TANZANIA NA UTURUKI KUIMARISHA BIASHARA NA MAENDELEO YA VIWANDA
Na Lubango Mleka. WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Kapinga, akiwa katika ziara ya kikazi nchini Uturuki Juni 06, 2026, Jijini Istanbul amefanya mazungumzo na Waziri wa Viwanda na Teknolojia wa Uturuki, Mehmet Fatih Kacır pamoja na Waziri wa Biashara wa Uturuki, Ömer Bolat, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na viwanda kati ya nchi hizi mbili. Mazungumzo na Waziri Kacır yamejikita katika kukuza maendeleo ya viwanda vya kimkakati, kuimarisha matumizi ya teknolojia, pamoja na kuhamasisha uwekezaji katika viwanda rafiki kwa mazingira. Mhe. Kapinga ameeleza dhamira ya serikali ya kutumia ushirikiano huo kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya mwaka 2050 ya kuwa nchi ya kipato cha kati cha juu kupitia mageuzi ya sekta ya viwanda, huku Uturuki ikiahidi kuendeleza ushirikiano wa kiufundi, kiteknolojia na ubunifu kwenye sekta hiyo. Kwa upande wa biashara, mazungumzo na Waziri Bolat yamejikita katika kuimarisha mazingira wezeshi ya uwekezaji na kuongeza kiwango cha ...