Machapisho

RAIS DKT MWINYI: SMZ KUIMARISHA USAFIRI NA USAFIRISHAJI WA MIZIGO PEMBA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali imejipanga kikamilifu kumaliza tatizo la usafiri na usafirishaji wa mizigo katika Kisiwa cha Pemba. Akizungumza leo tarehe 17 Februari 2026 wakati wa ufunguzi wa Msikiti mpya wa Chachani, uliopo Chake Chake, Mkoa wa Kusini Pemba uliojengwa na mfanyabiashara Ndg. Said Nassor Bopar, Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali imeandaa meli mbili za mwendo kasi na ipo katika hatua za kutafuta meli maalum ya mizigo kwa safari za Unguja na Pemba. Aidha, ameeleza kuwa Serikali imeliagiza Shirika la Meli la Zanzibar kuimarisha huduma zake na kubainisha kuwa meli ya MV Mapinduzi II itaanza kazi hivi karibuni baada ya matengenezo. Ameongeza kuwa uimarishaji wa bandari za Pemba utahamasisha sekta binafsi kuongeza vyombo vya usafiri. Rais Dkt. Mwinyi amewahimiza waumini kuitumia misikiti kujadili changamoto za kijamii, akiwapongeza wafadhili wa msikiti huo kwa mcha...

KIHONGOSI AKAGUA UTEKELEZAJI MIRADI YA BIL 2.5 NZEGA

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora.  KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) anayesimamia Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi ameeleza kufurahishwa na kazi nzuri ya utekelezaji miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Nzega Mkoani hapa. Akiwa katika siku ya pili ya ziara yake, Kihongosi ametembelea na kukagua utekelezaji miradi yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 2.5 iliyotekelezwa na serikali ya Awamu ya Sita katika Majimbo matatu ya Wilaya ya Nzega. Mradi wa kwanza aliotembelea ni wa ujenzi wa mabweni 2 ya wanafunzi wa kike na kiume katika shule ya sekondari Puge, ujenzi wa vyumba 6 vya madarasa na matundu 10 ya vyoo, vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 450. Amebainisha kuwa ujenzi wa miundombinu hiyo ambayo imefadhiliwa na Kampuni ya Barrick ni kichocheo muhimu sana cha kuinua ya taaluma katika shule hiyo, hivyo akatoa wito kwa walimu na wanafunzi kutumia vizuri miundombinu hiyo. Mradi mwingine ni ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Nzega uliogharimu za...

WATANZANIA TUNA WAJIBU WA KULINDA NCHI NA RASILIMALI ZAKE-WAZIRI KATAMBI

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Tanga.  WAZIRI wa Mambo ya Ndani Nchi, Mhe. Patrobas Katambi amesisitiza na kuwakumbusha Watanzania kuwa wanawajibika katika kulinda nchi na rasilimali za Tanzania pamoja na kuhakikisha Tanzania inaendelea kubakia salama na yenye amani kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa na ustawi wa jamii na kila Mtanzania. Waziri Katambi amebainisha hayo Mkoani Tanga wakati wa muendelezo wa ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akisisitiza kuwa bila amani na usalama hakuna shughuli yoyote ya kijamii ama kiuchumi inayoweza kuendelea. "Niwakumbushe Watanzania wenzangu kwamba sisi wote Watanzania tunao wajibu wa kuilinda nchi yetu. Jukumu la ulinzi na usalama wa rasilimali, raia wote ni wajibu wetu sote. Haya yote hayawezekani pia kama hakuna usalama kwani kupoteza usalama maana yake hakuna ulinzi, hakuna amani na kama hakuna amani hakuna shughuli  yoyote inayoweza kuendelea." "Leo tupo hapa tuna amani kwasababu ha...

MBUNGE AGNES MARWA ATOA SADAKA MAALUM KUUNGA MKONO MAANDALIZI YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Musoma.  MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Agnes Marwa, leo ametoa sadaka maalum kwa viongozi wa dini ya Kiislamu katika Misikiti tofauti ya Musoma Mjini ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono maandalizi ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Sadaka hiyo imelenga kuwasaidia viongozi wa dini pamoja na waumini katika kujiandaa na mwezi huo muhimu wa ibada, unaoheshimiwa na Waislamu duniani kote. Baadhi ya vitu vilivyotolewa ni pamoja na buswati, tende, kanzu, balaghashee pamoja na fedha taslimu, ambavyo vimekabidhiwa kwa viongozi kutoka misikiti mbalimbali ya Musoma Mjini. Akizungumza wakati wa tukio hilo, Agnes Marwa alisema kuwa sadaka hiyo ni ishara ya mshikamano, upendo na heshima kwa viongozi wa dini, pamoja na kuthamini mchango wao katika kujenga maadili mema na amani ndani ya jamii. “Nimeona ni muhimu kushiriki na ndugu zetu wa Kiislamu katika maandalizi ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Huu ni mwezi wa ibada, subira, na kusaidiana, hivyo ni wajibu wetu kama viongozi kuende...

WATU WAWILI WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MWENYEKITI WA CCM TAWI LA ITUMBI MBEYA.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Mbeya.  KUPITIA mitandao ya kijamii kunasambazwa picha mjongeo akionekana mtu mmoja mwanaume ambaye anajinasibu kuhusika katika tukio la mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Tawi la Itumbi aitwaye Elia Richard Sambala, miaka 53, mkazi wa Itumbi Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya. Ukweli ni kwamba, Februari 11,2026 saa 7 mchana katika Kijiji cha Itumbi, Elia Richard Sambala, alikutwa shambani kwake akiwa amejeruhiwa kwa kukatwa na kitu chenye makali kichwani na watu wasiojulikana na alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitali ya Wilaya ya Chunya kwa matibabu. Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, kupitia Askari wa kuchunguza matukio ya mauaji, walianza msako mkali na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili kuhusiana na tukio hilo na ufuatiliaji zaidi kwa wengine waliohusika unaendelea. Uchunguzi wa awali umebaini kuwa, chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa masilahi wa eneo la uchimbaji madini ya dhahabu ambapo mmoja wa wanafamilia hao alikodi...

MATUMIZI YA KONDOMU YASHUKA KWA ASILIMIA TANO: KENGELE YA TAHADHARI KWA TAIFA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  WAKATI  dunia ikiendelea kupaza sauti kuhusu umuhimu wa kinga dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na magonjwa ya zinaa, takwimu zinaonesha kuwa matumizi ya kondomu nchini yameshuka kwa takribani asilimia tano.  Hii si namba ya kupuuzwa ni ishara inayopaswa kuamsha mjadala mpana na hatua za haraka katika kulinda afya ya jamii. Kupungua huku kunakuja licha ya kampeni za muda mrefu za uhamasishaji na upatikanaji wa kondomu katika vituo vya afya na maeneo mbalimbali ya umma.  Je, tatizo ni nini? Je, ni uchovu wa kampeni, kuongezeka kwa dhana potofu, au kupungua kwa hofu ya maambukizi kutokana na maendeleo ya tiba? Baadhi ya wananchi wa Dodoma wanasema bado kuna pengo la elimu sahihi kuhusu matumizi ya kondomu. Ingawa asilimia hiyo inaweza kuonekana ndogo kwa mtazamo wa haraka, kwa tathmini ya afya ya umma ni takwimu yenye uzito mkubwa.  Kupungua huku kunamaanisha kuwa watu zaidi wako katika hatari ya kuambukizwa au wanawake ku...

POLISI YAWASAKA "WALIOMVUTISHA" SIGARA MTOTO, KUMREKODI NA KUSAMBAZA MTANDAONI

Picha
Na Hamida Ramadhan, Dodoma.  MSEMAJI wa Jeshi la Polisi Tanzania Naibu Kamishna wa Polisi DCP David Misime leo Jumapili Februari 15, 2026  amesema Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi na kuwafuatilia watu ambao wamesikika kwenye Kipande cha Video kilichosambaa kwenye Mitandao ya Kijamii, wakimuhamasisha mtoto mdogo wa kiume kuvuta sigara kwani kitendo hicho ni kinyume na sheria, kanuni na taratibu za kijamii. Taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya habari na Msemaji huyo wa Polisi imesema uchunguzi utakapokamilika hatua za kisheria zitachukuliwa, akitoa wito kwa yeyote anayewafahamu watu hao au mtoto huyo kulisaidia Jeshi la Polisi ili kuwafikia na kuokoa afya ya mtoto huyo aliyehamasishwa kuvuta sigara. "Tunatoa onyo pia kwa watu wenye tabia za kufanya vitendo vya kikatili na vya unyanyasaji kama hivyo na vinavyofanana na hivyo kwa watoto kwa lengo lolote lile." Imesema taarifa ya Polisi. Kulingana na Polisi Makao Makuu, Dodoma, wapo wanaofanya hivyo kwa watoto wadogo kwa msukumo w...

WATENDAJI SOKO LA HISA DSE WATAKIWA KUWA WABUNIFU KUVUTIA WAWEKEZAJI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) Bw. Peter Nalitolela, mazungumzo yaliyofanyika leo tarehe 13 Februari 2026, Dodoma. Katika Mazungumzo hayo, Makamu wa Rais amewahimiza watendaji DSE kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuwa wabunifu katika masuala ya masoko na kuendelea kuvutia uwekezaji. Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) Bw. Peter Nalitolela, ameahidi kuendelea kushirikiana vema na Serikali katika kutafuta mitaji ili kuweza kusaidia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ya kufikia uchumi wa Dola za Marekani Trilioni Moja ifikapo 2050. Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ni taasisi ya kimkakati ya Taifa inayowezesha ukusanyaji na usimamizi wa mitaji ya muda mrefu kwa ajili ya kufadhili maendeleo ya uchumi wa Tanzania. DSE ni jukwaa rasmi linalowawezesha wawekezaji wa ndani na ...