WATUHUMIWA MAUAJI YA BODABODA TABORA WAKAMATWA
Na Allan Kitwe, Tabora. JESHI la Polisi Mkoani Tabora linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za ujambazi na mauaji ya waendesha bodaboda yaliyokuwa yakiripotiwa mara kwa mara katika maeneo mbalimbali Mkoani hapa. Hayo yamebainishwa jana na Mkuu wa Mkoa Paul Matiko Chacha alipokuwa akizungumza na Wadau wa Maendelea na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa. Amesema kuwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na operesheni maalum iliyofanywa na askari wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa kwa kushirikiana na Vyombo Vingine vya Ulinzi na Usalama. Amedokeza kuwa msako huo ulilenga kunasa wahalifu wote waliokuwa wakijihusisha na vitendo hivyo ambavyo vimekuwa vikisababisha taharuki kubwa miongoni mwa jamii na hususan waendesha bodaboda. ‘Kukamatwa watuhumiwa hawa ni hatua moja, uchunguzi bado unaendelea ili kubaini mtandao mzima na kukamata wahusika wote ili kukomesha tabia hii na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wahusika wote’, ameeleza. Aidha ameongeza kuwa watu wengine wawil...