya mafunzo, walipewa vifaa vya kazi ikiwemo mashine za kushona nguo (chelehani), vifaa vya saluni, na mabanda ya kisasa ya kufugia kuku. Akizungumza wakati wa ugawaji wa vifaa hivyo, Afisa Mradi wa Restless Development Tanzania, Ally Saad, alisema taasisi yao inalenga kuwawezesha vijana hasa wasichana waliopata m...