WAZIRI AWESO APELEKA NEEMA URAMBO
Na Allan Kitwe, Tabora. WAKAZI wa Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora wamelipuka kwa shangwe na furaha baada ya Waziri wa Maji Jumaa Aweso kuagiza maji ya ziwa Victoria yafikishwe katika Wilaya hiyo ndani ya wiki tatu kuanzia sasa. Waziri ametoa agizo hilo jana alipokuwa akizungumza na mamia ya wakazi wa Wilaya hiyo katika Kata ya Muungano baada ya kutembelea na kukagua Mradi wa Maji wa Miji 28 unaotekelezwa na serikali ya awamu ya sita katika Wilaya tatu za Mkoa huo. Amesema kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi bilioni 143 ili kuleta maji ya uhakika ya ziwa Viktoria katika Wilaya za Kaliua, Urambo na Sikonge ambazo zinashida kubwa ya maji. ‘Mradi huu utekelezaji wake unaenda vizuri sana, ujenzi wa tanki kubwa la kupokelea maji tayari umekamilika, na nimeambiwa kuwa kipande kilichobakia hakizidi hata kilometa moja maji yatakuwa yamefika hapa Urambo’, ameeleza. ‘Nitawaongezea shilingi milioni 500 za mabomba ili kazi hii ifanyike ha...