RIPOTI YA FEDHA KUTOKA BENKI KUU YA TANZANIA
Ripoti ya hivi karibuni kabisa ya Benki Kuu ya Tanzania inaonesha zaidi ya robo ya wale waliochukua mikopo binafsi mwaka 2024 waliitumia kununua magari na kugharamia matibabu. Katika ripoti hiyo ya Uhimilivu wa Sekta ya Fedha, takwimu zinaonesha asilimia 14.7 ya mikopo ilikwenda kwenye matibabu na 14.2 ilitumika kununua magari. Ujenzi wa nyumba na kulipia masomo ni matumizi mengine makubwa yaliyofanywa na wale waliochukua mikopo binafsi mwaka uliopita. Je, wewe hukopa kufanyia nini?