ISMAIL USSI:- IGUNGA YATIMIZA UJENZI WA MIRADI KWA ASILIMIA 100.

 

Na Lubango Mleka, Igunga.

MKIMBIZA Mwenge wa Uhuru kitaifa 2025 Ismail Ali Ussi ameipongeza Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora kwa kusimamia vyema miradi yote iliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru Wilayani hapa kwa asilimia 100.

Ussi ametoa pongezi hizo leo tarehe 31.07.2025 alipozungumza na Wananchi na Viongozi mbalimbali waliojitokeza katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Barafu, ambapo amesema kuwa viongozi wa wilaya ya Igunga wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Igunga Sauda Mtondoo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Bi. Selwa Abdalla Hamid wamesimamia maelekezo yote yaliyotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pindi anapotoa fedha za miradi ya maendeleo kwa wananchi.

"Nimpongeze Mama yangu Mkuu wa Wilaya na Igunga Sauda Mtondoo na Mkurugenzi Mtendaji kwa kusimamia kwa ukaribu miradi hii yote ambayo tumeizindua leo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6, kwani katika miradi yote hatujakuta dosari yoyote,"

Mwenge wa Uhuru unapokimbizwa katika mikoa yetu na wilaya zetu unaleta matumaini kwa wananchi, hivyo mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi niwaombe Watanzania wote wnye sifa tujitikeze tukapige kura.









Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.