RADI YAUA WATU WAWILI TABORA
Na Allan Kitwe, Tabora WATU wawili wamepoteza maisha kwa kupigwa na radi wakiwa wamejikinga mvua kwenye kibaraza cha nyumba yao iliyoegemewa na mti katika Kijiji cha Songambele, Kata ya Uyowa, Wilayani Kaliua Mkoani hapa. Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa SACP Richard Abwao amethibitisha kutokea tukio hilo Desemba 27 mwaka huu na kuongeza kuwa mbali na waliopoteza maisha watu wengine wawili walijeruhiwa pia. Ametaja waliopoteza maisha kuwa ni Mwagala Marando (19) na Moses Lwega (20) wakulima, wakazi wa kijiji hicho na waliojeruhiwa ni Yohana Peter (18) na George Deusi (18), na wanaendelea kupatiwa matibabu kwenye kituo cha afya. Kamanda Abwao ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari hasa katika kipindi hiki ambapo mvua zimeendelea kuongezeka na kuwataka wajikinge katika maeneo yaliyo salama ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza. Wakati huo huo, mwili wa mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Hamis Ramadhan, mkazi wa Kata ya Isevya, dereva wa b...