Machapisho

DIAMOND AAHIDI VYOMBO VYAKE KUFUATA MATAKWA YA SHERIA.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam. MKURUGENZI wa Wasafi Media, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz, ameipongeza Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) kwa utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari, huku akiahidi kuwa tayari kufuata matakwa yote ya kisheria yanayohusu sekta ya habari na watumishi wake.  Akizungumza baada ya kufika katika ofisi za Bodi hiyo tarehe 31 Januari, 2026 jijinj Dar es Salaam kwa ajili ya kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kisheria, Diamond amesema Wasafi Media haina nia ya kukwepa utekelezaji wa Sheria, bali iko tayari kushirikiana kikamilifu na wasimamizi wa taaluma hiyo. Amesema licha ya Sheria ya Huduma za Habari kuathiri vyombo vya habari kwa namna moja au nyingine, haiwezi kupingwa kwani ilitoa muda wa kutosha kwa wadau kujipanga na kutimiza vigezo vilivyowekwa ikiwemo Waandishi wake kuwa na kiwango cha Elimu cha Diploma na kuendelea. Diamond amekiri kuwa ujio wa Bodi ya Ithibati umeleta nidhamu kubwa katika t...

SERIKALI YAENDELEA KUWEKEZA MAFUNZO YA UJUZI BOBEZI KWA WATAALAM SEKTA YA AFYA

Picha
  Na WAF, Kibiti. SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imeendelea kufanya uwekezaji kwenye sekta ya afya kwa hususan ni kwa wataalam Bingwa na  Bobezi ili wananchi wapate huduma bora za afya. Hayo yamebainishwa leo Januari 31, 2026 na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Dkt. Dismas Masulubu wakati wa zoezi la kuwajengea uwezo wataalam wa afya wanaotoa huduma za dharura (EMD) na huduma kwa wagonjwa mahututi (ICU). "Mafunzo haya yatawasaidia wataalam kumudu kuwahudumia wagonjwa mahututi kwa ufanisi pamoja na kutoa huduma za dharura kwa weledi zaidi. Pia yatawawezesha kutumia ipasavyo vifaa na mashine za kisasa zilizonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kuimarisha huduma hizo" amesema Dkt. Masulubu. Dkt. Masulubu ametimia wasaa huo kuwashukuru wataalam kutoka Wizara ya Afya waliofika hospitalini hapo kutoa mafunzo, akisisitiza kuwa hatua hiyo itahakikisha wananchi wa Kibiti wanapata huduma bora za dharura na uangalizi wa wagonjwa mahututi karibu na makazi yao. Kwa upande wake, Mganga Mfawi...

DC NYAMWESE: MADIWANI MSITANGULIZE MASLAHI BINAFSI KWENYE HALMASHAURI

Picha
Asisitiza uwajibikaji, uwazi na ubunifu katika kuongeza mapato. Na Augusta Njoji, Handeni. MKUU wa Wilaya ya Handeni, Mhe. Salum Nyamwese, amewataka madiwani wa Halmashauri ya Mji Handeni, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni na Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi kuacha kutanguliza maslahi binafsi au ya kisiasa wanapotekeleza majukumu yao, na badala yake kuweka mbele maslahi ya wananchi na maendeleo ya halmashauri. Nyamwese ametoa wito huo mjini Handeni wakati akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo madiwani, yaliyolenga kuwaimarisha katika masuala ya utawala bora, ufuatiliaji wa mapato na uelewa wa mipaka ya majukumu yao katika uendeshaji wa halmashauri. Amesisitiza kuwa serikali haitavumilia uzembe, hujuma wala vitendo vyovyote vinavyozorotesha maendeleo ya halmashauri, akiwataka madiwani kuwa macho na kutoa taarifa kwa wakati pindi wanapobaini mianya ya upotevu wa mapato. “Tunaomba mkawe wabunifu na mzishauri halmashauri namna bora ya kuboresha na kusimamia vyanzo vya mapato. Nyie ndio mnaoi...

BONANZA LA MICHEZO TASAC LAFANA

Picha
  Na Lubango Mleka, Dar Es Salaam. SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) leo, tarehe 31 Januari 2026, limefanya Bonanza la Michezo  katika viwanja vya APC Bunju, kwa lengo la kuimarisha afya, mshikamano, na mahusiano mema kazini. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Bonanza hilo, Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Bw. Mohamed Salum, aliwataka watumishi wote waliohudhuria kuendeleza tabia ya kufanya mazoezi kama njia ya kujenga na kuimarisha afya. "Nipende kuchukua nafasi hii kuwakaribisha watumishi wote mliojitokeza katika Bonanza hili la Michezo. Ushiriki wenu unaonesha mshikamano na umoja tulionao kama familia moja ya Shirika. Bonanza hili liwe chachu ya kuendeleza utamaduni wa michezo ndani ya Shirika letu.” Alisema Bw. Salum. Bw. Salum ametoa rai kwa watumishi hao kujibidiisha kwa kushiriki mic zo na mazoezi ya viungo mara kwa mara, kwani michezo ni nguzo muhimu katika kujenga na kuimarisha afya, kuongeza ufanisi kazini na kuimarisha mahusiano mema miongoni mwa wafanyakazi wa TA...

MICHEZO NI SILAHA YA UMOJA, AFYA NA TIJA KAZINI

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Dodoma. WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mwigulu Nchemba, amesema michezo ni nyenzo muhimu katika kuondoa mipasuko ya kijamii, kuimarisha mahusiano ya kikazi na kuongeza tija katika taasisi za umma na binafsi, akisisitiza kuwa mchango wake unaenda mbali zaidi ya burudani au mazoezi ya mwili. Akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri Mkuu katika Bonanza la Bunge lililofanyika jijini Dodoma kwa ufadhili wa Benki ya Azania, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukivi, amesema michezo imeendelea kuthibitisha nafasi yake kama nguzo ya mshikamano, umoja na maendeleo ya Taifa. Ameeleza kuwa pamoja na kujenga afya ya mwili, michezo ni njia madhubuti ya kupunguza msongo wa mawazo, kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari na shinikizo la damu, pamoja na kuimarisha afya ya akili kwa watumishi na jamii kwa ujumla. “Msingi wa Bonanza la Bunge ni kuhimiza mshikamano na ushiriki wa jamii. Ushirikishwaji wa wabunge, watumishi wa Bunge, taasisi za S...

SERIKALI YATOA VIFAA VYA KIDIJITI BILIONI 5.4 KUWAWEZESHA WALIMU WENYE ULEMAVU

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Dodoma. SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imenunua na kusambaza vifaa vya kidijiti na saidizi vyenye thamani ya shilingi bilioni 5.4 kwa walimu wa shule za msingi na sekondari, wakufunzi pamoja na walimu tarajali wenye ulemavu katika vyuo vya ualimu nchini, kwa lengo la kurahisisha ujifunzaji na ufundishaji jumuishi. Akizungumza na waandishi wa habari Januari 31, 2026 jijini Dodoma, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, amesema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya siku 100, akisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imejizatiti kuhakikisha wanafunzi na walimu wenye mahitaji maalum hawatengeki katika mfumo wa elimu. Prof. Mkenda amesema jumla ya wanufaika 1,055 kutoka Halmashauri 104 nchini wamenufaika na mpango huo, ambapo vifaa vilivyosambazwa ni pamoja na kompyuta mpakato 680, vifaa tisa vya Brain Note Touch Pass, vinasa sauti (voice recorders) 377, tablet 196 kwa wana...

WAGONJWA 2000 KUFANYIWA UPASUAJI WA MABUSHA, MILIONI 992 KUTUMIKA. ‎

Picha
  ‎Na Hamida Ramadhan, Dodoma. ‎SERIKALI imepanga kufanya upasuaji wa mabusha kwa wagonjwa 2,000 katika mwaka wa fedha 2025/2026, ambapo hadi sasa wagonjwa 1,700 wamepangiwa kufanyiwa upasuaji kwa gharama ya shilingi Milioni 992, fedha zinazotolewa na Serikali. ‎Hayo yameelezwa leo Ijumaa, Januari 30, 2026 jijini Dodoma na Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele Duniani. ‎Waziri Mchengerwa amesema walengwa wa huduma hiyo watatoka katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi, Pwani, Morogoro na Mbeya. ‎Amesema Serikali, kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, itaendelea kutoa huduma kwa wananchi wanaoathirika na magonjwa hayo, ikiwemo huduma za upasuaji. ‎“Katika mwaka wa fedha 2024/2025, jumla ya wananchi 1,084 wamepatiwa huduma ya upasuaji wa mabusha nchini,” amesema Mchengerwa.

RIDHIWANI:HAKUTAKUWA NA MABADILIKO YA VITUO VYA KAZI KWA WAAJIRIWA WAPYA

Picha
  Na Hamida Ramadhan,  Dodoma. SERIKALI imetangaza kuwa hakutakuwa na mabadiliko ya vituo vya kazi kwa waajiriwa wapya waliopata ajira katika zoezi la ajira 12,000, ikieleza kuwa nafasi hizo zilitolewa kulingana na mahitaji halisi ya kila Halmashauri na mwajiri husika. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma,kuhusu ahadi za Siku 100 za Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, amesema kuruhusu mabadiliko ya vituo vya kazi kutasababisha upungufu wa watumishi katika maeneo yaliyopangiwa na kuathiri utoaji wa huduma kwa wananchi. Ridhiwani amesema Serikali imefanya upangaji wa ajira hizo kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha kila Halmashauri inanufaika kulingana na uhitaji wake, hivyo waajiriwa wapya wanapaswa kwenda kufanya kazi katika vituo walivyopangiwa bila masharti. Amesisitiza kuwa waajiriwa wote wapya wanapaswa kuripoti katika vituo vyao vya kazi ndani ya siku 14 tangu kupokea barua za...

PBPA YAFUNGUA MILANGO KWA VIJANA WA UHANDISI WA MAFUTA KUTOKA UDSM NA DMI

Picha
Na Mwandishi Wetu- Dar es Salaam. WAKALA wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) leo tarehe 30 Januari, 2026 umepokea ugeni wa wanafunzi 30 wa Kitengo cha Petroleum Engineering kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), chini ya Chama cha wahandisi wa mafuta (Society of Petroleum Engineers -SPE),waliotembelea Wakala huo kwa lengo la kujifunza kwa vitendo kuhusu utendaji kazi wa PBPA na namna Mfumo wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (BPS) unavyotekelezwa nchini. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Kaimu Meneja wa Kitengo cha Lojistiki za Mafuta PBPA, Mhandisi Sophia Kidimwa, alisema kuwa wanafunzi hao wamepata fursa ya kuelewa mchakato mzima wa upatikanaji wa mafuta nchini kuanzia hatua za uagizaji hadi usimamizi wa lojistiki za kupokea mafuta. “Tumepokea ugeni wa wanafunzi wa mwaka wa nne kutoka UDSM na DMI waliokuja kujifunza kuhusu taratibu zote za upatikanaji wa mafuta hapa Tanzania, jinsi mafuta yanavyoingia nchini, mchakato mzima wa uletaji wake pamoj...

MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KUONGEZEKA MARA.

Picha
  Majiko banifu 8,486 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku mkoani Mara, Wilaya Sita kunufaika na mradi. Na Mwandishi Wetu, Mara. SERIKALI ya Mkoa wa Mara kupitia Kaimu katibu tawala wa mkoa wa Mara   ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji, Mhandisi Mwita Chacha Okayo leo Januari 30, 2026 imepokea mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku. Akizungumza wakati wa utoaji wa taarifa ya mradi, Mhandisi Mwandamizi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Deusdedith Malulu amesema, Kupitia tafiti iliyofanyika mwaka 2016 inakadiria  kuwa takribani watu 33,024 hufariki kabla ya wakati kila mwaka kutokana na magonjwa ambayo yanachangiwa na uchafuzi wa hewa ndani ya nyumba wakati wa upikaji kwa kutumia nishati isiyo  safi na salama ya kupikia na hii ni sawa na asilimia 8.49 ya vifo vyote nchini. Hivyo, kwa kutambua hilo Serikali kupitia REA imekuja na mpango wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku ili kupunguza a...