NDUGU WASHIKILIWA KWA KUMUUA SHEMEJI YAO 'KISA MGOGORO WA MASHAMBA'
Na Mwandishi Wetu, Mbeya. JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia ndugu wa familia moja ambao ni Solomon Mwambyale (68) na watoto wake wawili, Stephano Mwaisango (32) na Emmanuel Mwaisango (36), kwa tuhuma za mauaji ya Jenti Segelela (87) ambaye alikuwa shemeji yake na mtuhumiwa Solomon, wakidaiwa kumkata na kitu chenye ncha kali kisogoni na kisha kukimbia, chanzo kikiwa ni mgogoro wa mashamba ya ukoo na tamaa ya kujipatia mali kwa njia isiyo halali. Katika tukio la Pili, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga amesema wanamshikilia Bw. Charles Oden Mwakasege (32) fundi simu Mkazi wa Meta Jijini Mbeya na Bw. Isack Charles 'Bebwa' mkazi wa Shewa, kwa tuhuma za kuingilia mfumo wa kibiashara wa makampuni ya ukopeshaji wa simu. Kulingana na Kamanda Kuzaga katika taarifa yake ya leo Jumanne Februari 10, 2026 kwa Vyombo vya habari, watuhumiwa hao walikamatwa katika msako uliofanyika kuanzia Januari 27, 2026 katika maeneo mba...