Machapisho

KAPINGA: DHANA YA TAKA SIFURI INAFUNGUA FURSA ZA BIASHARA NA VIWANDA.

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Istanbul-Ururuki.  WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, amesema dhana ya taka sifuri na urejeshaji bidhaa ni fursa muhimu ya kukuza sekta ya viwanda, kuongeza thamani ya malighafi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa. Akizungumza katika kikao cha mawaziri kilichofanyika jijini Istanbul nchini Uturuki, Juni 5, 2026, kilichobeba mada ya Mageuzi ya Kijani ya Viwanda, Mtazamo wa taka sifuri na urejeshaji bidhaa, Kapinga amesema Tanzania inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuimarisha sekta ya viwanda huku ikisisitiza matumizi bora ya rasilimali na uhifadhi wa mazingira. Ameeleza kuwa dhana ya taka sifuri na urejeshaji bidhaa inatoa fursa kwa nchi zinazoendelea kupitia matumizi endelevu ya malighafi, kupunguza upotevu baada ya mavuno, kupunguza uzalishaji wa taka na kuongeza thamani ya bidhaa zinazotengenezwa viwandani. Kapinga amesema Serikali ya Tanzania imeendelea kuunganisha masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika s...

OLE MILLYA AKEMEA UUZWAJI ARDHI SIMANJIRO

Picha
  Na Mwandishi wetu, Mirerani.  NAIBU Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki James Ole Millya ambaye pia ni Mbunge wa Simanjiro Mkoani Manyara, amekemea vikali uuzwaji holela wa ardhi unafanywa baadhi ya viongozi wa vijiji. Ole Millya ameyasema hayo katika Kata ya Naisinyai Wilayani Simanjiro, kwenye ziara ya Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Laban Kihongosi alipohitimisha ziara yake ya siku tatu Mkoani Manyara. Amesema tatizo la uuzwaji holela wa ardhi katika wilaya ya Simanjiro, limekuwa kero kwani baadhi ya viongozi wa vijiji wenye tamaa wanagawa ardhi kwa maslahi yao  "Baadhi ya wenyeviti wanauza ardhi bila kushirikisha mkutano mkuu wa kijiji na baadhi ya wenyeviti wastaafu wanatembea na mihuri na mihutasari iliyopita katika uuzaji wa ardhi," amesema Ole Millya. Ameeleza kwamba wakati mwingine anaona ni vyema hata miradi ya maendeleo isifanyike kwa muda wa mwaka mmoja ili viongozi na jamii kwa ujumla ishuhulikie migogoro ya ar...

MATHIAS CANAL ATWAA TUZO YA USHIRIKI BORA WA KAZI ZA JAMII 2026

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Dodoma.  MWANZILISHI na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni za WAZOHURU MEDIA na WAZOHURU APPARTMENTS, Mathias Canal, ametunukiwa Tuzo ya Ushiriki Bora wa Kazi za Jamii 2026, ikiwa ni kutambua mchango wake mkubwa katika kuhamasisha maendeleo ya jamii kupitia shughuli mbalimbali za kijamii na misaada ya kijamii. Tuzo hiyo iliyotolewa usiku wa Juni 5, 2026 jijini Dodoma katika hafla ya utoaji wa tuzo iliyoandaliwa na Central Zone Awards, tukio lililowakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta tofauti waliotoa mchango wa kipekee katika maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla. Waandaaji wa tuzo hizo wamesema Mathias Canal amestahili kutunukiwa tuzo hiyo kutokana na kujitolea kwake, ushiriki wake wa karibu na jamii pamoja na mchango wake endelevu katika kusaidia makundi mbalimbali yenye uhitaji.  Tuzo hiyo pia imetambua moyo wake wa huruma, uwajibikaji na dhamira ya kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya wananchi. Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Mathia...

MADINI YA MILIONI 993 YAFANYIWA MNADA TANZANITE EXCHANGE CENTRE

Picha
  Na Mwandishi wetu, Mirerani.  MADINI ya Tanzanite ya thamani ya zaidi ya shilingi milioni 993 yameuzwa kwenye minada miwili iliyofanyika hivi karibuni katika jengo la Tanzanite Exchange Centre mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara. Afisa madini mkazi Mirerani (RMO) George Kaseza, ameyasema hayo kwenye ziara ya Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Kenani Laban Kihongosi alipotembelea jengo hilo na kukagua akiwa ameongozana na viongozi wa mkoa na wilaya. Kaseza amesema minada miwili ilifanyika hivi karibuni ambapo mnada wa kwanza wa mabroka ulifanyika Mei 15 mwaka 2026 kwa washiriki 84 na madini ya shilingi 271,270,100 yalinunuliwa. "Mnada wa pili wa dealers ulifanyika Mei 21 mwaka 2026 na madini ya thamani ya shilingi 721,750,000 yalinunuliwa," amesema RMO Kaseza. Amesema jengo la Tanzanite Exchange Centre linamilikiwa na Halamshauri ya Wilaya ya Simanjiro ila linaendeshwa na Tume ya Madini kupitia ofisi yake. Katibu wa NEC, Itikadi Uenezi na Mafunzo K...

CCM YAIPONGEZA FRANONE KWA CSR YA ZAHANATI

Picha
  Na Mwandishi wetu, Mirerani.  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeipongeza kampuni ya Franone Mining & Gem LTD, inayochimba madini ya Tanzanite kitalu C kwa kujenga zahanati ndani ya eneo tengefu la Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, kupitia mpango wa uwajibikaji kwa jamii (CSR). Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenan Laban Kilongozi akizungumza baada ya kukagua ujenzi unaoendelea wa zahanati hiyo ameipongeza kampuni ya Franone kwa kujitoa kwa ajili ya wachimbaji na wadau wa madini. Amesema zahanati hiyo ikikamilika itakuwa inatoa huduma za afya kwa wachimbaji na wadau wa madini ya Tanzanite hivyo ni jambo la kiungwana na la kuungwa mkono. "Nawakupongeza kampuni ya Franone Mining & Gem LTD kwa ujenzi wa zahanati hii, Mkurugenzi Onesmo Mbise hongereni sana, endelea kutoa kwa jamii kwani hautapungukiwa ila utazidi kuongezewa," amesema Kenani. Hata hivyo, Kenani amewaasa wadau wengine wa madini kuiga mfano kwa kampuni ya Franone Mining LTD,  kat...

WAZIRI MAVUNDE ATOA WITO WAMILIKI WOTE WA LESENI ZA UCHIMBAJI WA MADINI KINYWE KUANZA SHUGHULI ZA UCHIMBAJI MARA MOJA.

Picha
   Lengo ni kuifanya Tanzania kuwa kinara wa uzalishaji wa madini kinywe ifikapo Mwaka 2030, Serikali yasaini mkataba wa ubia na  Kampuni za Grafica na Eminent. Aitaka Timu ya majadiliano ya serikali kuanza mchakato wa majadiliano na Wamiliki wa Leseni 27, Amshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha sekta ya madini, Ruangwa kuwa sehemu ya mnyororo wa thamani na teknolojia ya madini kinywe duniani. Na Mwandishi Wetu, Ruangwa, Lindi.  WAZIRI wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde (Mb), ameielekeza Timu ya Majadiliano ya Serikali kwenye Sekta ya Madini (GNT) kuwaita na kufanya nao majadiliano wamiliki wote wa leseni za uchimbaji madini kinywe nchini Tanzania kujadiliana kuhusu ubia wa serikali katika Kampuni hizo na kuwataka kuanza utekelezaji wa uchimbaji kwa mujibu wa masharti ya leseni na Sheria ya Madini Sura ya 123. Ameyasema hayo leo tarehe 30 Mei, 2026 Wilayani Ruangwa aliposhiriki zoezi la utiaji saini na Kampuni za Grafica Resources na Eminent Min...

CHAMA CHA BIBLIA TANZANIA CHA SAMBAZA MAANDIKO ZAIDI YA LAKI TANO MWAKA 2025.

Picha
  Na Wellu Mtaki, Dodoma.  MWENYEKITI wa Bodi ya Chama cha Biblia Tanzania, Askofu Dkt. Mark Malwa Malekana amesema kuwa katika mwaka 2025 chama hicho kimefanikiwa kusambaza jumla ya maandiko 538,544, ikilinganishwa na maandiko 512,650 yaliyosambazwa mwaka 2024.Amesema maandiko hayo yamesambazwa kupitia mifumo na lugha mbalimbali ili kuwafikia Watanzania wengi zaidi. Askofu Malekana ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati wa Mkutano Mkuu wa 40 wa Chama cha Biblia Tanzania. Ameeleza kuwa chama hicho kimeendelea kupata mafanikio makubwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya kueneza Neno la Mungu nchini. Miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na ujenzi wa jengo la kitega uchumi la Bible Plaza, maandalizi ya Kamusi ya Biblia, Itifaki ya Biblia pamoja na uchapishaji wa kitabu cha historia ya Chama cha Biblia Tanzania. Pia chama hicho kimefanikiwa kuzindua Biblia za lugha za Kikagulu na Kihehe kwa lengo la kuwafikia waumini wanaotumia lugha hizo za asili. Kwa upande wake, Katibu Mku...

AHSANTE FOUNDATION WACHINJA NG'OMBE KONDOO NA MBUZI EID AL- ADHA MIRERANI

Picha
  Na Mwandishi wetu, Mirerani.  TAASISI ya Ahsante Foundation Tanzania imechinja ng'ombe 723, mbuzi na kondoo 2,500 na kutoa sadaka kwa watoto yatima, wajane, wahitaji na taasisi za serikali na binafsi, katika kusheherekea sikukuu ya Eid Al-Adha mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara. Meneja mipango wa taarifa ya Ahsante Foundation Tanzania, Omary Gyunda amesema lengo ni kuhakikisha jamii yenye mahitaji inanufaika na sadaka ya sikukuu hiyo ya Idd. Gyunda amesema taarifa ya Ahsante Foundation Tanzania wamechinja ng'ombe 723, mbuzi na kondoo 2,500 kwa ajili ya jamii kushiriki sherehe hiyo bila ubaguzi wa madhehebu katika mji mdogo na maeneo ya jirani. Amesema sadaka hiyo ya nyama ya kuchinja imetolewa kwa watoto yatima, wajane, wahitaji mbalimbali na taasisi za serikali na binafsi za mji mdogo wa Mirerani na majirani zao. "Tumetoa sadaka hiyo ya kuchinja kwa wahitaji hao na taasisi mbalimbali ikiwemo shule za msingi, sekondari, polisi, uhamiaji, zimamoto na ...

WANAMICHEZO 60 KUWAKILISHA SIMANJIRO UMITASHUMTA

Picha
  Na Mwandishi wetu, Simanjiro  WANAFUNZI wanamichezo 60 wa shule ya msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro wamechaguliwa kuiwakilisha Wilaya hiyo kwenye michuano ya michezo mbalimbali katika ngazi ya Mkoa wa Manyara. Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Gracian Max Makota akizungumza wakati akizindua rasmi michuano hiyo katika viwanja vya Mnyalu Complex Mji mdogo wa Mirerani amewaasa wanamichezo hao wanawawakilishe vyema na kuwa washindi katika ngazi ya Mkoa. "Mrudi na vikombe vya ushindi, mkashindane kwa akili, nguvu maarifa na nidhamu, kwani mchezaji mzuri ni yule ambaye anawasikiliza walimu na kutekeleza yale anavyoelezwa ili kufanikisha ushindi," amesema DED Makota. Afisa Elimu Msingi na Awali wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Darous Daudi Limandola amesema wanamichezo 60 wataiwakilisha Halmashauri hiyo kwenye ngazi ya Mkoa wa Manyara. Limandola amesema wanamichezo hao ni timu iliyosheheni hivyo wanatarajia watarudi na ushindi katika miche...

TANZANIA YAIMARISHA TAHADHARI DHIDI YA MLIPUKO WA EBOLA.

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  NAIBI Waziri wa Afya Mheshimiwa. Dkt. Florence Samizi amesema Tanzania imeendelea na hatua za kuzuia na kuimarisha utayari dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola unaosababishwa na virusi vya Bundibugyo unaoendelea katika nchi za Jamhuri ya Demokrasia Kongo na Uganda, huku akisisitiza mshikamano wa kikanda na umuhimu wa ushirikiano wa pamoja katika kulinda usalama wa afya wa wananchi. Dkt. Samizi amesema hayo leo Mei 26, 2026 kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati wa mjadala kuhusu mlipuko wa Ebola katika nchi hizo, ulioandaliwa jijini Brazzaville, Jamhuri ya Kongo, ambapo ameshiriki kwa njia ya mtandao akiwa katika ofisi za Wizara jijini Dodoma. Katika mjadala huo, Tanzania imeeleza mshikamano wake na Serikali pamoja na wananchi wa DRC na Uganda kufuatia mlipuko huo, huku ikitoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao pamoja na wahudumu wa afya waliopo mstari wa mbele wakitoa huduma. Aidha Dkt. Samizi amesema Tanzania inatambu...

JMAT: TANZANIA HAINA UBAGUZI WA KIDINI

Picha
  Na Lubango Mleka, Dodoma.  KATIBU wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Askofu Israel Maasa, amesema kwa zaidi ya nusu karne Watanzania wa dini zote wamekuwa wakiishi kwa upendo, mshikamano na kuheshimiana bila kujali tofauti zao za kiimani. Askofu Maasa amesema Tanzania imeendelea kuwa mfano wa amani, umoja na uhuru wa kuabudu kwa dini zote bila ubaguzi wowote, hali iliyosaidia kudumisha mshikamano wa kitaifa kwa miaka mingi. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, alisema jumuiya hiyo imesikitishwa na taarifa zilizotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania zinazodai kuwepo kwa ubaguzi wa kidini nchini. Alisema taarifa hizo, ambazo zinadaiwa kuungwa mkono na baadhi ya wabunge pamoja na Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la Marekani, haziakisi hali halisi ya Tanzania na zimewasikitisha pamoja na kuwafedhehesha wananchi. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa JMAT, Alihadi Mussa Salum, amesema hakuna kundi lolote nchini linalonyimwa uhuru wa kuabudu au kuumizw...

RUVUMA YAPOKEA MAJIKO BANIFU 7,648 KWA BEI YA RUZUKU.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Songea- Ruvuma. MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Mheshimiwa Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed, leo Mei 25, 2026 amepokea rasmi mradi wa uuzaji na usambazaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kupitia kampuni ya Burn Manufacturing Company Limited. Mradi huo unalenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kupitia usambazaji wa majiko banifu yenye teknolojia ya kisasa kwa gharama nafuu kutokana na ruzuku inayotolewa na Serikali. Akizungumza wakati wa kupokea mradi huo, Mkuu wa Mkoa ameipongeza REA kwa kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya nishati safi ya kupikia nchini, akieleza kuwa majiko banifu yana mchango mkubwa katika kuboresha afya za wananchi pamoja na kulinda mazingira. Amesema matumizi ya majiko hayo yatasaidia kupunguza athari zinazotokana na matumizi ya kuni na mkaa usio salama, ikiwemo moshi unaosababisha madhara ya kiafya kwa watumiaji, hususan wanawake na watoto. Mheshi...