CCM YAIPONGEZA FRANONE KWA CSR YA ZAHANATI
Na Mwandishi wetu, Mirerani. CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeipongeza kampuni ya Franone Mining & Gem LTD, inayochimba madini ya Tanzanite kitalu C kwa kujenga zahanati ndani ya eneo tengefu la Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, kupitia mpango wa uwajibikaji kwa jamii (CSR). Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenan Laban Kilongozi akizungumza baada ya kukagua ujenzi unaoendelea wa zahanati hiyo ameipongeza kampuni ya Franone kwa kujitoa kwa ajili ya wachimbaji na wadau wa madini. Amesema zahanati hiyo ikikamilika itakuwa inatoa huduma za afya kwa wachimbaji na wadau wa madini ya Tanzanite hivyo ni jambo la kiungwana na la kuungwa mkono. "Nawakupongeza kampuni ya Franone Mining & Gem LTD kwa ujenzi wa zahanati hii, Mkurugenzi Onesmo Mbise hongereni sana, endelea kutoa kwa jamii kwani hautapungukiwa ila utazidi kuongezewa," amesema Kenani. Hata hivyo, Kenani amewaasa wadau wengine wa madini kuiga mfano kwa kampuni ya Franone Mining LTD, kat...