Machapisho

TANZANIA YANG'ARA DUNIANI KUNDI LA VINARA WA SERIKALI KIDIGITALI - WORLD BANK 2025.

Picha
Na Hamida Ramadhani. TANZANIA imeendelea kung’ara kimataifa baada ya Benki ya Dunia (World Bank – WB) kuitaja kuwa miongoni mwa nchi zilizo na ukomavu wa juu wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika sekta ya umma.  Hatua hii ni uthibitisho wa mafanikio ya mageuzi ya kidijitali yanayoendelea kutekelezwa na Serikali katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. Kwa mujibu wa Ripoti ya GovTech Maturity Index (GTMI) ya mwaka 2025, Tanzania imeorodheshwa katika Kundi A – Ukomavu wa Juu wa Matumizi ya TEHAMA (Extensive GovTech Maturity).  Kundi hili linajumuisha nchi zinazoongoza duniani katika matumizi ya teknolojia katika utoaji wa huduma za serikali na ushirikishwaji wa wananchi kidijitali. GTMI: Kipimo cha Ukomavu wa Serikali Kidijitali. Ripoti ya GTMI hutathmini ukomavu wa matumizi ya TEHAMA serikalini katika takriban nchi zote duniani, ikizingatia maeneo muhimu kama sera, sheria, miongozo, mifumo ya TEHAMA na utekelezaji wake. Toleo la 2025 la ripot...

MIRERANI WALIA NA MAJI YA KUNYWA

Picha
  Na Mwandishi wetu, Mirerani. WAKAZI wa mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, kwa zaidi ya wiki moja wamelalamikia kutopata huduma ya maji ya kunywa, baada ya malori yanayouza maji hayo kutoka mji mdogo wa Boma ng'ombe wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kudaiwa kuzuiwa. Kwa zaidi ya miaka 20 wakazi wa mji mdogo wa Mirerani, wanatumia maji ya kunywa yanayouzwa na malori kutoka mji mdogo wa Boma ng'ombe. Hivi sasa, baadhi ya wakazi wengine wa mji huo wanatumia maji ya visima vifupi na virefu na maji ya mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jiji la Arusha (AUWSA) Mirerani, kwa ajili ya matumizi mengine ikiwemo kunywa. Baadhi ya wakazi wa mji mdogo wa Mirerani, wakizungumza juu ya changamoto hiyo wameiomba serikali kuingilia kati suala hilo kwani wanatumia gharama kubwa kupata maji ya kunywa. Mmoja kati ya wakazi hao, Andrew John amesema kwa zaidi ya miaka 20 walikuwa wanatumia maji ya kunywa yanayotoka Hai ila wanasikitishwa hivi sasa kupata zuio hilo. "...

JAMII YASWA KUWAPA NAFASI SAWA WATU WENYE ULEMAVU KATIKA ELIMU YA DINI.

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Dodoma. SHEIKH wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajab, ameitaka jamii kuacha tabia ya kuwatenga watu wenye Ulemavu na badala yake kuwapa nafasi sawa, hususan katika elimu na masuala ya dini, kwani nao ni sehemu muhimu ya jamii na wana haki sawa ya kujifunza na kutekeleza mafundisho ya dini. Sheikh Rajab ameyasema hayo alipo hutubia katika Mashindano ya Kitaifa ya Kuhifadhi Qur’an Tukufu kwa Watu wenye Ulemavu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Riziki Lulida Foundation. Amesema kuwa, mashindano hayo ni ya kipekee kwa kuwa yanawaleta pamoja kundi la watu ambalo kwa muda mrefu limekuwa likisahaulika na kupuuzwa na jamii. " Kwa miaka mingi jamii imekuwa ikiwanyima watu wenye ulemavu fursa mbalimbali bila kutambua kuwa nao ni binadamu kamili wenye haki ya kusoma, kuabudu na kushiriki kikamilifu katika masuala ya dini," amesema Sheikh Rajab. Ameongeza kuwa, kupitia mashindano hayo hatua muhimu imechukuliwa kurejesha heshima, thamani na nafasi yao katika jamii. Aidha, Shei...

SELWA :- ATOA ONYO KALI KWA WASIMAMIZI WA MIRADI IGUNGA.

Picha
  Na Lubango Mleka, Igunga. MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Selwa Hamid amewataka Wasimamizi wa Mafundi na Kamati za ujenzi kusimama  katika nafasi zao kwa lengo la kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa wakati na kuzingatia viwango vya fedha. Selwa ametoa wito huo, wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali katika kata za Jimbo la Manonga wilayani Igunga. "Tujirekebishe kwenye miradi yetu na kuongeza usimamizi kwa sababu hali ya  mafundi kuondoka maeneo ya ujenzi wakati unaendelea  hatukubaliani nayo," amesisitiza na kuongeza kuwa, "Ziogopeni fedha hizi za miradi kama ukoma na mambo ya udalali yasiwepo kwenye miradi, wapeni mafundi wanaofanya kazi ipasavyo."

WAKUU WA IDARA NA VITENGO IGUNGA WAGAWIWA VISHIKWAMBI ILI KUACHANA NA MATUMIZI YA KARATASI.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Igunga. WAKUU wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora,  wamegawiwa Vishikwambi kwa lengo la kuvitumia katika vikao mbalimbali na kuachana na matumizi ya karatasi. Akizungumza baada ya kuwagawia vishikwambi hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Selwa Hamid amesema wanaendelea kumuunga mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika matumizi ya kidijitali. Amesema hatua hiyo, inaendelea kuondoa  mnyororo wa matumizi ya karatasi ambazo hutengenezwa kwa miti, hivyo kuendelea kutunza miti kwa mazigira rafiki kwa mwanadamu. Aidha, amewataka wakuu hao wa Idara na Vitengo kuvitumia vishikwambi hivyo kuongeza ufanisi wa kazi huku akiwasihi kutojaza picha na taarifa zisizohusiana na Menejimenti.

TEITI YAIMARISHA ELIMU KWA UMMA KUHUSU MANUFAA YA RASILIMALI ZA MADINI NA GESI

Picha
Na.Mwandishi Wetu. Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) imesema imeendelea kuhimiza uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimali za nchi, ili kuhakikisha wananchi wananufaika na shughuli za uchimbaji na utafutaji. Akizungumza  jana katika mahojiano maalum,Katibu Mtendaji wa TEITI, Bi. Mariam Mgaya, amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi 57 zinazotekeleza viwango vya kimataifa vya uwazi na uwajibikaji vinavyosimamiwa na EITI. Amesema Tanzania ilijiunga na EITI mwaka 2009, hatua iliyolenga kuimarisha usimamizi bora wa rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia kwa maslahi ya maendeleo endelevu. “Asasi hii inahamasisha wananchi kuelewa hatua zote za mnyororo wa thamani wa rasilimali hizi, ikiwemo ukusanyaji na ufuatiliaji wa mapato,” amesema Bi.Mgaya Bi. Mgaya amebainisha kuwa utekelezaji wa majukumu ya TEITI unasimamiwa na Sheria ya TEITA ya mwaka 2015 ambayo imeainisha jukumu la kuboresha uwazi na uwajibikaji, hasa katika uvunaj...

RADI YAUA WATU WAWILI TABORA

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora WATU wawili wamepoteza maisha kwa kupigwa na radi wakiwa wamejikinga mvua kwenye kibaraza cha nyumba yao iliyoegemewa na mti katika Kijiji cha Songambele, Kata ya Uyowa, Wilayani Kaliua Mkoani hapa. Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa SACP Richard Abwao amethibitisha kutokea tukio hilo Desemba 27 mwaka huu na kuongeza kuwa mbali na waliopoteza maisha watu wengine wawili walijeruhiwa pia. Ametaja waliopoteza maisha kuwa ni Mwagala Marando (19) na Moses Lwega (20) wakulima, wakazi wa kijiji hicho na waliojeruhiwa ni Yohana Peter (18) na George Deusi (18), na wanaendelea kupatiwa matibabu kwenye kituo cha afya. Kamanda Abwao  ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari hasa katika kipindi hiki ambapo mvua zimeendelea kuongezeka na kuwataka wajikinge katika maeneo yaliyo salama ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.  Wakati huo huo, mwili wa mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Hamis Ramadhan, mkazi wa Kata ya Isevya, dereva wa b...

DIWANI AGUSWA NA KERO ZA AKINAMAMA WAJAWAZITO

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Tabora. DIWANI wa Kata ya Chemchem katika halmashauri ya manispaa Tabora kupitia CCM, Bandola Salum Milambo ameanza mikakati ya kutatua kero wanazopata akinamama wajawazito na wagonjwa wengine katika kata yake.  Akizungumza na wanahabari jana ameeleza kuwa baada ya kuapishwa sasa ana kazi moja tu ya kuhakikisha kero zote zinazowakabili wapiga kura wake zinashughulikiwa ipasavyo na mamlaka husika. Amedokeza kuwa kwa kuanzia anaanza na kero ya wajawazito ambao wamekuwa wakilalamikia kutozwa gharama kubwa wanapoenda kuanza kliniki kwenye Kituo cha kutolea huduma za afya cha Town Kliniki, kilichoko hapa Chemchem. ‘Nimepanga kutembelea Kituo hiki (Zahanati ya Town Kliniki) ili kujionea hali ya utoaji huduma lakini pia kufuatilia malalamiko ambayo yametolewa na akinamama wajawazito ya kutozwa gharama kubwa ili wapate huduma za kliniki’, ameeleza. Amesema kuwa utaratibu wa wananchi kuchangia huduma za afya unajulikana, lakini inapobainika kuwa wanatozwa gharama k...

KUONGEZWA KWA SAFARI ZA TRENI ZA SGR ILI KUKIDHI USUMBUFU WALIOUPATA ABIRIA DESEMBA 28, 2025.

Picha

HALI YA MVUA KUBWA NCHINI

Picha
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inapenda kutoa taarifa ya mwenendo wa Mvua Kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali hapa nchini.  Mnamo tarehe 26 hadi 27 Desemba, 2025 Mamlaka iliendelea kutoa Tahadhari ya vipindi vya Mvua Kubwa katika maeneo mengi nchini kuanzia tarehe 26 hadi 29 Desemba, 2025. Kwa mujibu wa Tahadhari hiyo maeneo yaliyotarajiwa kuathirika na vipindi hivi vya mvua kubwa ni pamoja na Mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Dodoma, Singida, Songea, Morogoro, Lindi, Mtwara, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumisha Kisiwa cha Mafia) pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba.  Kuanzia usiku wa kuamkia leo hadi hivi sasa maeneo mengi nchini yameendelea kupata vipindi vya Mvua Kubwa zikiambatana na upepo mkali na hivyo kusababisha uharibifu wa mali na miundombinu katika baadhi ya maeneo hapa nchini. Hadi kufikia saa 3:00 kamili asubuhi ya leo viwango vya mvua kubwa vinavyozidi milimita 50 ndan...

KITUO CHA KUPOOZA UMEME HANDENI KULETA MAPINDUZI YA UWEKEZAJI – NYAMWESE

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Handeni. Mkuu wa Wilaya ya Handeni,  Salum Nyamwese, ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kituo cha kupooza umeme (substation) cha Handeni mkoani Tanga, unaolenga kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wakazi na wawekezaji wa wilaya hiyo. Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho,  Nyamwese amesema kwa sasa Wilaya ya Handeni ina wawekezaji wakubwa katika sekta mbalimbali, hali inayoongeza mahitaji ya nishati ya umeme wa uhakika na wenye nguvu. “Kwa hiyo, kukamilika kwa substation hii kutaleta tumaini jipya kwa wakazi wa Handeni na wawekezaji. Wawekezaji wengi wanatamani kuja kuwekeza Handeni, lakini bado wanasuasua kutokana na kukosekana kwa umeme wa uhakika na wenye uwezo wa kuendesha mitambo yao,” amesema Nyamwese. Ameeleza kuwa mara baada ya kituo hicho kukamilika, kinatarajiwa kuvutia uwekezaji wa uhakika na kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi wilayani humo. “Tuishukuru Serikali chini ya u...

MBUNGE MNZAVA AWAKABIDHI WAZEE 300 BIMA ZA AFYA KUPITIA MAKUYUNI FESTIVAL

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Korogwe. MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Mhe. Timotheo Mnzava, ameendelea kutekeleza mikakati ya kuboresha huduma za afya kwa wazee kwa kugawa Bima za Afya kwa zaidi ya wazee 300 waliohudhuria Makuyuni Festival, tamasha lililowakutanisha wakazi wa maeneo mbalimbali ya jimbo hilo. Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mhe. Mnzava amesema  hatua hiyo inalenga kuhakikisha wazee wanapata huduma bora za matibabu bila vikwazo vya kifedha, huku akisisitiza kuwa afya ya wazee ni sehemu muhimu ya ustawi wa jamii.  "Bima hizo zitawawezesha wazee kupata matibabu kwa wakati wowote na katika vituo vilivyosajiliwa, hatua inayotafsiriwa kama kupunguza mzigo wa gharama za afya kwa familia nyingi za kipato cha chini."amesema Mhe.Mnzava Katika tamasha hilo, Mbunge Mnzava pia alipata fursa ya kushiriki chakula cha pamoja na wazee, watu wenye ulemavu, vijana na wananchi wengine waliohudhuria, akisema kitendo hicho ni sehemu ya kuimarisha mshikamano na kuonyesha ushiriki...