JESHI LA POLISI LATAKIWA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA WADAU WA UCHAGUZI NCHINI.
Na Mwandishi Wetu, Moshi. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema ni muhimu Jeshi la Polisi kuimarisha ushirikiano wa karibu na wadau wote wa uchaguzi, hatua ambayo itasaidia kuhakikisha kila mdau anatendewa haki, na kuondoa tofauti zinazoweza kusababisha migongano. Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika katika ukumbi wa Chuo Cha Polisi (CCP) Moshi Mkoani Kilimanjaro. Amesema Baadhi ya maeneo muhimu ya ushirikiano ni pamoja na kuhakikisha mikutano ya kampeni inafanyika kwenye maeneo yaliyoruhusiwa na ndani ya muda uliopangwa, Kuzuia maandamano yasiyo na kibali, kuimarisha ulinzi wa wagombea na viongozi wa vyama vya kisiasa, bila kujali vyama vyao au itikadi zao pamoja na kudhibiti misongamano mikubwa ya watu ili kuhakikisha shughuli nyingine za kijamii na kiuchumi zinaendelea bila usumbufu. Pia Makamu wa Rais amelitaka Jeshi la Polisi ku...