.MAIPAC YAWANOA WAANDISHI

 


Na mwandishi wetu. Arusha. 

TAAASI ya waandishi wa habari ya kusaidia jamii za pembezoni (MAIPAC) imetoa mafunzo kwa waandishi wa habari nchini, ya uandishi wakati wa migogoro ambao unazingatia usalama.wao na amani.

Mafunzo hayo yameshirikisha waandishi wa habari kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Geita, Mara, Manyara, Mbeya na Arusha, yalidhaminiwa na shirika la wanahabari la Press Unlimited.

Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa MAIPAC, Mussa Juma aliwataka wanahabari wanaokwenda kuripoti migogoro kuzingatia kuchukuwa tahadhari za kiusalama na.kutopendelea sehemu yoyote. 

Juma amesema habari za upande mmoja ambazo hazizingatii maadili na maslahi mapana ya Umma zimekuwa zikisababisha migogoro katika jamii.

Hata hivyo, amewataka wanahabari wakati wote wa kazi zao kuzingatia usalama wao,kufanya upembuzi yakinifu wa habari wananayotaka kuandika kabla ya kuandika na baada ya kuandika.

"Tujuwe habari ina madhara gani,inafaida gani ,tusiwe na upande katika hiyo habari na kubwa tuwe tunachukuwa tahadhali za kiusalama wa tunapotumia vyombo vya kidigitari na usalama binafsi," amesema.

Wakili  wa kujitegemea John Sendodo akitoa mafunzo kuhusu sheria mbalimbali za masuala ya habari ,amewataka wanahabari kuzingatia sheria hizo hata kama.zina mapungufu.

"Kuna sheria kadhaa ambazo lazima mzijuwe ikiwepo sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016, sheria ya makosa ya mitandaoni ya mwaka 2015, kanuni.za maudhui mitandao na nyingine kadhaa tusome tujuwe," amesema.

Wakili.Sendodo ambaye anafanyakazi na shirika la.kimataifa la Protection Afrika akifafanua sheria hizo,vifungu kwa vifungu pamoja na mikataba kadhaa ya kimataifa lnayohusiana na wanahabari aliwataka wanahabari kufanyakazi kwa kutovunja sheria lakini wakitekeleza wajibu wao.

Mmiliki wa chuo cha waandishi wa habari cha Fanikiwa kilichopo Arusha, mwanahabari Joseph Mayagilla akitoa mada katika mafunzo hayo, amewataka wanahabari wakati wote wa kazi zao kuzingatia maadili ya uandishi.

Mayagilla amesema habari za upande mmoja.zimekuwa na madhara katika jamii na sasa kumeibuka uandishi usiojali maadili ya uandishi.

Hata hivyo, amesema ili kuhakikisha habari.zinakuwa bora ni muhimu kurejesha madawati ya vitengo kadhaa kwenye vyombo vya habari ikiwepo madawati ya habari za uchunguzi,amani na maendeleo,uchumi na mengine kwani yataongozwa na waandishi wabobezi wa eneo husika.

Mtaalam wa masuala ya Saikolojia,Ester Cornelio amewataka wanahabari wanaokabiliwa na msongo wa mawazo kutojifungia kwenye vyombo vya habari na watoke kupata tiba.

Amesema kunywa pombe kupita kiasi ama kuvuta sana sigara hakuwezi kuondoa msongo wa mawazo (trouma) bali ni kufika kwa wataalam na kupata tiba ambayo ni ushauri nasihi.

Cornelio amesema wanaume wamekuwa wahanga wa msongo wa mawazo ama sonona kwa sababu hawazungumzi ili kutoa yaliyomoyoni tofaufi na wanawake.

Wakichangia mada katika mafunzo hayo, wanahabari Tausi Mbowe ambaye ni meneja wa dawati ya Kidigitali Star Tv,  na Anthony Mayunga kutoka Serengeti media, wameeleza umuhimu wa maadili ya uandishi na athari za msongo wa mawazo na mapungufu ya sheria.

Tausi Mbowe ameshauri kuendelea kuimarishwa mafunzo ya mara kwa mara kwa wanahabari hasa kuhusiana na sheria na kukabiliana na msongo wa mawazo.

Upande wake mwanahabari Elizabeth Nyivambe kutoka Mbeya, Muta Robet wa Geita na Zacharia Mtigandi wa Manyara wameeleza pia umuhimu wa kuendelezwa mafunzo hasa masuala ya matumizi sahihi ya mitandao na usalama kwa wanahabari.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.