Machapisho

AHSANTE FOUNDATION WACHINJA NG'OMBE KONDOO NA MBUZI EID AL- ADHA MIRERANI

Picha
  Na Mwandishi wetu, Mirerani.  TAASISI ya Ahsante Foundation Tanzania imechinja ng'ombe 723, mbuzi na kondoo 2,500 na kutoa sadaka kwa watoto yatima, wajane, wahitaji na taasisi za serikali na binafsi, katika kusheherekea sikukuu ya Eid Al-Adha mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara. Meneja mipango wa taarifa ya Ahsante Foundation Tanzania, Omary Gyunda amesema lengo ni kuhakikisha jamii yenye mahitaji inanufaika na sadaka ya sikukuu hiyo ya Idd. Gyunda amesema taarifa ya Ahsante Foundation Tanzania wamechinja ng'ombe 723, mbuzi na kondoo 2,500 kwa ajili ya jamii kushiriki sherehe hiyo bila ubaguzi wa madhehebu katika mji mdogo na maeneo ya jirani. Amesema sadaka hiyo ya nyama ya kuchinja imetolewa kwa watoto yatima, wajane, wahitaji mbalimbali na taasisi za serikali na binafsi za mji mdogo wa Mirerani na majirani zao. "Tumetoa sadaka hiyo ya kuchinja kwa wahitaji hao na taasisi mbalimbali ikiwemo shule za msingi, sekondari, polisi, uhamiaji, zimamoto na ...

WANAMICHEZO 60 KUWAKILISHA SIMANJIRO UMITASHUMTA

Picha
  Na Mwandishi wetu, Simanjiro  WANAFUNZI wanamichezo 60 wa shule ya msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro wamechaguliwa kuiwakilisha Wilaya hiyo kwenye michuano ya michezo mbalimbali katika ngazi ya Mkoa wa Manyara. Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Gracian Max Makota akizungumza wakati akizindua rasmi michuano hiyo katika viwanja vya Mnyalu Complex Mji mdogo wa Mirerani amewaasa wanamichezo hao wanawawakilishe vyema na kuwa washindi katika ngazi ya Mkoa. "Mrudi na vikombe vya ushindi, mkashindane kwa akili, nguvu maarifa na nidhamu, kwani mchezaji mzuri ni yule ambaye anawasikiliza walimu na kutekeleza yale anavyoelezwa ili kufanikisha ushindi," amesema DED Makota. Afisa Elimu Msingi na Awali wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Darous Daudi Limandola amesema wanamichezo 60 wataiwakilisha Halmashauri hiyo kwenye ngazi ya Mkoa wa Manyara. Limandola amesema wanamichezo hao ni timu iliyosheheni hivyo wanatarajia watarudi na ushindi katika miche...

TANZANIA YAIMARISHA TAHADHARI DHIDI YA MLIPUKO WA EBOLA.

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  NAIBI Waziri wa Afya Mheshimiwa. Dkt. Florence Samizi amesema Tanzania imeendelea na hatua za kuzuia na kuimarisha utayari dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola unaosababishwa na virusi vya Bundibugyo unaoendelea katika nchi za Jamhuri ya Demokrasia Kongo na Uganda, huku akisisitiza mshikamano wa kikanda na umuhimu wa ushirikiano wa pamoja katika kulinda usalama wa afya wa wananchi. Dkt. Samizi amesema hayo leo Mei 26, 2026 kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati wa mjadala kuhusu mlipuko wa Ebola katika nchi hizo, ulioandaliwa jijini Brazzaville, Jamhuri ya Kongo, ambapo ameshiriki kwa njia ya mtandao akiwa katika ofisi za Wizara jijini Dodoma. Katika mjadala huo, Tanzania imeeleza mshikamano wake na Serikali pamoja na wananchi wa DRC na Uganda kufuatia mlipuko huo, huku ikitoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao pamoja na wahudumu wa afya waliopo mstari wa mbele wakitoa huduma. Aidha Dkt. Samizi amesema Tanzania inatambu...

JMAT: TANZANIA HAINA UBAGUZI WA KIDINI

Picha
  Na Lubango Mleka, Dodoma.  KATIBU wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Askofu Israel Maasa, amesema kwa zaidi ya nusu karne Watanzania wa dini zote wamekuwa wakiishi kwa upendo, mshikamano na kuheshimiana bila kujali tofauti zao za kiimani. Askofu Maasa amesema Tanzania imeendelea kuwa mfano wa amani, umoja na uhuru wa kuabudu kwa dini zote bila ubaguzi wowote, hali iliyosaidia kudumisha mshikamano wa kitaifa kwa miaka mingi. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, alisema jumuiya hiyo imesikitishwa na taarifa zilizotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania zinazodai kuwepo kwa ubaguzi wa kidini nchini. Alisema taarifa hizo, ambazo zinadaiwa kuungwa mkono na baadhi ya wabunge pamoja na Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Marekani, haziakisi hali halisi ya Tanzania na zimewasikitisha pamoja na kuwafedhehesha wananchi. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa JMAT, Alihadi Mussa Salum, amesema hakuna kundi lolote nchini linalonyimwa uhuru wa kuabudu au kuumizw...

RUVUMA YAPOKEA MAJIKO BANIFU 7,648 KWA BEI YA RUZUKU.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Songea- Ruvuma. MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Mheshimiwa Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed, leo Mei 25, 2026 amepokea rasmi mradi wa uuzaji na usambazaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kupitia kampuni ya Burn Manufacturing Company Limited. Mradi huo unalenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kupitia usambazaji wa majiko banifu yenye teknolojia ya kisasa kwa gharama nafuu kutokana na ruzuku inayotolewa na Serikali. Akizungumza wakati wa kupokea mradi huo, Mkuu wa Mkoa ameipongeza REA kwa kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya nishati safi ya kupikia nchini, akieleza kuwa majiko banifu yana mchango mkubwa katika kuboresha afya za wananchi pamoja na kulinda mazingira. Amesema matumizi ya majiko hayo yatasaidia kupunguza athari zinazotokana na matumizi ya kuni na mkaa usio salama, ikiwemo moshi unaosababisha madhara ya kiafya kwa watumiaji, hususan wanawake na watoto. Mheshi...

REA YASHIRIKI MBIO ZA MWENGE WANGING'OMBE, YASAMBAZA MITUNGI YA GESI KWA BEI YA RUZUKU.

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Wanging’ombe -  Njombe.  WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) umeshiriki katika sherehe za Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2026 zilizofanyika Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe, ambapo umesambaza na kuuza mitungi ya gesi ya kilo sita kwa wananchi kwa bei ya ruzuku ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini. Akizungumza baada ya kutembelea banda la REA katika sherehe hizo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026, Wazo Michael Mwang’onda, ameipongeza REA kwa juhudi kubwa inazoendelea kuzifanya katika utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia nchini.  Amesema miradi hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika kuhamasisha wananchi kutumia nishati safi, salama na rafiki kwa mazingira. Ameeleza kuwa upatikanaji wa nishati safi ya kupikia ni hatua muhimu katika kuboresha afya za wananchi, kulinda mazingira pamoja na kupunguza matumizi ya kuni na mkaa ambayo yamekuwa yakichangia uharibifu wa mazingira kwa kiwang...

NCHIMBI AAGIZA VIONGOZI WANAOWAKWAMISHA WAANDISHI WAENDESHA OFISI KUCHUKULIWA HATUA

Picha
  Na Happyness Hans, WAF - ARUSHA  MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Dkt. Emmanuel Nchimbi amewataka viongozi na wakuu wa Idara wanaowazuia waandishi waendesha Ofisi kushiriki mikutano ya chama hicho kuchukuliwa hatua za kinidhamu. Amesema hayo leo Mei 21, 2026 Mkoani Arusha kwa niaba ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa 13 wa Waandishi Waendesha Ofisi Tanzania (TAPSEA), unaoambatana na uchaguzi wa viongozi wapya wa chama hicho. “Tunatamani kila kiongozi awapende, awajali, awape safari, motisha na kuwapongeza pale wanapofanya vizuri,” amesema Dkt. Nchimbi. Mhe. Dkt. Nchimbi amesema Ofisi yoyote bila uwepo wa waandishi waendesha Ofisi ni sawa na gari lisilo na usukani, kwani wao ndiyo sura na lango la Ofisi. Amesema hakuna mtu anayeweza kuonana moja kwa moja na kiongozi bila kupitia kwa mwendesha Ofisi. Aidha amesema waandishi waendesha Ofisi wamekuwa msaada mkubwa katika Taasisi mbalim...

AFROMEDIA YAIPONGEZA "CAIRO 24" KWA KWA KUTWAA TUZO YA "TOVUTI BORA ZAIDI MASHARIKI YA KATI"

Picha
Na Mwandishi Wetu, Cairo.  HASSAN Ghazaly, Mwanzilishi wa Mpango wa “Afromedia kwa Uandishi wa Habari na Vyombo vya Habari vya Afrika”, ametoa pongezi zake za dhati kwa wahariri wa tovuti ya “Cairo 24”, wakiongozwa na mwanahabari Mahmoud El-Mamlouk, Mhariri Mkuu, kwa mnasaba wa kutunukiwa kwa tovuti hiyo na kutwaa tuzo ya “Bora zaidi Mashariki ya Kati” katika hafla ya utoaji wa tuzo za Trend Awards.  Mafanikio haya yanaakisi nafasi madhubuti ya kitaaluma na kimedia ambayo tovuti hiyo imefanikiwa kuijenga katika kipindi kifupi nchini Misri na barani Afrika. Ghazaly alieleza kuwa kutunukiwa kwa “Cairo 24” kunawakilisha mfano wa vyombo vya habari wenye ushawishi mkubwa katika medani ya habari barani Afrika na nchini Misri, ulioweza kuunganisha kasi, usahihi na uaminifu katika uwasilishaji wa habari, pamoja na mchango wake katika kufuatilia masuala ya kikanda na kimataifa, hasa yale yanayohusiana na bara la Afrika na mataifa yake. Aidha, Hassan Ghazaly alisifu mafanikio hayo, akib...

SIKU YA NYUKI DUNIANI’ YAADHIMISHWA KITAIFA TABORA

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora.  MAADHIMISHO ya Siku ya Nyuki Duniani yanayoyohusisha utundikaji mizinga, maonesho ya bidhaa na mazao ya nyuki yameanza leo katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Vita Mjini Tabora na kuvuta umati mkubwa wa wananchi. Wakizungumza kwenye maadhimisho hayo wakazi wa Tabora wameeleza kufurahishwa na tukio hilo kwa kuwa linawapa fursa wageni kutembelea Mkoa huo na kuonja utamu wa asali inayozalishwa katika misitu ya Mkoa huo. Daud Elisha, mjasiriamali mkazi wa Kata ya Kanyenye, Halmashauri ya manispaa ya Tabora ameeleza kuwa zao la asali ni miongoni mwa mazao ya kujivunia yanayozalishwa katika Mkoa huo na kuuzwa kwa bei kubwa ndani na nje ya nchi. ‘Haya maadhimisho ni fursa muhimu sana kwa wana Tabora kuuza asali yao na kupanua wigo wa uzalishaji zao hilo katika Wilaya zote za Mkoa huu, hivyo kuwaneemesha zaidi kiuchumi’, amesema. Amina Madereka, mjasiriamali anayejishughulisha na utundikaji mizinga na uuzaji asali katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi ame...