RC TABORA APEWA TUZO MAALUMU
Na Allan Kitwe, Tabora CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Tabora kimetoa tuzo maalumu kwa Mkuu wa Mkoa huo Paul Matiko Chacha kama ishara ya kutambua na kuthamini mchango wake katika suala zima la kusimamia maendeleo ya Mkoa huo. Tuzo hiyo imetolewa juzi kwenye Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ngazi ya Mkoa baada ya Wajumbe wa mkutano huo kuridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na Kiongozi huyo hivyo kupendekeza apewa tuzo katika kikao hicho. Awali, akielezea tuzo hiyo, Katibu wa CCM Mkoa Wilson Nkambaku amesema kuwa pendekezo la kutoa tuzo hiyo lilitolewa na Wajumbe katika Kikao kilichopita, hivyo chama kimelifanyia kazi na sasa wapo tayari kumkabidhi. Ameongeza kuwa chama pia kitatoa tuzo kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mheshimiwa Said Juma Nkumba kama ishara ya kutambua kazi yake njema ya kuimarisha, kudumisha na kujenga mshikamano thabiti ndani ya chama. Akikabidhi tuzo kwa Mkuu wa Mkoa, Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Said Juma Nkumba amesema kuwa Chama kimeridhishwa na kazi yake, anatekeleza...