BONANZA LA MICHEZO TASAC LAFANA

 



Na Lubango Mleka, Dar Es Salaam.

SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) leo, tarehe 31 Januari 2026, limefanya Bonanza la Michezo  katika viwanja vya APC Bunju, kwa lengo la kuimarisha afya, mshikamano, na mahusiano mema kazini.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Bonanza hilo, Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Bw. Mohamed Salum, aliwataka watumishi wote waliohudhuria kuendeleza tabia ya kufanya mazoezi kama njia ya kujenga na kuimarisha afya.

"Nipende kuchukua nafasi hii kuwakaribisha watumishi wote mliojitokeza katika Bonanza hili la Michezo. Ushiriki wenu unaonesha mshikamano na umoja tulionao kama familia moja ya Shirika. Bonanza hili liwe chachu ya kuendeleza utamaduni wa michezo ndani ya Shirika letu.” Alisema Bw. Salum.

Bw. Salum ametoa rai kwa watumishi hao kujibidiisha kwa kushiriki mic

zo na mazoezi ya viungo mara kwa mara, kwani michezo ni nguzo muhimu katika kujenga na kuimarisha afya, kuongeza ufanisi kazini na kuimarisha mahusiano mema miongoni mwa wafanyakazi wa TASAC. 

Bonanza hilo lilijumuisha michezo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu, kuvuta kamba, kukimbia kwa magunia, na kukimbiza kuku. Washiriki walionyesha ushindani wa kirafiki, uliojaa furaha na burudani.

Aidha, kulifanyika matembezi ya pamoja na mazoezi ya viungo ambayo yalisisimua umoja, nguvu, na ari ya kufanya kazi kwa pamoja, na kuacha kumbukumbu nzuri na tabasamu kwa wote walioshiriki.












Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.