SERIKALI YAONYA WATAALAMU WA ARDHI WASIO WAADILIFU
Na Allan Kitwe, Tabora SERIKALI imewataka watumishi wa sekta ya ardhi nchini kufanya kazi kwa weledi na uadilifu ili kuhakikisha migogoro ya ardhi iliyopo katika maeneo yao inatatuliwa kwa wakati ili kuepusha malalamiko ya wananchi. Onyo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Kaspar Kaspar Mmuya alipokuwa akiongea na watumishi wa sekta hiyo kutoka taasisi mbalimbali za umma Mkoani hapa. Ameeleza kuwa ni jukumu la wataalamu wa sekta hii kuhakikisha kero na migogoro yoyote inayohusiana na masuala ya ardhi inashughulikiwa ipasavyo na kwa wakati ili wananchi wapate haki zao. ‘Ninyi ni wawakilishi wa Mheshimiwa Rais katika sekta hii, onyesheni weledi wenu, fanyeni kazi kwa uadilifu mkubwa, kuweni na maadili mema, tendeni haki kwa wananchi wote ili wawaamini, wengi wenu mnaitwa wapiga dili’, amesema. Ameonya kuwa serikali haitamvumilia mtumishi yeyote wa sekta hii anayeendekeza vitendo vya upigaji dili badala ya kutekeleza wajibu wake kwa kuzingatia she...