Machapisho

DAWA NA VIFAA TIBA VYA MIL 822.8 VYAKAMATWA TABORA

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora . MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Magharibi imefanya oparesheni maalumu na kufanikiwa kukamata dawa zenye thamani ya sh mil 822.8 zilizokuwa zinauzwa kinyume na utaratibu.   Hayo yamebainishwa jana na Meneja wa TMDA Kanda ya Magharibi, Christopher Migoha alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, ambapo alieleza kuwa jumla ya kilo 2,300 zenye thamani ya shilingi mil 822.8 zimekamatwa na kuteketezwa. Amefafanua kuwa dawa na vifaa tiba hivyo vimekamatwa katika oparesheni maalumu iliyofanyika katika hospitali, vituo vya afya, zahanati na maduka ya dawa baridi za binadamu na mifugo katika Wilaya zote. Migoha ameeleza kuwa dawa hizo haziruhusiwi kuuzwa katika maduka ya watu binafsi na ni kinyume cha sheria na kanuni ya 63 ya mwaka 2005 ya dawa zilizozuiliwa kuuzwa hadharani hususani katika maduka ya watu binafsi. Ameongeza kuwa katika operesheni hiyo walikagua jumla ya maduka 408 ya dawa, Hospital 16, vituo vya afya 17, zahanati 17, famas...

GOD MWANGA ATENGENEZA BARABARA 23 KWA GHARAMA ZAKE

Picha
  Na Mwandishi wetu, Moshi. MCHIMBAJI maarufu wa madini mbalimbali nchini God Mwanga amejitolea na kufanikisha ujenzi wa barabara tofauti 23 katika eneo la Mwika Kirueni, Wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro. Mchungaji mstaafu John Mlay ameyasema hayo wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa 2026 zilizofanyika nyumbani kwa ukoo wa mzee Mathayo Mwanga katika eneo la Mwika Kirueni. Mchungaji Mlay ameeleza kwamba Mkurugenzi wa kampuni ya God Charity, Godlisten Mwanga amekuwa baraka kwa wakazi wa eneo hilo na kutengeneza barabara hizo kwa gharama zake mwenyewe. "Huyu baba amefanya jambo jema kwani ametumia magari na mitambo yake binafsi na kutengeneza barabara 23 kwa gharama zake mwenyewe," amesema Mchungaji Mlay. Amesema barabara hizo 23 zilikuwa na changamoto ya ubovu na hasa wakati mvua zikinyesha zinapitika kwa shida mno ila baada ya kutengenezwa hivi sasa hazina shida. "Hivi sasa barabara hizi zinapitika kwa urahisi mno baada ya God Mwanga kufanya kazi hiyo kubwa ya...

ALIYEKUWA DED SIMANJIRO ASHINDA KESI YA PILI

Picha
  Na Mwandishi wetu, Simanjiro ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Samwel Warioba Gunza ameachiwa huru na mahakama kwenye kesi ya rushwa ya shilingi milioni 5 na matumizi mabaya ya madaraka. Hata hivyo, aliyekuwa DED huyo wa Simanjiro, Gunza hakuwepo mahakamani kwani yupo magereza bado anatumikia kifungo cha miaka 20 jela kwa kesi nyingine ya rushwa alipohukumiwa mwaka 2025. Katika kesi hiyo, Gunza alifikishwa mbele ya hakimu mwandamizi wa mahakama ya wilaya ya Simanjiro, Onesmo Nicodemo na kusomewa shitaka na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU). Katika hukumu ya shauri hilo la uhujumu uchumi lililosomwa kwenye mahakama hiyo iliyopo mji mdogo wa Orkesumet, Gunza hakukutwa na hatia. Hakimu Nicodemo akisoma hukumu hiyo ameieleza  mahakama hiyo kuwa hakukuwa na ushahidi usiokuwa na mashaka wenye kumtia hatiani mshtakiwa huyo, katika makosa mawili ya rushwa  na kutumia madaraka vibaya. Amesema katika shtaka la kw...

WATU SITA WAKAMATWA KWA UTEKAJI NA MAUAJI YA BODABODA

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora JESHI la Polisi Mkoani Tabora linawashikiria watu sita kwa tuhuma za kuteka na kuua mwendesha bodaboda Hamis Nchambi (27) msukuma, mkazi wa Kata ya Mbugani katika halmashauri ya manispaa ya Tabora. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, ACP Constantine Mbogambi amethibitisha kukamatwa watuhumiwa hao kutokana na msako mkali uliofanywa na Polisi katika maeneo mbalimbali baada ya kupokea taarifa za mauaji hayo. Kamanda Mbogambi ameeleza kuwa watuhumiwa hao walitumia mbinu ya mmoja wao kujifanya abiria na kukodi pikipiki hiyo siku ya tarehe 13 Januari 2026 majira ya saa 2 usiku ili impeleke nyumbani kwake. Amefafanua kuwa walipofika eneo la makaburi ya Miemba katika manispaa hiyo ghafla walimteka na kumfunga kamba shingoni, mikononi na miguuni na kisha kumnyonga ili kujipatia kipato kisicho halali. Mwili wa marehemu ulipatikana kesho yake siku ya tarehe 14 Januari 2026 majira ya saa 9.30 alasiri katika eneo la makaburi hayo, katika Kata ya Miemba, ukiwa umefungwa...

KAPINGA, LONDO WAANZA SAFARI YA KUIMARISHA SEKTA YA VIWANDA NA BIASHARA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma. WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Kapinga (Mb), ameongoza watumishi wa Wizara hiyo kumpokea Naibu Waziri mpya, Mhe. Denis Londo (Mb), huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa karibu katika kutekeleza majukumu ya wizara kwa maslahi mapana ya Taifa. Akizungumza Januari 15, 2026 katika Ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma, Mhe. Kapinga ameahidi kumpa ushirikiano wa kutosha Naibu Waziri Londo na kuelekeza Menejimenti pamoja na Watumishi wa Wizara kushirikiana kwa karibu ili kufanikisha malengo waliyojiwekea katika kuendeleza sekta ya viwanda na biashara nchini. “Ninawahimiza Menejimenti na watumishi wote kushirikiana kikamilifu na Naibu Waziri ili kwa pamoja tuweze kutimiza majukumu yetu kwa ufanisi na kufikia malengo ya Wizara kwa maslahi ya Taifa,” amesema Mhe. Kapinga. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Denis Londo (Mb), amesema kazi iliyo mbele yao ni kubwa na kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Sulu...

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA WIZARA YA VIWANDA KWA KUENDELEZA KONGANI NA KUSIMAMIA MIRADI YA KIMKAKATI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dodoma. MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Mhe. Deodatus Mwanyika, ameipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara kwa hatua inazoendelea kuchukua katika kuanzisha na kuendeleza kongani za viwanda kupitia taasisi zake, hatua inayochochea fursa za ajira na ukuaji wa uchumi nchini. Akizungumza katika kikao cha kwanza cha Kamati hiyo cha kupokea taarifa ya wizara kuhusu muundo, majukumu, sera na sheria kilichofanyika Januari 15, 2026 Bungeni jijini Dodoma, Mhe. Mwanyika,amesema  usimamizi madhubuti wa Wizara katika miradi ya kimkakati na miradi kielelezo kuwa kinaonyesha dhamira ya dhati ya serikali kubadili sura ya sekta ya viwanda.   “Miradi hiyo inapaswa kutekelezwa mapema iwezekanavyo kwa kuwa ina mchango muhimu katika kuongeza ajira, kukuza pato la taifa na kuimarisha uchumi wa viwanda kwa ujumla.”amesema Mhe.Mwanyika. Aidha, ameisisitiza Wizara kuendelea kuboresha sera na sheria ili ziendane na Dira ya Taifa ya Maend...

SERIKALI YASISITIZA MAADILI YA KAZI KWA WATUMISHI WA SERIKALI ZA MITAA

Picha
Na Hamida Ramadhan, Dodoma. WATUMISHI wa Serikali za Mitaa wametakiwa kuzingatia maadili ya kazi na utumishi wa Umma ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima inayosababisha kushambuliana au kurushiana maneno kati yao na Viongozi wakuu wa Serikali au Wanasiasa. Wito huo umetolewa Leo Januari 15,2026 na Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Deus Sangu, alipokuwa akizungumza jijini Dodoma katika Kikao cha 31 cha Baraza la Taifa la Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU). Amesema kuwa ili kuondokana na migogoro hiyo, kila mtumishi wa Umma anapaswa kuzingatia maadili ya kazi kwa kuepuka vitendo vya uongo, uzembe, pamoja na ubadhirifu wa fedha na mali za umma. Sangu ameeleza kuwa mikutano ya vyama vya wafanyakazi ni haki ya kikatiba na serikali imekuwa ikishirikiana na vyama hivyo katika kutatua migogoro, ikiwemo kuwatetea watumishi pale wanapotendewa kinyume cha maadili, kama vile kupewa lugha isiyo ya staha au kupewa miradi na kufany...

TANZANIA YASISITIZA UONGEZAJI THAMANI MADINI BARANI AFRIKA

Picha
Tanzania yajipanga kuwa kitovu cha  uongezaji thamani madini Afrika, yashauri kuhusu ushirikiano wa kikanda na kisekta. Na Mwandishi Wetu, Riyadh, Saudi Arabia. TANZANIA imetambua shughuli za uongezaji thamani madini kama nguzo muhimu ya kuleta maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii lengo kubwa ikiwa ni kuondokana na uuzaji na usafirishaji wa madini ghafi kwa nchi zinazozalisha madini mbalimbali Barani Afrika. Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dkt. Steven Kiruswa, wakati akizungumza kwenye Kongamano la Kimataifa la Madini lijukanalo kama Future Minerals Forum 2026 lililowakutanisha mawaziri, viongozi mashuhuri na wadau wa sekta ya madini kutoka zaidi ya nchi 100 ndani na nje ya Bara la Afrika.  Dkt. Kiruswa amesema kuwa, rasilimali madini ni moja ya utajiri mkubwa uliopo Barani Afrika hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuweka mkazo katika shughuli za uongezaji thamani madini ndani ya nchi za Afrika ambapo kama kila nchi itazingatia hilo itakuwa moja ya ufunguo wa ...

TASAC YAFANYA UKAGUZI CHUO KIPYA CHA MAFUNZO YA UBAHARIA

Picha
  Na Lubango Mleka, Dar Es Salaam. SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kupitia Mkurugenzi Mkuu ambae pia ni Msajili wa Mabaharia Bw. Mohamed Salum amefanya ukaguzi wa miundombinu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika Chuo cha Mafunzo ya Awali ya Ubaharia Cha Dar es Salaam - Dar es Salaam Maritime Training Academy (DMTA) kilichopo mtaa wa Nkurumah jijini Dar Es salaam. Aidha, chuo hicho kimeomba kupewa ithibati ya kufundisha kozi za awali za ubaharia (Basic Safety Training). Tasnia ya ubaharia nchini imepata msukumo mpya kwa sekta binafsi kuanzisha vyuo kwa ajili ya kuongeza ujuzi wa awali katika masuala ya usafiri majini.  Bw. Salum amesema kuwa, Tanzania kuna kundi kubwa la vijana ambao wakitumia fursa ya kujiunga na DMTA itasaidia kujenga safari mpya ya maisha yao.   “Tanzania tuna bahari na maziwa ambayo tukiyatumia vema yatachangia kuongeza ajira kwa vijana na kupunguza ukosefu wa ajira. Hongereni sana uongozi wa DMTA kwa kuanzisha chuo hiki, aidh...

SERIKALI YAAINISHA MKAKATI WA KUWAENDELEZA WACHIMBAJI WADOGO

Picha
  Kipaumbele kikubwa ni leseni za uchimbaji kwa wachimbaji wadogo, Waziri Mavunde aelezea mkakati wa kuwawezesha kimtaji, Kamati ya Bunge yaipongeza BoT kwa ununuzi wa tani 16.4 za dhahabu, Kamati yasisitiza kuongezwa kwa eneo la utafiti madini kutoka asilimia 16 ya sasa. Na Lubango Mleka, DODOMA. SERIKALI imeainisha mkakati mahsusi wa kuwaendeleza wachimbaji wadogo wa madini nchini, kwa kuweka kipaumbele katika utoaji wa leseni, upatikanaji wa mitaji, teknolojia, masoko ya uhakika pamoja na maeneo yenye taarifa za utafiti. Hayo yameelezwa na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, wakati wa kikao cha kwanza cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kilichofanyika leo Januari 15, 2025 katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma. Waziri Mavunde amesema kuwa shughuli zote za utafutaji, uchimbaji, uongezaji thamani na biashara ya madini zinatekelezwa kwa mujibu wa Sera ya Madini ya mwaka 2009 na Sheria ya Madini, Sura ya 123, kwa lengo la kuhakikisha wachimbaji wadogo...