ALIYEKUWA DED SIMANJIRO ASHINDA KESI YA PILI
Na Mwandishi wetu, Simanjiro ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Samwel Warioba Gunza ameachiwa huru na mahakama kwenye kesi ya rushwa ya shilingi milioni 5 na matumizi mabaya ya madaraka. Hata hivyo, aliyekuwa DED huyo wa Simanjiro, Gunza hakuwepo mahakamani kwani yupo magereza bado anatumikia kifungo cha miaka 20 jela kwa kesi nyingine ya rushwa alipohukumiwa mwaka 2025. Katika kesi hiyo, Gunza alifikishwa mbele ya hakimu mwandamizi wa mahakama ya wilaya ya Simanjiro, Onesmo Nicodemo na kusomewa shitaka na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU). Katika hukumu ya shauri hilo la uhujumu uchumi lililosomwa kwenye mahakama hiyo iliyopo mji mdogo wa Orkesumet, Gunza hakukutwa na hatia. Hakimu Nicodemo akisoma hukumu hiyo ameieleza mahakama hiyo kuwa hakukuwa na ushahidi usiokuwa na mashaka wenye kumtia hatiani mshtakiwa huyo, katika makosa mawili ya rushwa na kutumia madaraka vibaya. Amesema katika shtaka la kw...