WANANCHI WAHIMIZWA KUTUMIA LANDMAX KUEPUKA UTAPELI WA ARDHI
Na Hamida Ramadhan,Dodoma MBUNGE wa Jimbo la Mbozi, Onesmo Mnkondya, amewataka wananchi na madalali wanaohusika na biashara ya ardhi kutumia huduma za Landmax Real Estate Company Limited ili kufanya uwekezaji kwa usalama na kuondokana na migogoro inayotokana na mauzo au ununuzi usio rasmi wa ardhi. Mnkondya, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Landmax Real Estate Company Limited, amesema hayo Juni 24, 2026 jijini Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofisi za kampuni hiyo. Amesema Landmax imeanzishwa kwa lengo la kuwasaidia wananchi kupata ardhi salama na makazi bora huku ikichangia kupunguza migogoro ya ardhi. Aidha, amebainisha kuwa kampuni hiyo inatoa huduma mbalimbali ikiwemo uuzaji na ununuzi wa ardhi na mali isiyohamishika, ushauri wa uwekezaji wa ardhi, usimamizi wa mali, urasimishaji wa nyaraka za ardhi, uendelezaji wa miradi, tafiti za soko pamoja na ushirikiano katika miradi ya maendeleo. “Tunawaalika wananchi na madalali wote wanaotaka kununua au kuuza ardhi kufika ofisi...