Machapisho

WAZIRI MAVUNDE AZINDUA RASMI SHUGHULI ZA UJENZI WA MGODI MKUBWA WA MADINI YA KINYWE MAHENGE

Picha
Na Mwandishi Wetu, Mahenge -Morogoro.  WAZIRI wa Madini, Mhe. Anthony Peter Mavunde (MB), amezindua rasmi shughuli za ujenzi wa mgodi wa madini ya graphite wa Kinywe, unaotekelezwa na kampuni ya Faru Graphite Corporation kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania (hisa 16%) na Black Rock Mining Limited (hisa 84%) ikiwa ni hatua kubwa katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya sekta ya madini nchini. Akizungumza katika hafla iliyofanyika leo tarehe 9 Oktoba 2025 katika eneo la Mahenge, Wilaya ya Ulanga, Mkoa wa Morogoro, Mhe. Mavunde amesema uzinduzi huo ni ishara ya kasi mpya ya uendelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati katika Sekta ya Madini, kutokana na maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.  “Mradi huu si uchimbaji wa rasilimali pekee, bali ni injini ya maendeleo itakayochochea ukuaji wa viwanda, biashara, ajira, na ustawi wa jamii katika eneo la Mahenge kwa ujumla” amesema Waziri Mavunde. Kwa mujibu wa Waziri Mavunde, mradi wa Mahenge unatarajiwa kugharimu takriban...

WANANCHI ITILIMA WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUUNDA MFUMO WA MALIPO YA KIFUTA JASHO /MACHOZI

Picha
  Na Mwandishi Wetu- Itilima. Wananchi wa vijiji vya Nyantugutu, Lung'wa na Nding'ho vya Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu wameipongeza Serikali kwa kuunda na kuboresha   mfumo wa ukusanyaji  wa taarifa  za wanyamapori  wakali na waharibifu (Problem animal information  system- PAIS) ambao umerahisisha malipo ya kifuta jasho (machozi) pindi madhara ya wanyamapori wakali na waharibifu yanapotokea kwa wananchi. Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ndi'hgo , Bi. Salome Kambona katika mkutano wa hadhara wa kuelimisha wananchi namna ya kukabiliana na changamoto za wanyamapori wakali na waharibifu uliofanyika kijiji cha Ndi'hgo ,Wilaya ya Itilima leo Oktoba 9, 2025. "Tunaishukuru Serikali kwa mfumo huu ambao ndani ya siku saba mwananchi atatakiwa awe ametoa taarifa ya madhara yaliyotokana na mnyamapori ili aweze kulipwa" amesema Bi.Salome. Naye, Mkazi wa Kijiji cha Nyantugutu, Bw. Mosses Saguda amesema mfumo wa PAIS umepunguza urasimu na usumbufu wa m...

KIWANDA CHA KUSAFISHA DHAHABU CHUNYA CHAKAMILIKA , SERIKALI YATIMIZA AHADI

Picha
  ***Ni kupitia Kampuni ya Kitanzania ya Giant Equipment and Mashine’s Limited* *Kina uwezo wa Kusafisha kilo 20 za Dhahabu kwa Siku* *Mkuu wa Wilaya  Alhaji Batenga asema Chunya itajitosheleza kwenye mnyororo wa Madini* Na Mwandishi Wetu, Chunya. CHUNYA imepiga hatua kubwa baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Kiwanda cha Kusafisha Dhahabu cha Giant Equipment and Machine’s Limited. Kiwanda hiki kina uwezo wa kusafisha kilo 20 za dhahabu kwa siku kwa usafi (purity) wa asilimia 99.9 na kiko mbioni kuanza uzalishaji rasmi, baada ya kukamilika kwa baadhi ya taratibu za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) . Akizungumza katika mahojiano maalum na timu ya Madini Diary kutoka Wizara ya Madini, Meneja Uendeshaji wa Kampuni hiyo Hassan Pazi amesema tayari majaribio ya kusafisha dhahabu kiwandani hapo yamefanyika kwa awamu tatu tofauti na zote zimetoa matokeo ya kiwango cha kusafisha hadi asilimia 99.9, jambo linaloashiria kuwa dhahabu inayosafishwa na kiwanda hicho inakidhi vigezo vya kununuliwa n...

WANAOHAMASISHA MAANDAMANO MTANDAONI HAWAPO NCHINI NA HAWAITAKII MEMA TANZANIA.

Picha
Na Mwandishi Wetu. WANANCHI na Wapiga kura wa Tanzania wamesisitizwa kupuuza na kutokubali kuhadaika na watu na baadhi ya wanasiasa wanaohamasisha vurugu na maandamano Jumatano ya Oktoba 29, 2025 siku ya upigaji wa kura kwenye uchaguzi Mkuu wa Tanzania. Wananchi tuliozungumza nao akiwemo Shaban Maulid na Adrian Malikale wamewasihi wananchi kujifunza na kutathmini athari za vurugu na machafuko kwa jamii hasa kwa watoto, wanawake na wazee, wakiahidi kutoandamana na kusisitiza kufuatwa kwa taratibu na sheria zinazotambulika kisheria wakati wa zoezi la upigaji kura. "Ni muhimu sana kutokubali kushawishiwa au kudanganyika kwenda kuandamana kwa namna yoyote ile ifikapo Oktoba 29, 2025. Tujitokeze tupige kura, turudi nyumbani kuendelea na shughuli zetu kama mimi mama lishe nitakavyofanya. " amesema Bi. Zuhura Mohamed. Tayari serikali ya Tanzania kupitia kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imewahakikishia watanzania wote utulivu, amani na usalama siku hiyo ya upigaji wa kura, wakihimiz...

RC SENYAMULE; "THAMANI YA ARDHI YAPAA,DODOMA SASA NI KITUO KIKUU CHA MAENDELEO NCHINI.

Picha
Na Hamida Ramadhan, Dodoma. MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, amesema kuwa thamani ya ardhi katika jiji la Dodoma inaendelea kupanda kwa kasi kila siku, kutokana na mabadiliko makubwa ya kiuchumi, kijamii na kimiundombinu yanayoendelea kujitokeza katika mji huo ambao sasa ni makao makuu ya nchi. Akizungumza jijini Dodoma katika kikao na viongozi wa dini mbalimbali, Senyamule alisema kuwa mabadiliko ya Dodoma kutoka kuwa mji mdogo hadi kuwa jiji linaloongoza kwa kasi ya ukuaji yamefungua milango ya uwekezaji, ajira, na ustawi wa wananchi kwa ujumla. “Zamani ukisema unaishi Dodoma mtu anakushangaa, lakini leo hii Dodoma imekuwa ndoto ya kila Mtanzania. Kila mtu anatamani kuwa sehemu ya mabadiliko haya Ardhi ya Dodoma sasa ni dhahabu  thamani yake inapanda kila kukicha,” amesema Senyamule. Aidha, amebainisha kuwa serikali imeweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji na wananchi kwa kuhakikisha huduma muhimu kama maji safi na salama, umeme wa uhakika, barabara za lami, pamoja na ...

MGOMBEA UBUNGE KUPITIA CHAMA CHA WANANCHI (CUF) AUAWA KWA KUCHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Siha -Kilimanjaro. Mgombea ubunge wa Jimbo la Siha kupitia Chama cha Wananchi (CUF) mkoani Kilimanjaro, Daudi Wilbard Ntuyehabi, ameuawa na wananchi baada ya kudaiwa kumchoma kisu mtu mmoja aitwaye Abdul Issah Mohamed.  Tukio hilo lilitokea usiku wa Oktoba 7, 2025 katika Kijiji cha Kilingi, wilayani Siha. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa, tukio hilo lilitokea majira ya saa 1:30 usiku, ambapo marehemu Daudi anadaiwa kumchoma kisu tumboni Abdul Issah Mohamed na kumsababishia utumbo kutoka Nike.  Inadaiwa kuwa Abdul alikuwa anajaribu kuingilia ugomvi uliokuwa ukiendelea kati ya Daudi na kijana mwingine waliokuwa wakizozana kuhusu deni la fedha wakiwa kwenye baa ya pombe maarufu kama ‘grocery’. Baada ya tukio hilo, wananchi waliokuwepo eneo hilo walimshambulia Daudi hadi kusababisha kifo chake. Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi linawashikilia watu nane kwa tuhuma za kujichukulia sheria mkononi,Kamanda Maigwa ametaja majina y...

GST NA CHUO KIKUU CHA GOETHE WAFANYA UTAFITI MLIMA OLDOINYO LENGAI

Picha
  Na Mwandishi Wetu - Arusha. TAASISI ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kwa kushirikiana na wataalam wa jiosayansi kutoka Chuo Kikuu cha Goethe  cha nchini  Ujerumani wafanya utafiti wa jiosayansi katika Mlima Oldoinyo Lengai.  Akielezea kuhusu utafiti huo, Mkurugenzi wa Huduma za Jiolojia GST, Dkt. Ronald Massawe amesema kuwa, Mlima Oldoinyo Lengai ni moja ya milima ya volkano ambayo ipo hai, lakini pia ni mlima pekee duniani ambao volkano yake inatoa lava ya aina ya “natrocarbonatite” ambapo lava hii inapokauka na kugeuka vumbi, huweza kuwa na madhara ya kiafya kwa binadamu na wanyama, hasa inapovutwa kupitia hewa.  Akifafanua  kuhusu malengo  ya utafiti huo, Dkt. Massawe amesema kuwa, kulingana na mfumo wa kijiolojia ndani ya mlima, utafiti huo una malengo makubwa matatu ambayo ni: kuchunguza muundo wa ndani wa volkano, kubaini maeneo ya hifadhi ya magma na njia zake, pamoja na kutambua mabadiliko ya tabaka la miamba katika Ukanda wa Z...

WAZIRI MKUU ATOA MAAGIZO WIZARA YA MADINI

Picha
  _ Na Mwandishi Wetu -Lindi. WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Madini kufanya ufuatiliaji wa makampuni ya madini ambayo yameshilikilia maeneo kwa muda mrefu lakini hawajayaendeleza mpaka sasa yakiwemo makampuni matatu wilayani Ruangwa Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa makampuni ya Nachu, Uranex na Paco Gems Ltd yanapaswa kusema hatma ya maeneo waliyoyahodhi kwa muda mrefu vinginevyo ardhi hiyo itarudishwa kwa wananchi. Ametoa agizo hilo leo Jumanne (Oktoba 07, 2025) alipotembelea kampuni ya uchimbaji wa madini Huaer International Limited katika kijiji cha Ng’au Ruangwa mkoani Lindi. “Kampuni ya Paco Gems tangu 2009 mpaka leo hakuna maendeleo, tunatoka Utanex pale Chunyu, wameshalipa fidia tangu 2012 lakini mpaka leo hii hakuna maendeleo yoyote, ipo kampuni ya Nachu ambayo ilipata heshima ya kusaini mkataba mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mpaka leo hii wamepotea na hakuna taarifa.” Mheshimiwa Majaliwa ameipongeza kampuni ya Huaer International Limited...

WALIMU WAPAZA SAUTI CHANGAMOTO KWA WALIMU WA KIKE VIJIJINI

Picha
Na Hamida Ramadhan, Dodoma KATIKA  juhudi za kuibua na kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili walimu wa kike wanaofundisha maeneo ya vijijini, Shirika la ActionAid Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa elimu limeandaa kikao kazi maalum jijini Dodoma kujadili ripoti ya utafiti wa kazi zinazofanywa na walimu wakike katika shule za msingi za vijijini Tanzania Bara na Visiwani. Kikao hicho kimewakutanisha maafisa elimu wa shule za msingi na sekondari, walimu wa kike na wa kiume, wawakilishi wa vyama vya walimu kutoka ngazi ya wilaya Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na wawakilishi kutoka Wizara ya Elimu, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Utumishi na wadau wengine wa elimu kutoka taasisi mbalimbali huku kikihusisha walimu 12 kutoka mikoa 12 nchini ambao walishiriki moja kwa moja katika utafiti huo. Akizungumza katika kikao hicho Mratibu wa Programu za Vijana kutoka ActionAid Tanzania Arif Fazel alisema lengo kuu la kikao ni kufanya tathmini ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa kupit...

MHANDISI MATIVILA AMTAKA MKANDARASI ANAYEJENGA DARAJA LA MOHORO KUKAMILISHA UJENZI KWA WAKATI

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Rufiji- Pwani NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila amemtaka Mkandarasi anayejenga daraja la Mohoro (MAC CONTRACTORS COMPANY LTD) lenye urefu wa mita 100 wilayani Rufiji mkoani Pwani kukamilisha ujenzi wa daraja hilo kwa wakati. Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo, Mhandisi Mativila amesema fedha za mradi huo zipo hivyo, amemsisitiza Mhandisi Mshauri anayesimamia mradi huo kumsimamia Mkandarasi akamilishe kazi hiyo kwa wakati ili kutatua changamoto ya usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa kata ya Mohoro. "Mliomba fedha kutokana na kazi hii kuongezeka, Serikali imeongeza fedha 50% ili kazi hii ikamilike, zipo kazi ndogondogo zinaweza kuendelea kufanyika, hivyo nasisitiza kazi hii ikamilike kwa wakati", amesema. Aidha, amewataka Wakandarasi wazawa wajitahidi kukamilisha miradi kwa wakati ili Serikali iendelee kufanya kazi nyingi na Wakandarasi wa Kitanzania ba...