DKT. MPANGO AZINDUA MAONESHO YA 32 NANENANE KITAIFA JIJINI DODOMA
Na Mwandishi Wetu, Dodoma. MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amezindua rasmi Maonesho ya 32 ya Wakulima (Nanenane) yanayofanyika kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni, jijini Dodoma yenye kauli mbiu isemayo "Chagua Viongozi bora kwa Maendeleo Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025". Dkt. Mpango amesema kuwa Tanzania inaadhimisha Maonesho ya 32 ya Nanenane yenye hadhi ya Kitaifa na Kimataifa kwa lengo la kukuza uchumi na kuchochea matumizi ya teknolojia bora na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa. Tangu asubuhi ya leo, maelfu ya wananchi kutoka mikoa mbalimbali wamejitokeza kutembelea banda ya Wizara ya Madini na Taasisi zake, wakipata elimu juu ya mchango wa sekta ya madini katika kuimarisha uchumi wa wakulima na taifa kwa ujumla. Banda la wizara hiyo limepambwa na taarifa mbalimbali za kitaalamu kuhusu uongezaji thamani madini, usalama wa wachimbaji wadogo, fursa za uwekezaji, na matumizi ya teknolojia bunifu katika sekta ya madini. Akizungum...