Machapisho

SONGORO MARINE UBORA WA KIMATAIFA UJENZI MELI

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Mwanza.  KAMPUNI ya kizawa ya Songoro Marine iliyojikita katika ujenzi wa meli ndani na nje ya Tanzania inatajwa ni kampuni inayojenga meli kwa viwango vya kimataifa. Kampuni hiyo, imekuwa ikipewa zabuni na serikali za ujenzi wa vivuko, kutokana na kuonyesha uzalendo katika kutekeleza miradi kwa viwango vya kimataifa. Kwa miaka zaidi ya 30 Tangu kuanza kwa kampuni hii ya kizalendo imeonyesha dira kwa kampuni za kizawa baada ya kuaminiwa na serikali katika ujenzi wa vivuko. Kampuni hii iliyoanza kazi mwaka 1993 kwa sasa imeendeleza mizizi ya ujenzi wa meli za kisasa zinazotumiwa ziwani na baharini kwa kufungua matawi nje ya mipaka ya Tanzania. Inaelezwa kuanza kufungua matawi nje ya mipaka ya Tanzania ni hatua iliyotokana na kazi iliyotukuka kwa kujenga meli na vivuko vya umma na binafsi kwa viwango vya kimataifa. Serikali ya Tanzania mara kwa mara imekuwa ikitangaza zabuni za ujenzi wa meli, ambapo kampuni hii ya kizalendo imekuwa ikiibuka kidedea. Songoro...

KAMPUNI YA SONGORO MARINE YAKABIDHI KIVUKO UGANDA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Uganda.  KAMPUNI ya kizawa ya Songoro Marine iliyojikita katika ujenzi wa meli ndani na nje ya Tanzania imekamilisha ujenzi wa kivuko kikubwa kitakachokuwa na uwezo wa kubeba abiria 310. Kampuni hiyo imekamilisha ujenzi wa kivuko hicho kitakachokuwa kinafanya safari zake kati ya Bukungu - Kagwara - Kaberamaido nchini Uganda. Songoro marine ambayo imejikita na ujenzi wa vivuko, imeendelea kuaminiwa na serikali ya uganda katika ujenzi wa vivuko kadhaa nchini humo. Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo, Meja Songoro akizungumza wakati wa kukabidhi kivuko hicho, amesema ujenzi wa kivuko hicho ulianza februari 2020 na kukabidhiwa Februari 20 mwaka huu.  Kampuni ya Songoro Marine, ilisaini  mkataba wa ujenzi wa vivuko viwili pamoja na mashine ya kuondoa uchafu ziwani (dredger) kwa fedha za Uganda shilingi, 41,974,226,085. Baada ya siku ya jana kampuni hiyo kukabidhi kivuko hicho kwa serikali ya Uganda, inaendelea na kivuko kingine kimoja ambacho kitakabi...

BINTI MCHOMA MAHINDI TABORA AWEZESHWA MTAJI WA LAKI 3

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora.  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka ameleta neema kwa kijana muuza mahindi ya kuchoma Hadija Seif (26) mkazi wa Kata ya Ng’ambo, Manispaa ya Tabora baada ya kumwezesha mtaji wa shilingi laki 3. Waziri amemwezesha mtaji huo leo alipokuwa akifungua Jukwaa la Vijana wa Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati vilivyopo Mkoani Tabora, katika ukumbi wa Chuo Cha Utumishi wa Umma Mjini hapa. Ameeleza kuwa jana akiwa katika pita pita yake mitaani baada ya kuwasili Mjini Tabora alimwona dada mmoja akichoma mahindi na alipomuuliza mradi huo unamsaidiaje akasema kuwa unampatia kipato kidogo cha kutunza watoto wake. Na alipomuuliza ndoto yake ni nini, akaeleza kuwa anatamani kuwa na biashara ya kuuza vyombo vya nyumbani na kuuza samaki wa kukaanga, ila mtaji hana na alipoulizwa anatamani kuwa na mtaji wa kiasi gani akasema laki 3. ‘Sikujitambulisha kuwa mimi ni Waziri ila nilimwambia aje ukumbi wa Chuo cha Utumishi wa Umma kuna mkutano wa vijana, ...

KARDINALI POLYCAP PENGO AFARIKI DUNIA

Picha
 

WATUHUMIWA MAUAJI YA BODABODA TABORA WAKAMATWA

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora.  JESHI la Polisi Mkoani Tabora linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za ujambazi na mauaji ya waendesha bodaboda yaliyokuwa yakiripotiwa mara kwa mara katika maeneo mbalimbali Mkoani hapa. Hayo yamebainishwa jana na Mkuu wa Mkoa Paul Matiko Chacha alipokuwa akizungumza na Wadau wa Maendelea na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa. Amesema kuwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na operesheni maalum iliyofanywa na askari wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa kwa kushirikiana na Vyombo Vingine vya Ulinzi na Usalama. Amedokeza kuwa msako huo ulilenga kunasa wahalifu wote waliokuwa wakijihusisha na vitendo hivyo ambavyo vimekuwa vikisababisha taharuki kubwa miongoni mwa jamii na hususan waendesha bodaboda. ‘Kukamatwa watuhumiwa hawa ni hatua moja, uchunguzi bado unaendelea ili kubaini mtandao mzima na kukamata wahusika wote ili kukomesha tabia hii na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wahusika wote’, ameeleza. Aidha ameongeza kuwa watu wengine wawil...

REA YAHIMIZA WANANCHI KUJIUNGA NA HUDUMA YA UMEME TANGA

Picha
Wananchi wapewa elimu ya kufanya maombi ya umeme, waaswa kutumia umeme kwa tija kujiletea maendeleo. Na Mwandishi Wetu, Tanga.  WAKALA wa nishati vijijini (REA) umepiga kambi Mkoani Tanga kwa ajili ya zoezi la uhamasishaji wananchi kujiunga na huduma ya umeme. Uhamasihaji huo umefanyika katika maeneo ya pembezoni mwa wilaya ya Tanga mjini kwenye maeneo ya sokoni ,vituo vya bodaboda pamoja na mikutano ya hadhara iliyofanyika maeneo ya ofisi za kata na mitaa  lengo kubwa likiwa ni kuwapa uelewa wananchi juu ya umuhimu wa kujiunga na huduma ya umeme. Akizungumza wakati wa uhamasishaji Afisa maendeleo ya jamii kutoka REA , ndugu Abdulrazack Mkomi alisema , Lengo la wakala kufika wilayani humo ni kuwafikia wananchi na kuzungumza nao juu ya umuhimu wa kutumia fursa ya upatikanaji wa huduma ya umeme ambayo ni nafuu sana na kuwahimiza kujiunga mapema na huduma hiyo ya umeme hasa wakati ambapo mkandarasi bado yupo eneo la mradi. Aidha Mkomi amesema, utekelezaji wa miradi hii ya umeme u...

RAIS DKT MWINYI: SMZ KUIMARISHA USAFIRI NA USAFIRISHAJI WA MIZIGO PEMBA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali imejipanga kikamilifu kumaliza tatizo la usafiri na usafirishaji wa mizigo katika Kisiwa cha Pemba. Akizungumza leo tarehe 17 Februari 2026 wakati wa ufunguzi wa Msikiti mpya wa Chachani, uliopo Chake Chake, Mkoa wa Kusini Pemba uliojengwa na mfanyabiashara Ndg. Said Nassor Bopar, Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali imeandaa meli mbili za mwendo kasi na ipo katika hatua za kutafuta meli maalum ya mizigo kwa safari za Unguja na Pemba. Aidha, ameeleza kuwa Serikali imeliagiza Shirika la Meli la Zanzibar kuimarisha huduma zake na kubainisha kuwa meli ya MV Mapinduzi II itaanza kazi hivi karibuni baada ya matengenezo. Ameongeza kuwa uimarishaji wa bandari za Pemba utahamasisha sekta binafsi kuongeza vyombo vya usafiri. Rais Dkt. Mwinyi amewahimiza waumini kuitumia misikiti kujadili changamoto za kijamii, akiwapongeza wafadhili wa msikiti huo kwa mcha...

KIHONGOSI AKAGUA UTEKELEZAJI MIRADI YA BIL 2.5 NZEGA

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora.  KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) anayesimamia Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi ameeleza kufurahishwa na kazi nzuri ya utekelezaji miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Nzega Mkoani hapa. Akiwa katika siku ya pili ya ziara yake, Kihongosi ametembelea na kukagua utekelezaji miradi yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 2.5 iliyotekelezwa na serikali ya Awamu ya Sita katika Majimbo matatu ya Wilaya ya Nzega. Mradi wa kwanza aliotembelea ni wa ujenzi wa mabweni 2 ya wanafunzi wa kike na kiume katika shule ya sekondari Puge, ujenzi wa vyumba 6 vya madarasa na matundu 10 ya vyoo, vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 450. Amebainisha kuwa ujenzi wa miundombinu hiyo ambayo imefadhiliwa na Kampuni ya Barrick ni kichocheo muhimu sana cha kuinua ya taaluma katika shule hiyo, hivyo akatoa wito kwa walimu na wanafunzi kutumia vizuri miundombinu hiyo. Mradi mwingine ni ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Nzega uliogharimu za...

WATANZANIA TUNA WAJIBU WA KULINDA NCHI NA RASILIMALI ZAKE-WAZIRI KATAMBI

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Tanga.  WAZIRI wa Mambo ya Ndani Nchi, Mhe. Patrobas Katambi amesisitiza na kuwakumbusha Watanzania kuwa wanawajibika katika kulinda nchi na rasilimali za Tanzania pamoja na kuhakikisha Tanzania inaendelea kubakia salama na yenye amani kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa na ustawi wa jamii na kila Mtanzania. Waziri Katambi amebainisha hayo Mkoani Tanga wakati wa muendelezo wa ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akisisitiza kuwa bila amani na usalama hakuna shughuli yoyote ya kijamii ama kiuchumi inayoweza kuendelea. "Niwakumbushe Watanzania wenzangu kwamba sisi wote Watanzania tunao wajibu wa kuilinda nchi yetu. Jukumu la ulinzi na usalama wa rasilimali, raia wote ni wajibu wetu sote. Haya yote hayawezekani pia kama hakuna usalama kwani kupoteza usalama maana yake hakuna ulinzi, hakuna amani na kama hakuna amani hakuna shughuli  yoyote inayoweza kuendelea." "Leo tupo hapa tuna amani kwasababu ha...

MBUNGE AGNES MARWA ATOA SADAKA MAALUM KUUNGA MKONO MAANDALIZI YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Musoma.  MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Agnes Marwa, leo ametoa sadaka maalum kwa viongozi wa dini ya Kiislamu katika Misikiti tofauti ya Musoma Mjini ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono maandalizi ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Sadaka hiyo imelenga kuwasaidia viongozi wa dini pamoja na waumini katika kujiandaa na mwezi huo muhimu wa ibada, unaoheshimiwa na Waislamu duniani kote. Baadhi ya vitu vilivyotolewa ni pamoja na buswati, tende, kanzu, balaghashee pamoja na fedha taslimu, ambavyo vimekabidhiwa kwa viongozi kutoka misikiti mbalimbali ya Musoma Mjini. Akizungumza wakati wa tukio hilo, Agnes Marwa alisema kuwa sadaka hiyo ni ishara ya mshikamano, upendo na heshima kwa viongozi wa dini, pamoja na kuthamini mchango wao katika kujenga maadili mema na amani ndani ya jamii. “Nimeona ni muhimu kushiriki na ndugu zetu wa Kiislamu katika maandalizi ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Huu ni mwezi wa ibada, subira, na kusaidiana, hivyo ni wajibu wetu kama viongozi kuende...