RC TABORA APIGA MARUFUKU OMBAOMBA
Na Allan Ntana, Tabora. SERIKALI Mkoani Tabora imesema kuwa omba omba walio wengi wakiwemo wale wanaosukumwa kwenye vibaiskeli wana uwezo wa kufanya kazi zinazoweza kuwaingizia kipato na sio kukaa au kujipitisha mitaani wakiomba. Akihutubia Watumishi wa Umma na wa Sekta Binafsi kwenye Maadhimisho ya Mei Mosi yaliyofanyika Kimkoa Wilayani Kaliua Mkoani hapa jana, Mkuu wa Mkoa huo Paul Chacha amepiga marufuku ombaomba wanaojipitisha au kukaa mitaani. Ameeleza kuwa serikali ilianzisha Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ili kusaidia kaya zote zisizo na uwezo, hivyo omba omba wote wanapaswa kutambuliwa na kuingizwa katika mfuko huo na sio kuomba omba mitaani. ‘Wengi wao ni watu wazima ambao wana uwezo wa kufanya kazi na hata wale wanaowasukuma kwenye vibaiskeli hawana shida yoyote, hawa hawapaswi kuwa omba omba, wanapaswa kuwepo kwenye mfuko huo’, ameeleza. Chacha amesisitiza kuwa serikali iliweka utaratibu wa kusaidia wale wote wasio na uwezo (kaya maskini) kupitia mfuko huo wa maend...