WANANCHI WA SHIGELA-BUSEGA WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA FISI
Na Mwandishi Wetu, Simiyu. Wananchi wa Kijiji cha Shigela, Wilaya ya Busega mkoani Simiyu wametakiwa kuwa waangalifu na kuchukua tahadhari dhidi ya fisi wanaoripotiwa kuvamia makazi ya watu na kuleta hofu katika jamii. Rai hiyo imetolewa Oktoba 6, 2025 na Afisa Uhifadhi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Lusato Masinde, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo ambapo timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, TAWA na Maafisa Wanyamapori wa Halmashauri inaendelea kutoa elimu ya uhifadhi mkoani humo ili kupunguza madhara yatokanayo na wanyamapori wakali na waharibifu. “Tuchukue tahadhari kubwa, hatuko salama kwa sababu katika mazingira yetu hawa wanyamapori wapo na kuna vichaka na mapango mengi,” amesisitiza Masinde. Ameongeza kuwa watoto ndio waathirika wakubwa wa mashambulizi ya fisi, hivyo wananchi wanapaswa kuwa makini na kuhakikisha wanawalinda ipasavyo, hasa wakati wa jioni na usiku. Kwa upande wake, Afisa Maliasi...