Machapisho

WAKUU WA IDARA NA VITENGO IGUNGA WAGAWIWA VISHIKWAMBI ILI KUACHANA NA MATUMIZI YA KARATASI.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Igunga. WAKUU wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora,  wamegawiwa Vishikwambi kwa lengo la kuvitumia katika vikao mbalimbali na kuachana na matumizi ya karatasi. Akizungumza baada ya kuwagawia vishikwambi hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Selwa Hamid amesema wanaendelea kumuunga mkono Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika matumizi ya kidijitali. Amesema hatua hiyo, inaendelea kuondoa  mnyororo wa matumizi ya karatasi ambazo hutengenezwa kwa miti, hivyo kuendelea kutunza miti kwa mazigira rafiki kwa mwanadamu. Aidha, amewataka wakuu hao wa Idara na Vitengo kuvitumia vishikwambi hivyo kuongeza ufanisi wa kazi huku akiwasihi kutojaza picha na taarifa zisizohusiana na Menejimenti.

TEITI YAIMARISHA ELIMU KWA UMMA KUHUSU MANUFAA YA RASILIMALI ZA MADINI NA GESI

Picha
Na.Mwandishi Wetu. Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) imesema imeendelea kuhimiza uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimali za nchi, ili kuhakikisha wananchi wananufaika na shughuli za uchimbaji na utafutaji. Akizungumza  jana katika mahojiano maalum,Katibu Mtendaji wa TEITI, Bi. Mariam Mgaya, amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi 57 zinazotekeleza viwango vya kimataifa vya uwazi na uwajibikaji vinavyosimamiwa na EITI. Amesema Tanzania ilijiunga na EITI mwaka 2009, hatua iliyolenga kuimarisha usimamizi bora wa rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia kwa maslahi ya maendeleo endelevu. “Asasi hii inahamasisha wananchi kuelewa hatua zote za mnyororo wa thamani wa rasilimali hizi, ikiwemo ukusanyaji na ufuatiliaji wa mapato,” amesema Bi.Mgaya Bi. Mgaya amebainisha kuwa utekelezaji wa majukumu ya TEITI unasimamiwa na Sheria ya TEITA ya mwaka 2015 ambayo imeainisha jukumu la kuboresha uwazi na uwajibikaji, hasa katika uvunaj...

RADI YAUA WATU WAWILI TABORA

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora WATU wawili wamepoteza maisha kwa kupigwa na radi wakiwa wamejikinga mvua kwenye kibaraza cha nyumba yao iliyoegemewa na mti katika Kijiji cha Songambele, Kata ya Uyowa, Wilayani Kaliua Mkoani hapa. Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa SACP Richard Abwao amethibitisha kutokea tukio hilo Desemba 27 mwaka huu na kuongeza kuwa mbali na waliopoteza maisha watu wengine wawili walijeruhiwa pia. Ametaja waliopoteza maisha kuwa ni Mwagala Marando (19) na Moses Lwega (20) wakulima, wakazi wa kijiji hicho na waliojeruhiwa ni Yohana Peter (18) na George Deusi (18), na wanaendelea kupatiwa matibabu kwenye kituo cha afya. Kamanda Abwao  ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari hasa katika kipindi hiki ambapo mvua zimeendelea kuongezeka na kuwataka wajikinge katika maeneo yaliyo salama ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.  Wakati huo huo, mwili wa mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Hamis Ramadhan, mkazi wa Kata ya Isevya, dereva wa b...

DIWANI AGUSWA NA KERO ZA AKINAMAMA WAJAWAZITO

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Tabora. DIWANI wa Kata ya Chemchem katika halmashauri ya manispaa Tabora kupitia CCM, Bandola Salum Milambo ameanza mikakati ya kutatua kero wanazopata akinamama wajawazito na wagonjwa wengine katika kata yake.  Akizungumza na wanahabari jana ameeleza kuwa baada ya kuapishwa sasa ana kazi moja tu ya kuhakikisha kero zote zinazowakabili wapiga kura wake zinashughulikiwa ipasavyo na mamlaka husika. Amedokeza kuwa kwa kuanzia anaanza na kero ya wajawazito ambao wamekuwa wakilalamikia kutozwa gharama kubwa wanapoenda kuanza kliniki kwenye Kituo cha kutolea huduma za afya cha Town Kliniki, kilichoko hapa Chemchem. ‘Nimepanga kutembelea Kituo hiki (Zahanati ya Town Kliniki) ili kujionea hali ya utoaji huduma lakini pia kufuatilia malalamiko ambayo yametolewa na akinamama wajawazito ya kutozwa gharama kubwa ili wapate huduma za kliniki’, ameeleza. Amesema kuwa utaratibu wa wananchi kuchangia huduma za afya unajulikana, lakini inapobainika kuwa wanatozwa gharama k...

KUONGEZWA KWA SAFARI ZA TRENI ZA SGR ILI KUKIDHI USUMBUFU WALIOUPATA ABIRIA DESEMBA 28, 2025.

Picha

HALI YA MVUA KUBWA NCHINI

Picha
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inapenda kutoa taarifa ya mwenendo wa Mvua Kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali hapa nchini.  Mnamo tarehe 26 hadi 27 Desemba, 2025 Mamlaka iliendelea kutoa Tahadhari ya vipindi vya Mvua Kubwa katika maeneo mengi nchini kuanzia tarehe 26 hadi 29 Desemba, 2025. Kwa mujibu wa Tahadhari hiyo maeneo yaliyotarajiwa kuathirika na vipindi hivi vya mvua kubwa ni pamoja na Mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Dodoma, Singida, Songea, Morogoro, Lindi, Mtwara, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumisha Kisiwa cha Mafia) pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba.  Kuanzia usiku wa kuamkia leo hadi hivi sasa maeneo mengi nchini yameendelea kupata vipindi vya Mvua Kubwa zikiambatana na upepo mkali na hivyo kusababisha uharibifu wa mali na miundombinu katika baadhi ya maeneo hapa nchini. Hadi kufikia saa 3:00 kamili asubuhi ya leo viwango vya mvua kubwa vinavyozidi milimita 50 ndan...

KITUO CHA KUPOOZA UMEME HANDENI KULETA MAPINDUZI YA UWEKEZAJI – NYAMWESE

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Handeni. Mkuu wa Wilaya ya Handeni,  Salum Nyamwese, ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kituo cha kupooza umeme (substation) cha Handeni mkoani Tanga, unaolenga kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wakazi na wawekezaji wa wilaya hiyo. Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho,  Nyamwese amesema kwa sasa Wilaya ya Handeni ina wawekezaji wakubwa katika sekta mbalimbali, hali inayoongeza mahitaji ya nishati ya umeme wa uhakika na wenye nguvu. “Kwa hiyo, kukamilika kwa substation hii kutaleta tumaini jipya kwa wakazi wa Handeni na wawekezaji. Wawekezaji wengi wanatamani kuja kuwekeza Handeni, lakini bado wanasuasua kutokana na kukosekana kwa umeme wa uhakika na wenye uwezo wa kuendesha mitambo yao,” amesema Nyamwese. Ameeleza kuwa mara baada ya kituo hicho kukamilika, kinatarajiwa kuvutia uwekezaji wa uhakika na kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi wilayani humo. “Tuishukuru Serikali chini ya u...

MBUNGE MNZAVA AWAKABIDHI WAZEE 300 BIMA ZA AFYA KUPITIA MAKUYUNI FESTIVAL

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Korogwe. MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Mhe. Timotheo Mnzava, ameendelea kutekeleza mikakati ya kuboresha huduma za afya kwa wazee kwa kugawa Bima za Afya kwa zaidi ya wazee 300 waliohudhuria Makuyuni Festival, tamasha lililowakutanisha wakazi wa maeneo mbalimbali ya jimbo hilo. Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mhe. Mnzava amesema  hatua hiyo inalenga kuhakikisha wazee wanapata huduma bora za matibabu bila vikwazo vya kifedha, huku akisisitiza kuwa afya ya wazee ni sehemu muhimu ya ustawi wa jamii.  "Bima hizo zitawawezesha wazee kupata matibabu kwa wakati wowote na katika vituo vilivyosajiliwa, hatua inayotafsiriwa kama kupunguza mzigo wa gharama za afya kwa familia nyingi za kipato cha chini."amesema Mhe.Mnzava Katika tamasha hilo, Mbunge Mnzava pia alipata fursa ya kushiriki chakula cha pamoja na wazee, watu wenye ulemavu, vijana na wananchi wengine waliohudhuria, akisema kitendo hicho ni sehemu ya kuimarisha mshikamano na kuonyesha ushiriki...

WAZEE TABORA WANENA MAZITO KWA RAIS SAMIA

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora ZIKIWA zimebakia siku chache kumalizika mwaka 2025 na kuanza mwaka mpya wa 2026, wazee wa Mkoa wa Tabora wameeleza kuridhishwa na utendaji wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika awamu yake ya pili baada ya kuingia madarakani. Wameeleza kuwa weledi na ufanisi wa Kiongozi mzuri unapimwa kwa mambo makubwa matatu ambayo ni hali ya usalama wa nchi, kasi ya maendeleo na uchumi, mambo haya yamesimamiwa vizuri na nchi inapiga hatua kubwa. Mzee Elisha Daud Mponeja ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi wa Jadi katika halmashauri ya manispaa Tabora ameeleza kuwa Rais Samia amefanya kazi nzuri sana katika kipindi chake cha miaka minne na hata sasa anaendelea vizuri. Amefafanua kuwa baada ya kukabidhiwa nchi Machi 19, 2021 kutoka kwa mtangulizi wake aliyetangulia mbele za haki, Dkt John Pombe Magufuli, watanzania walishuhudia kasi kubwa ya utekekezaji miradi ya maendeleo katika sekta zote. ‘Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake mambo makubwa yamefanyika ikiw...

ASKOFU MEIVUKIE ATAKA UPENDO, HAKI NA AMANI VIDUMISHWE

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora ASKOFU wa Kanisa la TAG Jimbo la Tabora Kati na Kiongozi wa Kanisa la Kitete Christian Centre (KCC) la Mjini Tabora Rev. Paul Meivukie ameomba upendo, haki na amani viendelee kudumishwa nchini ili jamii iishi kwa utulivu. Ametoa rai hiyo leo kwenye ibada ya sikukuu ya krismas ambapo ameeleza kuwa krismasi ni tukio kubwa linalobeba ujumbe wa upendo, haki na amani kwa watu wote, hivyo mamlaka na jamii kwa ujumla hawana budi kuyadumisha. Amesisitiza kuwa tunapoadhimisha sikukuu hii ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo hatuna budi kumwomba Mungu ili taifa liendelee kuwa na amani na utulivu na upendo na haki viendelee kudumishwa wakati wote ili Mungu aliinue taifa lake. ‘Taifa liliingia kwenye wakati mgumu sana Oktoba 29, 2025 siku ya uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, hili halipaswi kufumbiwa macho, kama taifa tunapaswa kusameheana na kupendana ili kudumishwa amani yetu', amesema. Askofu Meivukie ameasa waumini wa kanisa hilo na jamii kwa ujumla kuishi tabia na...

KONYAGI INATOA FURSA YA KIPEKEE MSIMU HUU WA SIKUU

Picha
Konyagi inatoa fursa ya kipekee mashabiki wake kujishinda Zawadi mbali mbali kupitia maswali mbali mbali.

TANGAZO

Picha
Kwa Matangazo wasiliana nasi kupitia namba 0789852956 na 0624489100. Tunatoa punguzo kwa kila Tangazo katika kipindi hiki cha Msimu wa Sikuu ya Krismas na Mwaka Mpya. Mteja wetu na mdau wetu wa habari wahi mapema......

MIRERANI WAWAPATIA TABASAMU LA SIKUKUU WATOTO YATIMA

Picha
  Na Mwandishi wetu, Mirerani MAMLAKA ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, imewapatia zawadi ya vyakula, mbuzi na fedha taslimu, watoto yatima na waliokuwa wanaishi katika mazingira hatarishi wa kituo cha Light In Africa kwenye kusherehekea sikukuu ya Christmas na mwaka mpya wa 2026 kwa tabasamu. Afisa mtendaji mkuu wa mamlaka ya mji mdogo wa Mirerani, (TEO) Isack Mgaya akizungumza wakati akikabidhi vyakula hivyo ameeleza kwamba gharama walizotumia kuwapatia tabasamu watoto hao ni shilingi 1,847,000. Mgaya amesema lengo lao ni kuwapa tabasamu  kwenye sikukuu ya Christmas na mwaka mpya wa 2026 watoto hao wa kituo cha Light In Africa ambao ni yatima na waliokuwa wanaoishi katika mazingira hatarishi washerehekee kwa furaha. Amesema pamoja na kuwapa fedha taslimu shilingi 220,000 wametumia shilingi 1,627,000 katika kununua mahitaji mbalimbali ikiwemo mbuzi mmoja, nyama kilo 10  na vyakula kwa ajili ya kusherehekea sikukuu hizo za mwisho wa mwaka. Ameele...

WAZIRI SHARIFF AZINDUA JENGO LA MRI HOSPITALI YA ABDULAA MZEE

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Pemba. WAZIRI wa Kazi na Uwekezaji Shariff Ali Shariff amesema Uwepo wa huduma ya MRI katika Hospitali ya Abdulaa Mzee Mkoani, Pemba ni hatua kubwa katika kuimarisha uwezo wa mfumo wetu wa afya na utawezesha wagonjwa kupata uchunguzi wa haraka, sahihi na wa uhakika.  Hayo ameyaeleza katika Hospitali ya Abdulla Mzee Mkoani wakati wa alipofungua jengo la huduma za MRI ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za Miaka 62 ya Mapinduzi Zanzibar.  Waziri Shariff amesema huduma ya MRI itaongeza uwezo wa madaktari kufanya maamuzi ya kitabibu kwa ufanisi zaidi, sambamba na matumizi ya teknolojia ya kisasa katika sekta ya afya na itasaidia kupunguza kuchelewa kwa matibabu, kuokoa maisha na kupunguza gharama kwa familia na Serikali kwa ujumla.  Aidha amesema kuwa uwamuzi wa kuanzisha huduma ya MRI kisiwani Pemba unaonesha wazi dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Nane ya kusogeza huduma muhimu karibu kwa wananchi na kupunguza rufaa zisizo za lazima, kuimarisha ...

BANK YA AMANA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TRA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam. KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda, leo tarehe 24.12.2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Bank ya Amana, Bw. Abubakar Athman Ali, katika ofisi za TRA jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili. Katika kikao hicho, viongozi hao wamejadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano ikiwemo kuboresha mifumo ya ulipaji kodi kupitia taasisi za kifedha, pamoja na kuhamasisha walipakodi kulipa kodi kwa hiari kwa kutumia huduma za kibenki. Bw. Abubakar amesema Bank ya Amana ipo tayari kushirikiana kwa karibu na TRA katika kuhakikisha huduma bora zinapatikana kwa walipakodi, huku akiweka mkazo kwenye uboreshaji wa mifumo na elimu ya kodi kwa wateja wa benki hiyo. Kwa upande wake, Kamishna Mkuu Bw. Mwenda amepongeza ushirikiano huo na kusema kuwa hatua kama hizo zinaimarisha mazingira ya ulipaji kodi na kuchangia katika kukuza mapato ya Taifa.