Machapisho

UMIKIDO WASHIRIKI MKUTANO MKUU WA MWAKA WA VYOMBO VYA UTANGAZAJI

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  UMOJA wa Vyombo vya Habari vya Mitandao ya Kijamii Mkoa wa Dodoma (UMIKIDO) umeshiriki Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji nchini. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika katika Ukumbi wa New Generation jijini Dodoma, ukianza leo Februari 12, 2026. Mkutano huo umeandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Katika mkutano huo, mada na mafunzo mbalimbali yanawasilishwa kwa waandishi wa habari pamoja na wadau wa sekta ya utangazaji.  Aidha, kunafanyika mijadala mbalimbali inayolenga kujadili masuala muhimu yanayohusu maendeleo na uboreshaji wa vyombo vya utangazaji nchini. Mkutano huo umefunguliwa rasmi na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma.

SIKU 100 ZA RAIS SAMIA ZALETA NEEMA IGUNGA

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora.  SIKU 100 baada ya kuingia madarakani katika awamu ya pili ya uongozi wake,  Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameleta neema kwa wakazi wa Mji wa Igunga Mkoani hapa kwa kuwawezesha kupata huduma ya maji kwa masaa 24 kila siku. Akizungumza na gazeti hili jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Igunga (IGUWASA) Alex Ntonge ameeleza kuwa kazi nzuri iliyofanywa na Mheshimiwa Rais imemaliza changamoto za huduma ya maji. Amebainisha kuwa maboresho makubwa ya miundombinu na kupanuliwa kwa mradi wa maji ya Ziwa Victoria kumewezesha wakazi wote wa Mji huo na maeneo jirani kupata huduma ya maji safi na salama wakati wote, kwa masaa 24 kila siku. ‘Kazi nzuri iliyofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika siku 100 za kwanza tangu aingie Ofisini, imeleta neema, mabilioni aliyotuletea yameendelea kuboresha huduma ya maji na usafi wa mazingira Mji wote’, amesema. Mkurugenzi amefafanua kuwa zaidi ya asilimia 98 ya wakazi wote wa Mj...

GHAZALY AMPONGEZ WAZIRI MPYA WA VIJANA NA MICHEZO

Picha
Na Mwandishi Wetu, Misri.  MTAFITI wa Anthropolojia Hassan Ghazaly, Mwanzilishi wa Afromedia, mpango wa uandishi wa habari na vyombo vya habari barani Afrika, pamoja na timu ya Afromedia, wanatoa pongezi za dhati kwa Mheshimiwa Waziri Gohar Nabil kwa kuteuliwa kwake kuwa Waziri wa Vijana na Michezo, kufuatia kutolewa kwa amri ya rais na kuapishwa kwake rasmi. Katika taarifa yake, Ghazaly alieleza kuthamini kwa kina imani aliyopewa, akisisitiza kuwa hatua inayofuata inahitaji maono mapya na sera madhubuti za kuwawezesha vijana, kuendeleza vipaji vya michezo, na kuifanya michezo kuwa chombo muhimu cha maendeleo, kwa kuendana na mkakati wa taifa la Misri na dira ya Jamhuri Mpya. Ghazaly pia alibainisha umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa Kiafrika katika nyanja za vyombo vya habari, vijana na michezo, kwa lengo la kujenga madaraja kati ya mataifa, kuimarisha maadili ya pamoja, kugundua na kukuza vipaji vya vijana wa Afrika, kuangazia mifano chanya, kutangaza mipango ya pamoja, na kusu...

.MAIPAC YAWANOA WAANDISHI

Picha
  Na mwandishi wetu. Arusha.  TAAASI ya waandishi wa habari ya kusaidia jamii za pembezoni (MAIPAC) imetoa mafunzo kwa waandishi wa habari nchini, ya uandishi wakati wa migogoro ambao unazingatia usalama.wao na amani. Mafunzo hayo yameshirikisha waandishi wa habari kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Geita, Mara, Manyara, Mbeya na Arusha, yalidhaminiwa na shirika la wanahabari la Press Unlimited. Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa MAIPAC, Mussa Juma aliwataka wanahabari wanaokwenda kuripoti migogoro kuzingatia kuchukuwa tahadhari za kiusalama na.kutopendelea sehemu yoyote.  Juma amesema habari za upande mmoja ambazo hazizingatii maadili na maslahi mapana ya Umma zimekuwa zikisababisha migogoro katika jamii. Hata hivyo, amewataka wanahabari wakati wote wa kazi zao kuzingatia usalama wao,kufanya upembuzi yakinifu wa habari wananayotaka kuandika kabla ya kuandika na baada ya kuandika. "Tujuwe habari ina madhara gani,inafaida gani ,tusiwe na upande katika hiyo habari na...

NDUGU WASHIKILIWA KWA KUMUUA SHEMEJI YAO 'KISA MGOGORO WA MASHAMBA'

Picha
Na Mwandishi Wetu, Mbeya.  JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia ndugu wa familia moja ambao ni Solomon Mwambyale (68) na watoto wake wawili, Stephano Mwaisango (32) na Emmanuel Mwaisango (36), kwa tuhuma za mauaji ya Jenti Segelela (87) ambaye alikuwa shemeji yake na mtuhumiwa Solomon, wakidaiwa kumkata na kitu chenye ncha kali kisogoni na kisha kukimbia, chanzo kikiwa ni mgogoro wa mashamba ya ukoo na tamaa ya kujipatia mali kwa njia isiyo halali. Katika tukio la Pili, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga amesema wanamshikilia Bw. Charles Oden Mwakasege (32) fundi simu Mkazi wa Meta Jijini Mbeya na Bw. Isack Charles 'Bebwa' mkazi wa Shewa, kwa tuhuma za kuingilia mfumo wa kibiashara wa makampuni ya ukopeshaji wa simu. Kulingana na Kamanda Kuzaga katika taarifa yake ya leo Jumanne Februari 10, 2026 kwa Vyombo vya habari, watuhumiwa hao walikamatwa katika msako uliofanyika kuanzia Januari 27, 2026 katika maeneo mba...

WAZIRI WA FEDHA AWAHAKIKISHIA USHIRIANO WAWEKEZAJI NCHINI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  WAZIRI wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amewaahidi wawekezaji kuwa Serikali itaendelea kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya uwekezaji nchini kwa manufaa ya pande zote mbili kutokana na manufaa ya sekta hiyo kwa uchumi wa nchi na wawekezaji. Mhe. Balozi Omar amesema hayo mjini Dodoma, alipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Kampuni mpya ya Uchimbaji Dhahabu Nyanzaga (Nyanzaga Mining Company Ltd), unaojengwa katika eneo la Nyanzaga Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza ambao hadi kukamilika kwake unatarajiwa kugharimu zaidi ya dola za Marekani milioni 523. Alisema kuwa mradi huo ni mkubwa kujengwa Tanzania toka miaka zaidi ya 18 iliyopita ambapo mgodi wa Buzwagi ulijengwa. Na fursa zitaendelea hivyo kwa ukubwa wake. Lakini pia kuchangia uchumi wa nchi Kupitia kodi mbalimbali. “Ni mara yangu ya kwanza kukutana na uongozi wa mgodi wa dhahabu wa Nyanzagi na tumejadili kuhusu changamoto ya msamaha wa kodi na nimewaahidi kuwa hadi mwisho w...

NZUWASA YAONGEZA UZALISHAJI MAJI NZEGA

Picha
  Na Allan Kitwe, Nzega.  MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Nzega (NZUWASA) imeongeza mtandao wa upatikanaji huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa Mji wa Nzega hadi kufikia kilomita 738.3 ambazo ni sawa na asilimia 99.5 ya eneo lote. Akizungumza na gazeti hili jana Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo Mhandisi Humphrey Mwiyombela amesema kuwa takribani eneo lote la Mji wa wa Nzega kwa sasa limefikiwa na huduma ya maji safi na salama. Amebainisha kuwa mafanikio hayo yametokana na mikakati yao ya kuendelea kuzalisha maji kupitia vyanzo vyake vya ndani kwa lengo la kupanua wigo wa upatikanaji huduma hiyo katika maeneo yote ya Mji huo na maeneo jirani. Ametaja mkakati mwingine uliosaidia kuimarisha upatikanaji huduma hiyo kuwa ni kuendelea kushirikiana na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kahama na Shinyanga (KASHWASA). Mkurugenzi amedokeza kuwa mahitaji ya maji kwa wakazi wa Mji huo kwa siku ni mita za ujazo 5,600 na kiasi kinachozalishwa kupitia vyanzo vya...

SERIKALI YAENDELEA KUIMARISHA AFUA ZA KINGA DHIDI YA VVU, MAGONJWA YA NGONO NA HOMA YA INI

Picha
  Na WAF, Morogoro.  SERIKALI imeendelea na utekelezaji wa afua za kinga dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU), Magonjwa ya Ngono (STIs) na Homa ya Ini  kwa ngazi ya mikoa na jamii, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kufikia malengo ya kitaifa ya kudhibiti maambukizi mapya na kulinda afya ya mwananchi. Hayo yamebainishwa Februari 10, 2026 na Meneja Mpango wa Taifa wa kudhibiti UKIMWI, Magonjwa ya Ngono na Homa ya Ini (NASHCoP) Dkt. Prosper Faustine wakati wa ufunguzi wa mkutano wa waratibu wa afua za UKIMWI nchini, kinachoendelea mkoani Morogoro mkutano ambao unaangazia kufanya mapitio ya utendaji na utekelezaji wa huduma mbalimbali za kinga. "Upimaji wa VVU, matumizi ya dawa kinga za PrEP, tohara ya hiari ya wanaume, programu za kondomu pamoja na afua zinazolenga wasichana balehe na wanawake vijana na wavulana balehe na wanaume vijana zimekua endelevu ili kufikia lengo la 95 95 95 ifikapo mwaka 2030" amesema Dkt. Faustine. Mapitio hayo yanalenga kubaini mafanikio yali...

TASAC YATOA ELIMU YA USAFIRI MAJINI FUKWE YA MSIMBATI - MTWARA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Mtwara.  SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limetoa elimu ya usafiri kwa njia ya maji kwa wadau wake katika fukwe ya Msimbati, mkoani Mtwara.  Elimu hiyo imelenga kuongeza uelewa kuhusu matumizi salama ya vyombo vya usafiri majini, ikiwemo kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama wakati wa safari. Katika utoaji wa elimu hiyo, maafisa wa TASAC wamewakumbusha wamiliki na waendeshaji wa vyombo vya usafiri majini, wavuvi pamoja na abiria umuhimu wa kuvaa vifaa vya kujikinga kama vile jaketi za kuokoa Maisha (life jacket), kufanya ukaguzi wa vyombo kabla ya safari na kuepuka kupakia abiria au mizigo kupita kiasi.  Wadau walioshiriki wamepongeza juhudi za TASAC kwa kuendelea kuwafikia moja kwa moja katika maeneo yao ya kazi na kutoa elimu yenye tija. Wamesema elimu hiyo itasaidia kupunguza ajali za majini na kuongeza usalama wa vyombo na watumiaji wake, huku wakiahidi kushirikiana na TASAC katika kutekeleza miongozo ya usalama kwa manu...