Machapisho

WANAOHAMASISHA MAANDAMANO MTANDAONI HAWAPO NCHINI NA HAWAITAKII MEMA TANZANIA.

Picha
Na Mwandishi Wetu. WANANCHI na Wapiga kura wa Tanzania wamesisitizwa kupuuza na kutokubali kuhadaika na watu na baadhi ya wanasiasa wanaohamasisha vurugu na maandamano Jumatano ya Oktoba 29, 2025 siku ya upigaji wa kura kwenye uchaguzi Mkuu wa Tanzania. Wananchi tuliozungumza nao akiwemo Shaban Maulid na Adrian Malikale wamewasihi wananchi kujifunza na kutathmini athari za vurugu na machafuko kwa jamii hasa kwa watoto, wanawake na wazee, wakiahidi kutoandamana na kusisitiza kufuatwa kwa taratibu na sheria zinazotambulika kisheria wakati wa zoezi la upigaji kura. "Ni muhimu sana kutokubali kushawishiwa au kudanganyika kwenda kuandamana kwa namna yoyote ile ifikapo Oktoba 29, 2025. Tujitokeze tupige kura, turudi nyumbani kuendelea na shughuli zetu kama mimi mama lishe nitakavyofanya. " amesema Bi. Zuhura Mohamed. Tayari serikali ya Tanzania kupitia kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imewahakikishia watanzania wote utulivu, amani na usalama siku hiyo ya upigaji wa kura, wakihimiz...

RC SENYAMULE; "THAMANI YA ARDHI YAPAA,DODOMA SASA NI KITUO KIKUU CHA MAENDELEO NCHINI.

Picha
Na Hamida Ramadhan, Dodoma. MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, amesema kuwa thamani ya ardhi katika jiji la Dodoma inaendelea kupanda kwa kasi kila siku, kutokana na mabadiliko makubwa ya kiuchumi, kijamii na kimiundombinu yanayoendelea kujitokeza katika mji huo ambao sasa ni makao makuu ya nchi. Akizungumza jijini Dodoma katika kikao na viongozi wa dini mbalimbali, Senyamule alisema kuwa mabadiliko ya Dodoma kutoka kuwa mji mdogo hadi kuwa jiji linaloongoza kwa kasi ya ukuaji yamefungua milango ya uwekezaji, ajira, na ustawi wa wananchi kwa ujumla. “Zamani ukisema unaishi Dodoma mtu anakushangaa, lakini leo hii Dodoma imekuwa ndoto ya kila Mtanzania. Kila mtu anatamani kuwa sehemu ya mabadiliko haya Ardhi ya Dodoma sasa ni dhahabu  thamani yake inapanda kila kukicha,” amesema Senyamule. Aidha, amebainisha kuwa serikali imeweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji na wananchi kwa kuhakikisha huduma muhimu kama maji safi na salama, umeme wa uhakika, barabara za lami, pamoja na ...

MGOMBEA UBUNGE KUPITIA CHAMA CHA WANANCHI (CUF) AUAWA KWA KUCHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Siha -Kilimanjaro. Mgombea ubunge wa Jimbo la Siha kupitia Chama cha Wananchi (CUF) mkoani Kilimanjaro, Daudi Wilbard Ntuyehabi, ameuawa na wananchi baada ya kudaiwa kumchoma kisu mtu mmoja aitwaye Abdul Issah Mohamed.  Tukio hilo lilitokea usiku wa Oktoba 7, 2025 katika Kijiji cha Kilingi, wilayani Siha. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa, tukio hilo lilitokea majira ya saa 1:30 usiku, ambapo marehemu Daudi anadaiwa kumchoma kisu tumboni Abdul Issah Mohamed na kumsababishia utumbo kutoka Nike.  Inadaiwa kuwa Abdul alikuwa anajaribu kuingilia ugomvi uliokuwa ukiendelea kati ya Daudi na kijana mwingine waliokuwa wakizozana kuhusu deni la fedha wakiwa kwenye baa ya pombe maarufu kama ‘grocery’. Baada ya tukio hilo, wananchi waliokuwepo eneo hilo walimshambulia Daudi hadi kusababisha kifo chake. Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi linawashikilia watu nane kwa tuhuma za kujichukulia sheria mkononi,Kamanda Maigwa ametaja majina y...

GST NA CHUO KIKUU CHA GOETHE WAFANYA UTAFITI MLIMA OLDOINYO LENGAI

Picha
  Na Mwandishi Wetu - Arusha. TAASISI ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kwa kushirikiana na wataalam wa jiosayansi kutoka Chuo Kikuu cha Goethe  cha nchini  Ujerumani wafanya utafiti wa jiosayansi katika Mlima Oldoinyo Lengai.  Akielezea kuhusu utafiti huo, Mkurugenzi wa Huduma za Jiolojia GST, Dkt. Ronald Massawe amesema kuwa, Mlima Oldoinyo Lengai ni moja ya milima ya volkano ambayo ipo hai, lakini pia ni mlima pekee duniani ambao volkano yake inatoa lava ya aina ya “natrocarbonatite” ambapo lava hii inapokauka na kugeuka vumbi, huweza kuwa na madhara ya kiafya kwa binadamu na wanyama, hasa inapovutwa kupitia hewa.  Akifafanua  kuhusu malengo  ya utafiti huo, Dkt. Massawe amesema kuwa, kulingana na mfumo wa kijiolojia ndani ya mlima, utafiti huo una malengo makubwa matatu ambayo ni: kuchunguza muundo wa ndani wa volkano, kubaini maeneo ya hifadhi ya magma na njia zake, pamoja na kutambua mabadiliko ya tabaka la miamba katika Ukanda wa Z...

WAZIRI MKUU ATOA MAAGIZO WIZARA YA MADINI

Picha
  _ Na Mwandishi Wetu -Lindi. WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Madini kufanya ufuatiliaji wa makampuni ya madini ambayo yameshilikilia maeneo kwa muda mrefu lakini hawajayaendeleza mpaka sasa yakiwemo makampuni matatu wilayani Ruangwa Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa makampuni ya Nachu, Uranex na Paco Gems Ltd yanapaswa kusema hatma ya maeneo waliyoyahodhi kwa muda mrefu vinginevyo ardhi hiyo itarudishwa kwa wananchi. Ametoa agizo hilo leo Jumanne (Oktoba 07, 2025) alipotembelea kampuni ya uchimbaji wa madini Huaer International Limited katika kijiji cha Ng’au Ruangwa mkoani Lindi. “Kampuni ya Paco Gems tangu 2009 mpaka leo hakuna maendeleo, tunatoka Utanex pale Chunyu, wameshalipa fidia tangu 2012 lakini mpaka leo hii hakuna maendeleo yoyote, ipo kampuni ya Nachu ambayo ilipata heshima ya kusaini mkataba mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mpaka leo hii wamepotea na hakuna taarifa.” Mheshimiwa Majaliwa ameipongeza kampuni ya Huaer International Limited...

WALIMU WAPAZA SAUTI CHANGAMOTO KWA WALIMU WA KIKE VIJIJINI

Picha
Na Hamida Ramadhan, Dodoma KATIKA  juhudi za kuibua na kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili walimu wa kike wanaofundisha maeneo ya vijijini, Shirika la ActionAid Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa elimu limeandaa kikao kazi maalum jijini Dodoma kujadili ripoti ya utafiti wa kazi zinazofanywa na walimu wakike katika shule za msingi za vijijini Tanzania Bara na Visiwani. Kikao hicho kimewakutanisha maafisa elimu wa shule za msingi na sekondari, walimu wa kike na wa kiume, wawakilishi wa vyama vya walimu kutoka ngazi ya wilaya Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na wawakilishi kutoka Wizara ya Elimu, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Utumishi na wadau wengine wa elimu kutoka taasisi mbalimbali huku kikihusisha walimu 12 kutoka mikoa 12 nchini ambao walishiriki moja kwa moja katika utafiti huo. Akizungumza katika kikao hicho Mratibu wa Programu za Vijana kutoka ActionAid Tanzania Arif Fazel alisema lengo kuu la kikao ni kufanya tathmini ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa kupit...

MHANDISI MATIVILA AMTAKA MKANDARASI ANAYEJENGA DARAJA LA MOHORO KUKAMILISHA UJENZI KWA WAKATI

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Rufiji- Pwani NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila amemtaka Mkandarasi anayejenga daraja la Mohoro (MAC CONTRACTORS COMPANY LTD) lenye urefu wa mita 100 wilayani Rufiji mkoani Pwani kukamilisha ujenzi wa daraja hilo kwa wakati. Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo, Mhandisi Mativila amesema fedha za mradi huo zipo hivyo, amemsisitiza Mhandisi Mshauri anayesimamia mradi huo kumsimamia Mkandarasi akamilishe kazi hiyo kwa wakati ili kutatua changamoto ya usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa kata ya Mohoro. "Mliomba fedha kutokana na kazi hii kuongezeka, Serikali imeongeza fedha 50% ili kazi hii ikamilike, zipo kazi ndogondogo zinaweza kuendelea kufanyika, hivyo nasisitiza kazi hii ikamilike kwa wakati", amesema. Aidha, amewataka Wakandarasi wazawa wajitahidi kukamilisha miradi kwa wakati ili Serikali iendelee kufanya kazi nyingi na Wakandarasi wa Kitanzania ba...

NISHATI YAWASILISHA MIPANGO YA KIMKAKATI KUTEKELEZA DIRA YA TAIFA 2050

Picha
*📌 Ni katika kikao kazi na Tume ya Taifa ya Mipango.* *📌Mradi wa usafirishaji umeme Chalinze–Dodoma ni miongoni mwa miradi ya kipaumbele kufanikisha Dira 2050,* *📌Wizara ya Nishati na Tume ya Mipango kushirikiana kwa karibu kusimamia miradi ya Nishati kufanikisha malengo ya Dira 2050.* Na Hamida Ramadhani, Dodoma. KATIBU Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, amekutana na wataalam kutoka Tume ya Taifa ya Mipango wakiongozwa na Naibu Katibu Mtendaji – Menejimenti ya Utendaji na Tathmini, Dkt. Linda  Ezekiel kwa lengo la kujadili namna ambavyo Wizara na Taasisi zake zimejipanga kutekeleza miradi ya kimkakati ya nishati inayochangia katika kufanikisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Msingi wa kikao hicho umetokana na  Sekta ya Nishati kuainishwa katika Dira 2050 kuwa ni moja ya  vichocheo vitano vitakavyoongeza kasi ya kufikia malengo ya Dira hiyo, ikielezwa kuwa Nishati ya uhakika ni nyenzo muhimu katika kuchochea maendeleo ya viwanda na shughuli ...

SERIKALI YASAINI MKATABA WA NYONGEZA NA KAMPUNI YA VIETTEL GLOBAL KUBORESHA MAWASILIANO NCHINI

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma. SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Wizara ya Mawasilianio na Teknolojia ya Habari, imesaini mkataba wa nyongeza na Kampuni ya Viettel Global Joint Stock, ya Vietnam wenye lengo la kufikisha huduma za mawasiliano katika maeneo ambayo bado hayajafikiwa na mtandao wa mawasiliano. Hafla ya utiaji saini wa mkataba huo imefanyika leo katika Ofisi za Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mji wa Serikali Mtumba, ikishuhudiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. Adolf Ndunguru, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Majadiliano. Bw. Ndunguru ameeleza kuwa mkataba huu wa nyongeza unalenga kuimarisha utekelezaji wa makubaliano ya awali kwa kuhakikisha huduma za mawasiliano zinawafikia Watanzania wote, hususan walioko vijijini.  Aidha, amebainisha kuwa nyongeza hiyo pia inashughulikia changamoto zilizojitokeza awali, ikiwemo suala la kupeleka huduma za mawasiliano katika maeneo am...

WANANCHI WA SHIGELA-BUSEGA WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA FISI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Simiyu. Wananchi wa Kijiji cha Shigela, Wilaya ya Busega mkoani Simiyu wametakiwa kuwa waangalifu na kuchukua tahadhari dhidi ya fisi wanaoripotiwa kuvamia makazi ya watu na kuleta hofu katika jamii. Rai hiyo imetolewa  Oktoba 6, 2025 na Afisa Uhifadhi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Lusato Masinde, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo ambapo timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, TAWA na Maafisa Wanyamapori wa Halmashauri inaendelea kutoa elimu ya uhifadhi mkoani humo ili kupunguza madhara yatokanayo na wanyamapori wakali na waharibifu.  “Tuchukue tahadhari kubwa, hatuko salama kwa sababu katika mazingira yetu hawa wanyamapori wapo na kuna vichaka na mapango mengi,” amesisitiza  Masinde. Ameongeza kuwa watoto ndio waathirika wakubwa wa mashambulizi ya fisi, hivyo wananchi wanapaswa kuwa makini na kuhakikisha wanawalinda ipasavyo, hasa wakati wa jioni na usiku. Kwa upande wake, Afisa Maliasi...