GST NA CHUO KIKUU CHA GOETHE WAFANYA UTAFITI MLIMA OLDOINYO LENGAI
Na Mwandishi Wetu - Arusha. TAASISI ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kwa kushirikiana na wataalam wa jiosayansi kutoka Chuo Kikuu cha Goethe cha nchini Ujerumani wafanya utafiti wa jiosayansi katika Mlima Oldoinyo Lengai. Akielezea kuhusu utafiti huo, Mkurugenzi wa Huduma za Jiolojia GST, Dkt. Ronald Massawe amesema kuwa, Mlima Oldoinyo Lengai ni moja ya milima ya volkano ambayo ipo hai, lakini pia ni mlima pekee duniani ambao volkano yake inatoa lava ya aina ya “natrocarbonatite” ambapo lava hii inapokauka na kugeuka vumbi, huweza kuwa na madhara ya kiafya kwa binadamu na wanyama, hasa inapovutwa kupitia hewa. Akifafanua kuhusu malengo ya utafiti huo, Dkt. Massawe amesema kuwa, kulingana na mfumo wa kijiolojia ndani ya mlima, utafiti huo una malengo makubwa matatu ambayo ni: kuchunguza muundo wa ndani wa volkano, kubaini maeneo ya hifadhi ya magma na njia zake, pamoja na kutambua mabadiliko ya tabaka la miamba katika Ukanda wa Z...