MIRADI 6 YA MAENDELEO YENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 2.6 YAZINDULIWA NA MWENGE WA UHURU 2025 WILAYANI IGUNGA.
Na Lubango Mleka, Igunga.
MWENGE wa Uhuru zimepokelewa leo Julai 31,2025 Wilayani Igunga na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Sauda Salum Mtondoo katika Viwanja vya Gulioni kijiji cha Simbo kata ya Simbo ,Mwenge huo utakimbizwa kwa Umbali wa Kilomita 229.4 utapita katika tarafa tatu na kata tano na kupitia Miradi 6 ya Maendeleo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.6 kwa lengo la Kuhimiza maendeleo, Uzalendo na Wanachi Kushiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29 Mwaka huu.
Katika hatua nyingine Mwenge wa Uhuru Wilayani Igunga utapitia Miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo Kutembelea na kukagua vikundi vitatu vya Vijana wanaojihusisha na Usafirishaji wa abiria na mizigo vyenye thamani ya Sh. 63 Milioni,Kuzindua mradi wa ujenzi wa madarasa manne na matundu Sita ya vyoo Shule ya Msingi Igumila wenye thamani ya 118.2 Milioni,Kufungua Mradi wa Ujenzi wa Majengo manne Hospitali ya Wilaya ya Igunga wenye thamani ya Sh. 900 Milioni
Vilevile Kufungua Mradi wa Jengo la Biashara la Halmashauri wenye thamani ya Sh.584.2,Kuzindua mradi wa Upanuzi wa mtandao wa Maji safi ya Ziwa Victoria (Makomero-Mgongoro) wenye thamani ya Sh. 840.8 Milioni na Kuzindua Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya RC Church -Barafu kwa kiwango cha Lami mita 245 wenye thamani ya Sh.130 Milioni.
Aidha Mbio za Mwenge zitakagua masuala ya Lishe,Kudhibiti UKIMWI,Matumizi nishati safi ,Malaria na Mapambano dhidi ya Rushwa.
Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 zinakwenda na kauli mbiu isemayo:-
"Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu."
Maoni