BODA BODA KUSHIRIKI KUPIGA KURA OCTOBA 29,2025.

 



Waahidi kumpigia kura za kishindo Dkt Samia.

Na Hamida Ramadhani, Dar es Salaam.

MWENEYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) ambaye pia ni Mratibu wa Kampeni za CCM Jijini DSM, Leo amekutana na Maafisa Usafirishaji (Boda Boda) wa Kata ya Kinyerezi Jimbo la Segerea, Wilaya ya Ilala jijiji Dar es Salaam.

Chatanda amewataka kutofuata maudhui machafu yanayorushwa kwenye mitandao ya kijamii kutoka kwa baadhi ya wanasiasa wa upinzani ambayo hawana nia njema na Taifa la Tanzania, Badala yake wajiamini na kujitokeza kwa wingi kupiga kura ya ndiyo kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



Aidha amewataka pia kumchagua Mgombea Ubunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Kamoli, pamoja na Madiwani wote wa Kata ndani ya Jimbo la Segerea kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).












Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.