Machapisho

WIZARA YA VIJANA NA MICHEZO YAIMARISHA USHIRIKIANO WA TIBA YA MICHEZO NA TANZANIA

Picha
Na Lubango Mleka. WIZARA ya Vijana na Michezo katika kusaidia na kuendeleza mfumo wa tiba ya michezo,  chini ya ufadhili wa Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, na usimamizi wa Kamati Kuu ya Tiba ya Wizara, inayoongozwa na Profesa Dkt. Hazem Khamis, Kituo cha Olimpiki cha Maadi kimepokea ujumbe kutoka Taasisi ya Moyo ya Tanzania (JKCI) katika ziara maalum. Ujumbe huo umejumuisha Mkurugenzi  wa Hospitali ya JKCI, Dar Group Dkt. Tulizo Shemu , Dkt. Tatizo Waane, Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa ya Moyo JKCI na Dkt. Eva Michel, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa Watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete JKCI. Ziara hiyo iliandaliwa kwa ushirikiano na uratibu na Jumuiya ya Misri na Afrika ya Utafiti na Magonjwa ya Moyo, inayoongozwa na Profesa Dkt. Ahmed Ashraf Issa; Jumuiya ya Kiarabu - Ushirikiano wa Afrika, inayoongozwa na Balozi Mohamed Lagouzi; na Chama cha "Kutoka Moyoni hadi Moyoni", kinachoongozwa na Profesa Dkt. Ghada Qazamel. Ujumbe huo pia ulijumuisha ...

FCC, ZFCC ZAJADILI UIMARISHAJI WA USHINDANI WA BIASHARA NA KUMLINDA MLAJI

Picha
Na Mwandishi wetu. KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), Bi. Khadija Ngasongwa, amefanya ziara ya kikazi katika Tume ya Ushindani Halali wa Biashara Zanzibar (ZFCC) ikiwa ni hatua ya kuimarisha mashirikiano kati ya taasisi hizo mbili katika masuala ya ushindani, ulinzi wa mlaji na udhibiti wa bidhaa bandia. Bi. Ngasongwa alipokelewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ZFCC, Bi. Aliya Juma ambapo viongozi hao walifanya mazungumzo kuhusu kuendeleza ustawi wa taasisi hizo na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao. Akizungumza katika ziara hiyo iliyofanyika tarehe 14 Januari, 2026 katika ofisi za ZFCC - Zanzibar, Bi. Ngasongwa alisema ushirikiano kati ya taasisi hizo unaendelea kuimarika kupitia utekelezaji wa Hati ya Makubaliano (MoU) yaliyokwisha sainiwa. "FCC na ZFCC tayari zimeanza kutekeleza kwa vitendo maeneo ya ushirikiano ikiwemo kujengeana uwezo, kubadilishana uzoefu na kufanya ukaguzi wa pamoja ili kudhibiti bidhaa bandia na kulinda haki za watumiaji wa bidh...

WANASWA KWA KUHUJUMU MRADI WA MAJI WA MIJI 28

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora. WATU wanne wamekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Tabora kwa tuhuma za kuhujumu Mradi wa Maji wa Miji 28 unaoendelea kutekelezwa na serikali katika Wilaya za Sikonge, Urambo na Kaliua ili kumaliza kero ya wananchi. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani hapa ACP Constatine Mbogambi amethibitisha kukamatwa watuhumiwa hao wakiwa na vifaa mbalimbali vilivyoibiwa kwenye mradi huo Wilayani Urambo. Ametaja baadhi ya vifaa vilivyokamatwa kuwa ni mashine kubwa 3 za kuchomelea mabomba, grenda mashine 2 za kukatia mabomba, nyaya 9 za kuunganishia grenda hizo na lita 40 za mafuta ya mitambo ya hydroliki. Kamanda amefafanua kuwa vifaa hivyo viliibiwa usiku wa tarehe 11 Januari 2026 Wilayani Urambo katika eneo la mradi huo mkubwa wa maji kutoka ziwa Victoria ambao unatekelezwa na serikali kwa gharama ya zaidi ya sh bil 143. ‘Baada ya kuibiwa mashine na vifaa hivyo, vilisafirishwa na kwenda kufichwa katika Kitongoji cha Ubalani-Majengo, Mjini Urambo tayari kwa ajili ya kutafuta ...

MAMA AJIFUNGUA NA KUTELEKEZA KICHANGA GESTI

Picha
  Na Allan Kitwe, Nzega. MWANAMKE mmoja ambaye jina halijajulikana amejifungua mtoto na kumtelekeza kwenye nyumba ya kulala wageni (gesti) Wilayani Nzega Mkoani Tabora na kutokomea kusikojulikana. Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Mkuu wa Wilaya hiyo Naitapwak Tukai ameeleza kusikitishwa na tukio hilo na kuahidi kutoa donge nono la shilingi 500,000 kwa mtu yeyote atakayesaidia kupatikana mwanamke huyo. Alieleza kuwa kitendo hicho hakikubaliki katika jamii na ni ukatili wa hali ya juu, kama huyo mama aliweza kukaa na mimba kwa miezi yote tisa na kujifungua salama iweje amtupe mtoto gesti?, alihoji. ‘Naomba mtu yeyote mwenye taarifa za mwanamke aliyekuwa mjamzito na sasa haonekani kuwa na mtoto atoe taarifa Kituo cha Polisi au aje kwa Mkuu wa Wilaya moja kwa moja anipe taarifa, hatutamtaja kokote’, alisema. DC alibainisha kuwa mtoto anakadiriwa kuwa na umri wa siku 3 tu tangu azaliwe, hivyo kumtelekeza namna hii ni kumnyima haki yake ya msingi ya kunyonya maziwa ya mama, kupata m...

KAPINGA AWASHUKURU WANANCHI KATA YA MKAKO NA KIHANGIMAHUKI, AHAHIDI USHIRIKIANO WA KARIBU KUTATUA CHANGAMOTO ZAO.

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Mbinga. MBUNGE wa Jimbo la Mbinga Vijijini na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Salvio Kapinga, ametembelea Kata za Mkako na Kihangimahuka katika mwendelezo wa ziara yake ya kuwashukuru wananchi kwa ushindi mkubwa waliompatia yeye na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025. Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Lihale, Mhe. Kapinga aliahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali ya Wilaya pamoja na taasisi husika ili kutatua changamoto zinazowakabili wananchi, hususan katika sekta za miundombinu, maji na umeme. “Serikali ipo pamoja nanyi, na mimi kama Mbunge wenu nitaendelea kushirikiana na viongozi wa wilaya na taasisi zote kuhakikisha changamoto zenu zinapatiwa ufumbuzi wa kudumu". Katika kuonesha dhamira yake ya kuunga mkono maendeleo ya elimu, Mhe. Kapinga alitoa msaada wa bati 50 za geji 28 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 1.7 pamoja na kiasi cha shilingi laki tano kwa ajili ya ununuzi wa kenchi...

DAWA NA VIFAA TIBA VYA MIL 822.8 VYAKAMATWA TABORA

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora . MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Magharibi imefanya oparesheni maalumu na kufanikiwa kukamata dawa zenye thamani ya sh mil 822.8 zilizokuwa zinauzwa kinyume na utaratibu.   Hayo yamebainishwa jana na Meneja wa TMDA Kanda ya Magharibi, Christopher Migoha alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, ambapo alieleza kuwa jumla ya kilo 2,300 zenye thamani ya shilingi mil 822.8 zimekamatwa na kuteketezwa. Amefafanua kuwa dawa na vifaa tiba hivyo vimekamatwa katika oparesheni maalumu iliyofanyika katika hospitali, vituo vya afya, zahanati na maduka ya dawa baridi za binadamu na mifugo katika Wilaya zote. Migoha ameeleza kuwa dawa hizo haziruhusiwi kuuzwa katika maduka ya watu binafsi na ni kinyume cha sheria na kanuni ya 63 ya mwaka 2005 ya dawa zilizozuiliwa kuuzwa hadharani hususani katika maduka ya watu binafsi. Ameongeza kuwa katika operesheni hiyo walikagua jumla ya maduka 408 ya dawa, Hospital 16, vituo vya afya 17, zahanati 17, famas...

GOD MWANGA ATENGENEZA BARABARA 23 KWA GHARAMA ZAKE

Picha
  Na Mwandishi wetu, Moshi. MCHIMBAJI maarufu wa madini mbalimbali nchini God Mwanga amejitolea na kufanikisha ujenzi wa barabara tofauti 23 katika eneo la Mwika Kirueni, Wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro. Mchungaji mstaafu John Mlay ameyasema hayo wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa 2026 zilizofanyika nyumbani kwa ukoo wa mzee Mathayo Mwanga katika eneo la Mwika Kirueni. Mchungaji Mlay ameeleza kwamba Mkurugenzi wa kampuni ya God Charity, Godlisten Mwanga amekuwa baraka kwa wakazi wa eneo hilo na kutengeneza barabara hizo kwa gharama zake mwenyewe. "Huyu baba amefanya jambo jema kwani ametumia magari na mitambo yake binafsi na kutengeneza barabara 23 kwa gharama zake mwenyewe," amesema Mchungaji Mlay. Amesema barabara hizo 23 zilikuwa na changamoto ya ubovu na hasa wakati mvua zikinyesha zinapitika kwa shida mno ila baada ya kutengenezwa hivi sasa hazina shida. "Hivi sasa barabara hizi zinapitika kwa urahisi mno baada ya God Mwanga kufanya kazi hiyo kubwa ya...

ALIYEKUWA DED SIMANJIRO ASHINDA KESI YA PILI

Picha
  Na Mwandishi wetu, Simanjiro ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Samwel Warioba Gunza ameachiwa huru na mahakama kwenye kesi ya rushwa ya shilingi milioni 5 na matumizi mabaya ya madaraka. Hata hivyo, aliyekuwa DED huyo wa Simanjiro, Gunza hakuwepo mahakamani kwani yupo magereza bado anatumikia kifungo cha miaka 20 jela kwa kesi nyingine ya rushwa alipohukumiwa mwaka 2025. Katika kesi hiyo, Gunza alifikishwa mbele ya hakimu mwandamizi wa mahakama ya wilaya ya Simanjiro, Onesmo Nicodemo na kusomewa shitaka na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU). Katika hukumu ya shauri hilo la uhujumu uchumi lililosomwa kwenye mahakama hiyo iliyopo mji mdogo wa Orkesumet, Gunza hakukutwa na hatia. Hakimu Nicodemo akisoma hukumu hiyo ameieleza  mahakama hiyo kuwa hakukuwa na ushahidi usiokuwa na mashaka wenye kumtia hatiani mshtakiwa huyo, katika makosa mawili ya rushwa  na kutumia madaraka vibaya. Amesema katika shtaka la kw...

WATU SITA WAKAMATWA KWA UTEKAJI NA MAUAJI YA BODABODA

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora JESHI la Polisi Mkoani Tabora linawashikiria watu sita kwa tuhuma za kuteka na kuua mwendesha bodaboda Hamis Nchambi (27) msukuma, mkazi wa Kata ya Mbugani katika halmashauri ya manispaa ya Tabora. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, ACP Constantine Mbogambi amethibitisha kukamatwa watuhumiwa hao kutokana na msako mkali uliofanywa na Polisi katika maeneo mbalimbali baada ya kupokea taarifa za mauaji hayo. Kamanda Mbogambi ameeleza kuwa watuhumiwa hao walitumia mbinu ya mmoja wao kujifanya abiria na kukodi pikipiki hiyo siku ya tarehe 13 Januari 2026 majira ya saa 2 usiku ili impeleke nyumbani kwake. Amefafanua kuwa walipofika eneo la makaburi ya Miemba katika manispaa hiyo ghafla walimteka na kumfunga kamba shingoni, mikononi na miguuni na kisha kumnyonga ili kujipatia kipato kisicho halali. Mwili wa marehemu ulipatikana kesho yake siku ya tarehe 14 Januari 2026 majira ya saa 9.30 alasiri katika eneo la makaburi hayo, katika Kata ya Miemba, ukiwa umefungwa...

KAPINGA, LONDO WAANZA SAFARI YA KUIMARISHA SEKTA YA VIWANDA NA BIASHARA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma. WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Kapinga (Mb), ameongoza watumishi wa Wizara hiyo kumpokea Naibu Waziri mpya, Mhe. Denis Londo (Mb), huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa karibu katika kutekeleza majukumu ya wizara kwa maslahi mapana ya Taifa. Akizungumza Januari 15, 2026 katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma, Mhe. Kapinga ameahidi kumpa ushirikiano wa kutosha Naibu Waziri Londo na kuelekeza Menejimenti pamoja na Watumishi wa Wizara kushirikiana kwa karibu ili kufanikisha malengo waliyojiwekea katika kuendeleza sekta ya viwanda na biashara nchini. “Ninawahimiza Menejimenti na watumishi wote kushirikiana kikamilifu na Naibu Waziri ili kwa pamoja tuweze kutimiza majukumu yetu kwa ufanisi na kufikia malengo ya Wizara kwa maslahi ya Taifa,” amesema Mhe. Kapinga. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Denis Londo (Mb), amesema kazi iliyo mbele yao ni kubwa na kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Sulu...

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA WIZARA YA VIWANDA KWA KUENDELEZA KONGANI NA KUSIMAMIA MIRADI YA KIMKAKATI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma. MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Mhe. Deodatus Mwanyika, ameipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara kwa hatua inazoendelea kuchukua katika kuanzisha na kuendeleza kongani za viwanda kupitia taasisi zake, hatua inayochochea fursa za ajira na ukuaji wa uchumi nchini. Akizungumza katika kikao cha kwanza cha Kamati hiyo cha kupokea taarifa ya wizara kuhusu muundo, majukumu, sera na sheria kilichofanyika Januari 15, 2026 Bungeni jijini Dodoma, Mhe. Mwanyika,amesema  usimamizi madhubuti wa Wizara katika miradi ya kimkakati na miradi kielelezo kuwa kinaonyesha dhamira ya dhati ya serikali kubadili sura ya sekta ya viwanda.   “Miradi hiyo inapaswa kutekelezwa mapema iwezekanavyo kwa kuwa ina mchango muhimu katika kuongeza ajira, kukuza pato la taifa na kuimarisha uchumi wa viwanda kwa ujumla.”amesema Mhe.Mwanyika. Aidha, ameisisitiza Wizara kuendelea kuboresha sera na sheria ili ziendane na Dira ya Taifa ya Maend...